Marko 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 5 (Swahili) Mark 5 (English)

Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Marko 5:1

They came to the other side of the sea, into the country of the Gadarenes.

Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; Marko 5:2

When he had come out of the boat, immediately there met him out of the tombs a man with an unclean spirit,

makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; Marko 5:3

who had his dwelling in the tombs. Nobody could bind him any more, not even with chains,

kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Marko 5:4

because he had been often bound with fetters and chains, and the chains had been torn apart by him, and the fetters broken in pieces. Nobody had the strength to tame him.

Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Marko 5:5

Always, night and day, in the tombs and in the mountains, he was crying out, and cutting himself with stones.

Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; Marko 5:6

When he saw Jesus from afar, he ran and bowed down to him,

akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Marko 5:7

and crying out with a loud voice, he said, "What have I to do with you, Jesus, you Son of the Most High God? I adjure you by God, don't torment me."

Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Marko 5:8

For he said to him, "Come out of the man, you unclean spirit!"

Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. Marko 5:9

He asked him, "What is your name?" He said to him, "My name is Legion, for we are many."

Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Marko 5:10

He begged him much that he would not send them away out of the country.

Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. Marko 5:11

Now there was on the mountainside a great herd of pigs feeding.

Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Marko 5:12

All the demons begged him, saying, "Send us into the pigs, that we may enter into them."

Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. Marko 5:13

At once Jesus gave them permission. The unclean spirits came out and entered into the pigs. The herd of about two thousand rushed down the steep bank into the sea, and they were drowned in the sea.

Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. Marko 5:14

Those who fed them fled, and told it in the city and in the country. The people came to see what it was that had happened.

Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Marko 5:15

They came to Jesus, and saw him who had been possessed by demons sitting, clothed, and in his right mind, even him who had the legion; and they were afraid.

Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. Marko 5:16

Those who saw it declared to them how it happened to him who was possessed by demons, and about the pigs.

Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao. Marko 5:17

They began to beg him to depart from their region.

Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; Marko 5:18

As he was entering into the boat, he who had been possessed by demons begged him that he might be with him.

lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Marko 5:19

He didn't allow him, but said to him, "Go to your house, to your friends, and tell them what great things the Lord has done for you, and how he had mercy on you."

Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu. Marko 5:20

He went his way, and began to proclaim in Decapolis how Jesus had done great things for him, and everyone marveled.

Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari. Marko 5:21

When Jesus had crossed back over in the boat to the other side, a great multitude was gathered to him; and he was by the sea.

Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake, Marko 5:22

Behold, one of the rulers of the synagogue, Jairus by name, came; and seeing him, he fell at his feet,

akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi. Marko 5:23

and begged him much, saying, "My little daughter is at the point of death. Please come and lay your hands on her, that she may be made healthy, and live."

Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa. Marko 5:24

He went with him, and a great multitude followed him, and they pressed upon him on all sides.

Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, Marko 5:25

A certain woman, who had an issue of blood for twelve years,

na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya Marko 5:26

and had suffered many things by many physicians, and had spent all that she had, and was no better, but rather grew worse,

aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; Marko 5:27

having heard the things concerning Jesus, came up behind him in the crowd, and touched his clothes.

maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Marko 5:28

For she said, "If I just touch his clothes, I will be made well."

Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Marko 5:29

Immediately the flow of her blood was dried up, and she felt in her body that she was healed of her affliction.

Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Marko 5:30

Immediately Jesus, perceiving in himself that the power had gone out from him, turned around in the crowd, and asked, "Who touched my clothes?"

Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa? Marko 5:31

His disciples said to him, "You see the multitude pressing against you, and you say, 'Who touched me?'"

Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo. Marko 5:32

He looked around to see her who had done this thing.

Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Marko 5:33

But the woman, fearing and trembling, knowing what had been done to her, came and fell down before him, and told him all the truth.

Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena. Marko 5:34

He said to her, "Daughter, your faith has made you well. Go in peace, and be cured of your disease."

Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? Marko 5:35

While he was still speaking, they came from the synagogue ruler's house saying, "Your daughter is dead. Why bother the Teacher any more?"

Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. Marko 5:36

But Jesus, when he heard the message spoken, immediately said to the ruler of the synagogue, "Don't be afraid, only believe."

Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo. Marko 5:37

He allowed no one to follow him, except Peter, James, and John the brother of James.

Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Marko 5:38

He came to the synagogue ruler's house, and he saw an uproar, weeping, and great wailing.

Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. Marko 5:39

When he had entered in, he said to them, "Why do you make an uproar and weep? The child is not dead, but is asleep."

Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana. Marko 5:40

They ridiculed him. But he, having put them all out, took the father of the child and her mother and those who were with him, and went in where the child was lying.

Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Marko 5:41

Taking the child by the hand, he said to her, "Talitha cumi;" which means, being interpreted, "Girl, I tell you, get up."

Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. Marko 5:42

Immediately the girl rose up, and walked, for she was twelve years old. They were amazed with great amazement.

Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula. Marko 5:43

He strictly ordered them that no one should know this, and commanded that something should be given to her to eat.