Mithali 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mithali 22 (Swahili) Proverbs 22 (English)

Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu. Mithali 22:1

A good name is more desirable than great riches, And loving favor is better than silver and gold.

Tajiri na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote wawili. Mithali 22:2

The rich and the poor have this in common: Yahweh is the maker of them all.

Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia. Mithali 22:3

A prudent man sees danger, and hides himself; But the simple pass on, and suffer for it.

Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. Mithali 22:4

The result of humility and the fear of Yahweh Is wealth, honor, and life.

Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo. Mithali 22:5

Thorns and snares are in the path of the wicked: Whoever guards his soul stays from them.

Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee. Mithali 22:6

Train up a child in the way he should go, And when he is old he will not depart from it.

Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye. Mithali 22:7

The rich rule over the poor. The borrower is servant to the lender.

Yeye apandaye uovu atavuna msiba, Na fimbo ya ghadhabu yake itakoma. Mithali 22:8

He who sows wickedness reaps trouble, And the rod of his fury will be destroyed.

Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana huwapa maskini chakula chake. Mithali 22:9

He who has a generous eye will be blessed; For he shares his food with the poor.

Mtupe nje mwenye dharau, na ugomvi utatoka; Naam, fitina na fedheha zitakoma. Mithali 22:10

Drive out the mocker, and strife will go out; Yes, quarrels and insults will stop.

Apendaye usafi wa moyo, na neema ya midomo; Mfalme atakuwa rafiki yake. Mithali 22:11

He who loves purity of heart and speaks gracefully Is the king's friend.

Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini. Mithali 22:12

The eyes of Yahweh watch over knowledge; But he frustrates the words of the unfaithful.

Mtu mvivu husema, Simba yuko nje; Nitauawa katika njia kuu. Mithali 22:13

The sluggard says, "There is a lion outside! I will be killed in the streets!"

Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na Bwana atatumbukia ndani yake. Mithali 22:14

The mouth of an adulteress is a deep pit: He who is under Yahweh's wrath will fall into it.

Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali. Mithali 22:15

Folly is bound up in the heart of a child: The rod of discipline drives it far from him.

Yeye awaoneaye maskini ili kuongeza mapato, Naye ampaye tajiri, hupata hasara. Mithali 22:16

Whoever oppresses the poor for his own increase and whoever gives to the rich, Both come to poverty.

Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; Mithali 22:17

Turn your ear, and listen to the words of the wise. Apply your heart to my teaching.

maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Mithali 22:18

For it is a pleasant thing if you keep them within you, If all of them are ready on your lips.

Ili matumaini yako uyaweke kwa Bwana, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Mithali 22:19

That your trust may be in Yahweh, I teach you today, even you.

Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; Mithali 22:20

Haven't I written to you thirty excellent things Of counsel and knowledge,

ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli? Mithali 22:21

To teach you truth, reliable words, To give sound answers to the ones who sent you?

Usimnyang'anye maskini, kwa kuwa ni maskini; Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; Mithali 22:22

Don't exploit the poor, because he is poor; And don't crush the needy in court;

Kwa sababu Bwana atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka. Mithali 22:23

For Yahweh will plead their case, And plunder the life of those who plunder them.

Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Mithali 22:24

Don't befriend a hot-tempered man, And don't associate with one who harbors anger:

Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego. Mithali 22:25

Lest you learn his ways, And ensnare your soul.

Usiwe mmoja wao wawekao rehani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Mithali 22:26

Don't you be one of those who strike hands, Of those who are collateral for debts.

Kama huna kitu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chako chini yako? Mithali 22:27

If you don't have means to pay, Why should he take away your bed from under you?

Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako. Mithali 22:28

Don't move the ancient boundary stone, Which your fathers have set up.

Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme; Hatasimama mbele ya watu wasio na cheo. Mithali 22:29

Do you see a man skilled in his work? He will serve kings; He won't serve obscure men.