Marko 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 13 (Swahili) Mark 13 (English)

Hata alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, Mwalimu, tazama, yalivyo mawe na majengo haya! Marko 13:1

As he went out of the temple, one of his disciples said to him, "Teacher, see what kind of stones and what kind of buildings!"

Yesu akajibu, akamwambia, Wayaona majengo haya makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa. Marko 13:2

Jesus said to him, "Do you see these great buildings? There will not be left here one stone on another, which will not be thrown down."

Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, kuelekea hekalu Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea walimwuliza kwa faragha, Marko 13:3

As he sat on the Mount of Olives opposite the temple, Peter, James, John, and Andrew asked him privately,

Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya wakati, hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia? Marko 13:4

"Tell us, when will these things be? What is the sign that these things are all about to be fulfilled?"

Yesu akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye. Marko 13:5

Jesus, answering, began to tell them, "Be careful that no one leads you astray.

Wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye, nao watadanganya wengi. Marko 13:6

For many will come in my name, saying, 'I am he!{Literally, "I AM!"}' and will lead many astray.

Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. Marko 13:7

"When you hear of wars and rumors of wars, don't be troubled. For those must happen, but the end is not yet.

Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu. Marko 13:8

For nation will rise against nation, and kingdom against kingdom. There will be earthquakes in various places. There will be famines and troubles. These things are the beginning of birth pains.

Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao. Marko 13:9

But watch yourselves, for they will deliver you up to councils. You will be beaten in synagogues. You will stand before rulers and kings for my sake, for a testimony to them.

Na sharti Injili ihubiriwe kwanza katika mataifa yote. Marko 13:10

The Gospel must first be preached to all the nations.

Na watakapowachukua ninyi, na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni; kwa maana si ninyi msemao, bali ni Roho Mtakatifu. Marko 13:11

When they lead you away and deliver you up, don't be anxious beforehand, or premeditate what you will say, but say whatever will be given you in that hour. For it is not you who speak, but the Holy Spirit.

Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, na baba atamsaliti mtoto, na watoto watashambulia wazazi wao, na kuwafisha. Marko 13:12

"Brother will deliver up brother to death, and the father his child. Children will rise up against parents, and cause them to be put to death.

Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Marko 13:13

You will be hated by all men for my name's sake, but he who endures to the end, the same will be saved.

Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; Marko 13:14

But when you see the abomination of desolation, spoken of by Daniel the prophet, standing where it ought not (let the reader understand), then let those who are in Judea flee to the mountains,

na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; Marko 13:15

and let him who is on the housetop not go down, nor enter in, to take anything out of his house.

naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Marko 13:16

Let him who is in the field not return back to take his cloak.

Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Marko 13:17

But woe to those who are with child and to those who nurse babies in those days!

Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Marko 13:18

Pray that your flight won't be in the winter.

Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Marko 13:19

For in those days there will be oppression, such as there has not been the like from the beginning of the creation which God created until now, and never will be.

Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. Marko 13:20

Unless the Lord had shortened the days, no flesh would have been saved; but for the sake of the chosen ones, whom he picked out, he shortened the days.

Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; Marko 13:21

Then if anyone tells you, 'Look, here is the Christ!' or, 'Look, there!' don't believe it.

kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. Marko 13:22

For there will arise false christs and false prophets, and will show signs and wonders, that they may lead astray, if possible, even the chosen ones.

Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele. Marko 13:23

But you watch. "Behold, I have told you all things beforehand.

Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. Marko 13:24

But in those days, after that oppression, the sun will be darkened, the moon will not give its light,

na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Marko 13:25

the stars will be falling from the sky, and the powers that are in the heavens will be shaken.

Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Marko 13:26

Then they will see the Son of Man coming in clouds with great power and glory.

Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu. Marko 13:27

Then he will send out his angels, and will gather together his chosen ones from the four winds, from the ends of the earth to the ends of the sky.

Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liishapo kuwa laini, na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno ni karibu; Marko 13:28

"Now from the fig tree, learn this parable. When the branch has now become tender, and puts forth its leaves, you know that the summer is near;

nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Marko 13:29

even so you also, when you see these things coming to pass, know that it is near, at the doors.

Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie. Marko 13:30

Most assuredly I say to you, this generation{The word translated "generation" (genea) could also be translated "race," "family," or "people."} will not pass away until all these things happen.

Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Marko 13:31

Heaven and earth will pass away, but my words will not pass away.

Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba. Marko 13:32

But of that day or that hour no one knows, not even the angels in heaven, nor the Son, but only the Father.

Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo. Marko 13:33

Watch, keep alert, and pray; for you don't know when the time is.

Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe. Marko 13:34

"It is like a man, traveling to another country, having left his house, and given authority to his servants, and to each one his work, and also commanded the doorkeeper to keep watch.

Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi; Marko 13:35

Watch therefore, for you don't know when the lord of the house is coming, whether at evening, or at midnight, or when the rooster crows, or in the morning;

asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. Marko 13:36

lest coming suddenly he might find you sleeping.

Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni. Marko 13:37

What I tell you, I tell all: Watch."