Marko 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 8 (Swahili) Mark 8 (English)

Katika siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha kula, akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Marko 8:1

In those days, when there was a very great multitude, and they had nothing to eat, Jesus called his disciples to himself, and said to them,

Nawahurumia mkutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; Marko 8:2

"I have compassion on the multitude, because they have stayed with me now three days, and have nothing to eat.

nami nikiwaaga waende zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka mbali. Marko 8:3

If I send them away fasting to their home, they will faint on the way, for some of them have come a long way."

Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate hapa nyikani? Marko 8:4

His disciples answered him, "From where could one satisfy these people with bread here in a deserted place?"

Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, Marko 8:5

He asked them, "How many loaves do you have?" They said, "Seven."

Akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano. Marko 8:6

He commanded the multitude to sit down on the ground, and he took the seven loaves. Having given thanks, he broke them, and gave them to his disciples to serve, and they served the multitude.

Walikuwa na visamaki vichache; akavibarikia, akasema wawaandikie na hivyo pia. Marko 8:7

They had a few small fish. Having blessed them, he said to serve these also.

Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. Marko 8:8

They ate, and were filled. They took up seven baskets of broken pieces that were left over.

Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga. Marko 8:9

Those who had eaten were about four thousand. Then he sent them away.

Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha. Marko 8:10

Immediately he entered into the boat with his disciples, and came into the region of Dalmanutha.

Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu. Marko 8:11

The Pharisees came out and began to question him, seeking from him a sign from heaven, and testing him.

Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. Marko 8:12

He sighed deeply in his spirit, and said, "Why does this generation{The word translated "generation" here (genea) could also be translated "people," "race," or "family."} seek a sign? Most assuredly I tell you, no sign will be given to this generation."

Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng'ambo. Marko 8:13

He left them, and again entering into the boat, departed to the other side.

Wakasahau kuchukua mikate, wala chomboni hawana ila mkate mmoja tu. Marko 8:14

They forgot to take bread; and they didn't have more than one loaf in the boat with them.

Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode. Marko 8:15

He charged them, saying, "Take heed: beware of the yeast of the Pharisees and the yeast of Herod."

Wakabishana wao kwa wao, kwa kuwa hawana mikate. Marko 8:16

They reasoned with one another, saying, "It's because we have no bread."

Naye Yesu akatambua, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Je! Mioyo yenu ni mizito? Marko 8:17

Jesus, perceiving it, said to them, "Why do you reason that it's because you have no bread? Don't you perceive yet, neither understand? Is your heart still hardened?

Mna macho, hamwoni; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki? Marko 8:18

Having eyes, don't you see? Having ears, don't you hear? Don't you remember?

Nilipoivunja ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Kumi na viwili. Marko 8:19

When I broke the five loaves among the five thousand, how many baskets full of broken pieces did you take up?" They told him, "Twelve."

Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba. Marko 8:20

"When the seven loaves fed the four thousand, how many baskets full of broken pieces did you take up?" They told him, "Seven."

Akawaambia, Hamjafahamu bado? Marko 8:21

He asked them, "Don't you understand, yet?"

Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. Marko 8:22

He came to Bethsaida. They brought a blind man to him, and begged him to touch him.

Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? Marko 8:23

He took hold of the blind man by the hand, and brought him out of the village. When he had spit on his eyes, and laid his hands on him, he asked him if he saw anything.

Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda. Marko 8:24

He looked up, and said, "I see men; for I see them like trees walking."

Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. Marko 8:25

Then again he laid his hands on his eyes. He looked intently, and was restored, and saw everyone clearly.

Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie. Marko 8:26

He sent him away to his house, saying, "Don't enter into the village, nor tell anyone in the village."

Akatoka Yesu na wanafunzi wake, wakaenda kwenye vijiji vya Kaisaria-Filipi; na njiani akawauliza wanafunzi wake, akasema, Watu huninena mimi kuwa ni nani? Marko 8:27

Jesus went out, with his disciples, into the villages of Caesarea Philippi. On the way he asked his disciples, "Who do men say that I am?"

Wakamjibu, Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; wengine, Mmojawapo wa manabii. Marko 8:28

They told him, "John the Baptizer, and others say Elijah, but others: one of the prophets."

Naye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo. Marko 8:29

He said to them, "But who do you say that I am?" Peter answered, "You are the Christ."

Akawaonya wasimwambie mtu habari zake. Marko 8:30

He charged them that they should tell no one about him.

Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka. Marko 8:31

He began to teach them that the Son of Man must suffer many things, and be rejected by the elders, the chief priests, and the scribes, and be killed, and after three days rise again.

Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea. Marko 8:32

He spoke to them openly. Peter took him, and began to rebuke him.

Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. Marko 8:33

But he, turning around, and seeing his disciples, rebuked Peter, and said, "Get behind me, Satan! For you have in mind not the things of God, but the things of men."

Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Marko 8:34

He called the multitude to himself with his disciples, and said to them, "Whoever wants to come after me, let him deny himself, and take up his cross, and follow me.

Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. Marko 8:35

For whoever wants to save his life will lose it; and whoever will lose his life for my sake and the Gospel's will save it.

Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Marko 8:36

For what does it profit a man, to gain the whole world, and forfeit his life?

Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Marko 8:37

For what will a man give in exchange for his life?

Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu. Marko 8:38

For whoever will be ashamed of me and of my words in this adulterous and sinful generation, the Son of Man also will be ashamed of him, when he comes in the glory of his Father with the holy angels."