Marko 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 6 (Swahili) Mark 6 (English)

Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. Marko 6:1

He went out from there. He came into his own country, and his disciples followed him.

Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Marko 6:2

When the Sabbath had come, he began to teach in the synagogue, and many hearing him were astonished, saying, "Where did this man get these things?" and, "What is the wisdom that is given to this man, that such mighty works come about by his hands?

Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Marko 6:3

Isn't this the carpenter, the son of Mary, and brother of James, Joses, Judas, and Simon? Aren't his sisters here with us?" They were offended at him.

Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. Marko 6:4

Jesus said to them, "A prophet is not without honor, except in his own country, and among his own relatives, and in his own house."

Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Marko 6:5

He could do no mighty work there, except that he laid his hands on a few sick people, and healed them.

Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha. Marko 6:6

He marveled because of their unbelief. He went around the villages teaching.

Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; Marko 6:7

He called to himself the twelve, and began to send them out two by two; and he gave them authority over the unclean spirits.

akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni; Marko 6:8

He charged them that they should take nothing for their journey, except a staff only: no bread, no wallet, no money in their purse,

lakini wajifungie viatu; akasema, Msivae kanzu mbili. Marko 6:9

but to wear sandals, and not put on two tunics.

Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale. Marko 6:10

He said to them, "Wherever you enter into a house, stay there until you depart from there.

Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao. Marko 6:11

Whoever will not receive you nor hear you, as you depart from there, shake off the dust that is under your feet for a testimony against them. Assuredly, I tell you, it will be more tolerable for Sodom and Gomorrah in the day of judgment than for that city!"

Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. Marko 6:12

They went out and preached that people should repent.

Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza. Marko 6:13

They cast out many demons, and anointed many with oil who were sick, and healed them.

Naye Mfalme Herode akasikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa kutangaa, akasema, Yohana Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Marko 6:14

King Herod heard this, for his name had become known, and he said, "John the Baptizer has risen from the dead, and therefore these powers are at work in him."

Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama mmoja wa manabii. Marko 6:15

But others said, "It is Elijah." Others said, "It is the Prophet, or like one of the prophets."

Lakini Herode aliposikia, alisema, Yohana, niliyemkata kichwa, amefufuka. Marko 6:16

But Herod, when he heard this, said, "This is John, whom I beheaded. He has risen from the dead."

Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake, kwa kuwa amemwoa; Marko 6:17

For Herod himself had sent out and arrested John, and bound him in prison for the sake of Herodias, his brother Philip's wife, for he had married her.

kwa sababu Yohana alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. Marko 6:18

For John said to Herod, "It is not lawful for you to have your brother's wife."

Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. Marko 6:19

Herodias set herself against him, and desired to kill him, but she couldn't,

Maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha. Marko 6:20

for Herod feared John, knowing that he was a righteous and holy man, and kept him safe. When he heard him, he did many things, and he heard him gladly.

Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; Marko 6:21

Then a convenient day came, that Herod on his birthday made a supper for his nobles, the high officers, and the chief men of Galilee.

ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa. Marko 6:22

When the daughter of Herodias herself came in and danced, she pleased Herod and those sitting with him. The king said to the young lady, "Ask me whatever you want, and I will give it to you."

Akamwapia, Lo lote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu. Marko 6:23

He swore to her, "Whatever you shall ask of me, I will give you, up to half of my kingdom."

Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohana Mbatizaji. Marko 6:24

She went out, and said to her mother, "What shall I ask?" She said, "The head of John the Baptizer."

Mara akaingia kwa haraka mbele ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji. Marko 6:25

She came in immediately with haste to the king, and asked, "I want you to give me right now the head of John the Baptizer on a platter."

Mfalme akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. Marko 6:26

The king was exceedingly sorry, but for the sake of his oaths, and of his dinner guests, he didn't wish to refuse her.

Mara mfalme akatuma askari, akaamuru kuleta kichwa chake. Basi akaenda, akamkata kichwa mle gerezani, Marko 6:27

Immediately the king sent out a soldier of his guard, and commanded to bring John's head, and he went and beheaded him in the prison,

akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye. Marko 6:28

and brought his head on a platter, and gave it to the young lady; and the young lady gave it to her mother.

Wanafunzi wake waliposikia habari, walikwenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini. Marko 6:29

When his disciples heard this, they came and took up his corpse, and laid it in a tomb.

Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha. Marko 6:30

The apostles gathered themselves together to Jesus, and they told him all things, whatever they had done, and whatever they had taught.

Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula. Marko 6:31

He said to them, "You come apart into a deserted place, and rest awhile." For there were many coming and going, and they had no leisure so much as to eat.

Wakaenda zao faragha mashuani, mahali pasipokuwa na watu. Marko 6:32

They went away in the boat to a desert place by themselves.

Watu wakawaona wakienda zao, na wengi wakatambua, wakaenda huko mbio kwa miguu, toka miji yote, wakatangulia kufika. Marko 6:33

They{TR reads "The multitudes" instead of "They"} saw them going, and many recognized him and ran there on foot from all the cities. They arrived before them and came together to him.

Naye aliposhuka mashuani, akaona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi. Marko 6:34

Jesus came out, saw a great multitude, and he had compassion on them, because they were like sheep without a shepherd, and he began to teach them many things.

Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; Marko 6:35

When it was late in the day, his disciples came to him, and said, "This place is deserted, and it is late in the day.

uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. Marko 6:36

Send them away, that they may go into the surrounding country and villages, and buy themselves bread, for they have nothing to eat."

Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula? Marko 6:37

But he answered them, "You give them something to eat." They asked him, "Shall we go and buy two hundred denarii{200 denarii was about 7 or 8 months wages for an agricultural laborer.} worth of bread, and give them something to eat?"

Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili. Marko 6:38

He said to them, "How many loaves do you have? Go see." When they knew, they said, "Five, and two fish."

Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. Marko 6:39

He commanded them that everyone should sit down in groups on the green grass.

Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini. Marko 6:40

They sat down in ranks, by hundreds and by fifties.

Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote. Marko 6:41

He took the five loaves and the two fish, and looking up to heaven, he blessed and broke the loaves, and he gave to his disciples to set before them, and he divided the two fish among them all.

Wakala wote wakashiba. Marko 6:42

They all ate, and were filled.

Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia. Marko 6:43

They took up twelve baskets full of broken pieces and also of the fish.

Na walioila ile mikate wapata elfu tano wanaume. Marko 6:44

Those who ate the loaves were{TR adds "about"} five thousand men.

Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano. Marko 6:45

Immediately he made his disciples get into the boat, and to go ahead to the other side, to Bethsaida, while he himself sent the multitude away.

Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba. Marko 6:46

After he had taken leave of them, he went up the mountain to pray.

Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yu peke yake katika nchi kavu. Marko 6:47

When evening had come, the boat was in the midst of the sea, and he was alone on the land.

Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita. Marko 6:48

Seeing them distressed in rowing, for the wind was contrary to them, about the fourth watch of the night he came to them, walking on the sea, and he would have passed by them,

Nao walipomwona anatembea juu ya bahari, walidhani ya kuwa ni kivuli, wakapiga yowe, Marko 6:49

but they, when they saw him walking on the sea, supposed that it was a ghost, and cried out;

kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope. Marko 6:50

for they all saw him, and were troubled. But he immediately spoke with them, and said to them, "Cheer up! It is I!{Literally, "I AM!"} Don't be afraid."

Akapanda mle chomboni walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao; Marko 6:51

He got into the boat with them; and the wind ceased, and they were very amazed among themselves, and marveled;

kwa maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito. Marko 6:52

for they hadn't understood about the loaves, but their hearts were hardened.

Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga. Marko 6:53

When they had crossed over, they came to land at Gennesaret, and moored to the shore.

Nao wakiisha kutoka mashuani, mara watu walimtambua, Marko 6:54

When they had come out of the boat, immediately the people recognized him,

wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani walio hawawezi, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo. Marko 6:55

and ran around that whole region, and began to bring those who were sick, on their mats, to where they heard he was.

Na kila alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse ngaa pindo la vazi lake; nao wote waliomgusa wakapona. Marko 6:56

Wherever he entered, into villages, or into cities, or into the country, they laid the sick in the marketplaces, and begged him that they might touch just the fringe of his garment; and as many as touched him were made well.