Mithali 26 Swahili & English
Listen/Download AudioMithali 26 (Swahili) | Proverbs 26 (English) |
---|---|
Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu. Mithali 26:1 |
Like snow in summer, and as rain in harvest, So honor is not fitting for a fool. |
Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu. Mithali 26:2 |
Like a fluttering sparrow, Like a darting swallow, So the undeserved curse doesn't come to rest. |
Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu. Mithali 26:3 |
A whip for the horse, A bridle for the donkey, And a rod for the back of fools! |
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye. Mithali 26:4 |
Don't answer a fool according to his folly, Lest you also be like him. |
Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. Mithali 26:5 |
Answer a fool according to his folly, Lest he be wise in his own eyes. |
Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Mithali 26:6 |
One who sends a message by the hand of a fool Is cutting off feet and drinking violence. |
Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Mithali 26:7 |
Like the legs of the lame that hang loose: So is a parable in the mouth of fools. |
Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Mithali 26:8 |
As one who binds a stone in a sling, So is he who gives honor to a fool. |
Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Mithali 26:9 |
Like a thornbush that goes into the hand of a drunkard, So is a parable in the mouth of fools. |
Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao. Mithali 26:10 |
As an archer who wounds all, So is he who hires a fool Or he who hires those who pass by. |
Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Mithali 26:11 |
As a dog that returns to his vomit, So is a fool who repeats his folly. |
Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye. Mithali 26:12 |
Do you see a man wise in his own eyes? There is more hope for a fool than for him. |
Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Mithali 26:13 |
The sluggard says, "There is a lion in the road! A fierce lion roams the streets!" |
Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mithali 26:14 |
As the door turns on its hinges, So does the sluggard on his bed. |
Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mithali 26:15 |
The sluggard buries his hand in the dish. He is too lazy to bring it back to his mouth. |
Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu. Mithali 26:16 |
The sluggard is wiser in his own eyes Than seven men who answer with discretion. |
Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake. Mithali 26:17 |
Like one who grabs a dog's ears Is one who passes by and meddles in a quarrel not his own. |
Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Mithali 26:18 |
Like a madman who shoots firebrands, arrows, and death, |
Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu? Mithali 26:19 |
Is the man who deceives his neighbor and says, "Am I not joking?" |
Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. Mithali 26:20 |
For lack of wood a fire goes out; Without gossip, a quarrel dies down. |
Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. Mithali 26:21 |
As coals are to hot embers, And wood to fire, So is a contentious man to kindling strife. |
Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia pande za ndani za tumbo. Mithali 26:22 |
The words of a whisperer are as dainty morsels, They go down into the innermost parts. |
Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha. Mithali 26:23 |
Like silver dross on an earthen vessel Are the lips of a fervent one with an evil heart. |
Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Mithali 26:24 |
A malicious man disguises himself with his lips, But he harbors evil in his heart. |
Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Mithali 26:25 |
When his speech is charming, don't believe him; For there are seven abominations in his heart: |
Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. Mithali 26:26 |
His malice may be concealed by deception, But his wickedness will be exposed in the assembly. |
Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia. Mithali 26:27 |
Whoever digs a pit shall fall into it. Whoever rolls a stone, it will come back on him. |
Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu. Mithali 26:28 |
A lying tongue hates those it hurts; And a flattering mouth works ruin. |