Marko 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 2 (Swahili) Mark 2 (English)

Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani. Marko 2:1

When he entered again into Capernaum after some days, it was heard that he was in the house.

Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. Marko 2:2

Immediately many were gathered together, so that there was no more room, not even around the door; and he spoke the word to them.

Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Marko 2:3

Four people came, carrying a paralytic to him.

Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Marko 2:4

When they could not come near to him for the crowd, they removed the roof where he was. When they had broken it up, they let down the mat that the paralytic was lying on.

Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako. Marko 2:5

Jesus, seeing their faith, said to the paralytic, "Son, your sins are forgiven you."

Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Marko 2:6

But there were some of the scribes sitting there, and reasoning in their hearts,

Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? Marko 2:7

"Why does this man speak blasphemies like that? Who can forgive sins but God alone?"

Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Marko 2:8

Immediately Jesus, perceiving in his spirit that they so reasoned within themselves, said to them, "Why do you reason these things in your hearts?

Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Marko 2:9

Which is easier, to tell the paralytic, 'Your sins are forgiven;' or to say, 'Arise, and take up your bed, and walk?'

Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), Marko 2:10

But that you may know that the Son of Man has authority on earth to forgive sins"--he said to the paralytic--

Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako. Marko 2:11

"I tell you, arise, take up your mat, and go to your house."

Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe. Marko 2:12

He arose, and immediately took up the mat, and went out in front of them all; so that they were all amazed, and glorified God, saying, "We never saw anything like this!"

Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha. Marko 2:13

He went out again by the seaside. All the multitude came to him, and he taught them.

Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata. Marko 2:14

As he passed by, he saw Levi, the son of Alphaeus, sitting at the tax office, and he said to him, "Follow me." And he arose and followed him.

Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata. Marko 2:15

It happened, that he was reclining at the table in his house, and many tax collectors and sinners sat down with Jesus and his disciples, for there were many, and they followed him.

Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Marko 2:16

The scribes and the Pharisees, when they saw that he was eating with the sinners and tax collectors, said to his disciples, "Why is it that he eats and drinks with tax collectors and sinners?"

Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. Marko 2:17

When Jesus heard it, he said to them, "Those who are healthy have no need for a physician, but those who are sick. I came not to call the righteous, but sinners to repentance."

Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Marko 2:18

John's disciples and the Pharisees were fasting, and they came and asked him, "Why do John's disciples and the disciples of the Pharisees fast, but your disciples don't fast?"

Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga. Marko 2:19

Jesus said to them, "Can the groomsmen fast while the bridegroom is with them? As long as they have the bridegroom with them, they can't fast.

Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile. Marko 2:20

But the days will come when the bridegroom will be taken away from them, and then will they fast in that day.

Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi. Marko 2:21

No one sews a piece of unshrunk cloth on an old garment, or else the patch shrinks and the new tears away from the old, and a worse hole is made.

Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya. Marko 2:22

No one puts new wine into old wineskins, or else the new wine will burst the skins, and the wine pours out, and the skins will be destroyed; but they put new wine into fresh wineskins."

Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke. Marko 2:23

It happened that he was going on the Sabbath day through the grain fields, and his disciples began, as they went, to pluck the ears of grain.

Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato? Marko 2:24

The Pharisees said to him, "Behold, why do they do that which is not lawful on the Sabbath day?"

Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa ana haja, na kuona njaa, yeye na wenziwe? Marko 2:25

He said to them, "Did you never read what David did, when he had need, and was hungry--he, and they who were with him?

Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiathari, akaila mikate ile ya Wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe? Marko 2:26

How he entered into the house of God when Abiathar was high priest, and ate the show bread, which it is not lawful to eat except for the priests, and gave also to those who were with him?"

Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Marko 2:27

He said to them, "The Sabbath was made for man, not man for the Sabbath.

Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia. Marko 2:28

Therefore the Son of Man is lord even of the Sabbath."