Mithali 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mithali 20 (Swahili) Proverbs 20 (English)

Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima. Mithali 20:1

Wine is a mocker, and beer is a brawler; Whoever is led astray by them is not wise.

Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba; Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake. Mithali 20:2

The terror of a king is like the roaring of a lion: He who provokes him to anger forfeits his own life.

Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana. Mithali 20:3

It is an honor for a man to keep aloof from strife; But every fool will be quarreling.

Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu. Mithali 20:4

The sluggard will not plow by reason of the winter; Therefore he shall beg in harvest, and have nothing.

Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka. Mithali 20:5

Counsel in the heart of man is like deep water; But a man of understanding will draw it out.

Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata? Mithali 20:6

Many men claim to be men of unfailing love, But who can find a faithful man?

Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake. Mithali 20:7

A righteous man walks in integrity. Blessed are his children after him.

Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake. Mithali 20:8

A king who sits on the throne of judgment Scatters away all evil with his eyes.

Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu? Mithali 20:9

Who can say, "I have made my heart pure. I am clean and without sin?"

Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa Bwana. Mithali 20:10

Differing weights and differing measures, Both of them alike are an abomination to Yahweh.

Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili. Mithali 20:11

Even a child makes himself known by his doings, Whether his work is pure, and whether it is right.

Sikio lisikialo, na jicho lionalo, Bwana ndiye aliyeyafanya yote mawili. Mithali 20:12

The hearing ear, and the seeing eye, Yahweh has made even both of them.

Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Mithali 20:13

Don't love sleep, lest you come to poverty; Open your eyes, and you shall be satisfied with bread.

Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu. Mithali 20:14

"It's no good, it's no good," says the buyer; But when he is gone his way, then he boasts.

Dhahabu iko, na marijani tele; Lakini midomo ya maarifa ni kito cha thamani. Mithali 20:15

There is gold and abundance of rubies; But the lips of knowledge are a rare jewel.

Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni; Mtoze rehani aliye mdhamini wa wageni. Mithali 20:16

Take the garment of one who puts up collateral for a stranger; And hold him in pledge for a wayward woman.

Chakula cha uongo ni kitamu kwa mtu; Lakini halafu kinywa chake kitajaa changarawe. Mithali 20:17

Fraudulent food is sweet to a man, But afterwards his mouth is filled with gravel.

Kila kusudi huthibitika kwa kushauriana; Na kwa shauri la akili fanya vita. Mithali 20:18

Plans are established by advice; By wise guidance you wage war!

Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana. Mithali 20:19

He who goes about as a tale-bearer reveals secrets; Therefore don't keep company with him who opens wide his lips.

Amlaaniye babaye au mamaye, Taa yake itazimika katika giza kuu. Mithali 20:20

Whoever curses his father or his mother, His lamp shall be put out in blackness of darkness.

Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa. Mithali 20:21

An inheritance quickly gained at the beginning, Won't be blessed in the end.

Usiseme, Mimi nitalipa mabaya; Mngojee Bwana, naye atakuokoa. Mithali 20:22

Don't say, "I will pay back evil." Wait for Yahweh, and he will save you.

Vipimo mbalimbali ni chukizo kwa Bwana; Tena mizani ya hila si njema. Mithali 20:23

Yahweh detests differing weights, And dishonest scales are not pleasing.

Mwenendo wa mtu watoka kwa Bwana; Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake? Mithali 20:24

A man's steps are from Yahweh; How then can man understand his way?

Ni mtego, mtu aseme kwa haraka, Kitu hiki ni wakfu; Na baada ya kuweka nadhiri kuuliza-uliza habari. Mithali 20:25

It is a snare to a man to make a rash dedication, Then later to consider his vows.

Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki; Naye hulipitisha gurudumo la kupuria juu yao. Mithali 20:26

A wise king winnows out the wicked, And drives the threshing wheel over them.

Pumzi ya mwanadamu ni taa ya Bwana; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake. Mithali 20:27

The spirit of man is Yahweh's lamp, Searching all his innermost parts.

Fadhili na uaminifu humhifadhi mfalme, Na kiti chake cha enzi huthibitishwa kwa fadhili. Mithali 20:28

Love and faithfulness keep the king safe. His throne is sustained by love.

Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi. Mithali 20:29

The glory of young men is their strength. The splendor of old men is their gray hair.

Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikilia ndani ya mtima. Mithali 20:30

Wounding blows cleanse away evil, And beatings purge the innermost parts.