Marko 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 15 (Swahili) Mark 15 (English)

Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato. Marko 15:1

Immediately in the morning the chief priests, with the elders and scribes, and the whole council, held a consultation, and bound Jesus, and carried him away, and delivered him up to Pilate.

Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Wewe wasema. Marko 15:2

Pilate asked him, "Are you the King of the Jews?" He answered, "So you say."

Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi. Marko 15:3

The chief priests accused him of many things.

Pilato akamwuliza tena akisema, Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki! Marko 15:4

Pilate again asked him, "Have you no answer? See how many things they testify against you!"

Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu. Marko 15:5

But Jesus made no further answer, so that Pilate marveled.

Basi wakati wa sikukuu huwafungulia mfungwa mmoja, wamwombaye. Marko 15:6

Now at the feast he used to release to them one prisoner, whom they asked of him.

Palikuwa na mtu aitwaye Baraba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina, na kufanya uuaji katika fitina ile. Marko 15:7

There was one called Barabbas, bound with those who had made insurrection, men who in the insurrection had committed murder.

Makutano wakaja, wakaanza kuomba awafanyie kama vile alivyozoea. Marko 15:8

The multitude, crying aloud, began to ask him to do as he always did for them.

Pilato akawajibu, akisema, Je! Mnataka niwafungulie mfalme wa Wayahudi? Marko 15:9

Pilate answered them, saying, "Do you want me to release to you the King of the Jews?"

Kwa maana alitambua ya kuwa wakuu wa makuhani wamemtoa kwa husuda. Marko 15:10

For he perceived that for envy the chief priests had delivered him up.

Lakini wakuu wa makuhani wakawataharakisha makutano, kwamba afadhali awafungulie Baraba. Marko 15:11

But the chief priests stirred up the multitude, that he should release Barabbas to them instead.

Pilato akajibu tena akawaambia, Basi nimtendeje huyu mnayemnena kuwa ni mfalme wa Wayahudi? Marko 15:12

Pilate again asked them, "What then should I do to him whom you call the King of the Jews?"

Wakapiga kelele tena, Msulibishe. Marko 15:13

They cried out again, "Crucify him!"

Pilato akawaambia, Kwani, ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulibishe. Marko 15:14

Pilate said to them, "Why, what evil has he done?" But they cried out exceedingly, "Crucify him!"

Pilato akipenda kuwaridhisha makutano, akawafungulia Baraba; akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, ili asulibiwe. Marko 15:15

Pilate, wishing to please the multitude, released Barabbas to them, and handed over Jesus, when he had flogged him, to be crucified.

Nao askari wakamchukua ndani ya behewa, ndiyo Praitorio (yaani, nyumba ya uliwali), wakakusanya pamoja kikosi kizima. Marko 15:16

The soldiers led him away within the court, which is the Praetorium; and they called together the whole cohort.

Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani; Marko 15:17

They clothed him with purple, and weaving a crown of thorns, they put it on him.

wakaanza kumsalimu, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! Marko 15:18

They began to salute him, "Hail, King of the Jews!"

Wakampiga mwanzi wa kichwa, wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudia. Marko 15:19

They struck his head with a reed, and spat on him, and bowing their knees, did homage to him.

Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi la rangi ya zambarau, wakamvika mavazi yake mwenyewe; wakamchukua nje ili wamsulibishe. Marko 15:20

When they had mocked him, they took the purple off of him, and put his own garments on him. They led him out to crucify him.

Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simoni Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake. Marko 15:21

They compelled one passing by, coming from the country, Simon of Cyrene, the father of Alexander and Rufus, to go with them, that he might bear his cross.

Wakamleta mpaka mahali paitwapo Golgotha, yaani, Fuvu la kichwa. Marko 15:22

They brought him to the place called Golgotha, which is, being interpreted, "The place of a skull."

Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane, asiipokee. Marko 15:23

They offered him wine mixed with myrrh to drink, but he didn't take it.

Wakamsulibisha, wakagawa mavazi yake, wakayapigia kura kila mtu atwae nini. Marko 15:24

Crucifying him, they parted his garments among them, casting lots on them, what each should take.

Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha. Marko 15:25

It was the third hour,{9:00 A. M.} and they crucified him.

Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI. Marko 15:26

The superscription of his accusation was written over him, "THE KING OF THE JEWS."

Na pamoja naye walisulibisha wanyang'anyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. [ Marko 15:27

With him they crucified two robbers; one on his right hand, and one on his left.

Basi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na waasi.] Marko 15:28

The Scripture was fulfilled, which says, "He was numbered with transgressors."

Nao waliokuwa wakipita njiani wakamtukana, wakitikisa-tikisa vichwa, wakisema, Ahaa! Wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga katika siku tatu, Marko 15:29

Those who passed by blasphemed him, wagging their heads, and saying, "Ha! You who destroy the temple, and build it in three days,

jiponye nafsi yako, ushuke msalabani. Marko 15:30

save yourself, and come down from the cross!"

Kadhalika na wakuu wa makuhani wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliponya wengine; hawezi kujiponya mwenyewe. Marko 15:31

Likewise, also the chief priests mocking among themselves with the scribes said, "He saved others. He can't save himself.

Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Hata wale waliosulibiwa pamoja naye wakamfyolea. Marko 15:32

Let the Christ, the King of Israel, now come down from the cross, that we may see and believe him.{TR omits "him"}" Those who were crucified with him insulted him.

Na ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yote, hata saa tisa. Marko 15:33

When the sixth hour{or, noon} had come, there was darkness over the whole land until the ninth hour.{3:00 PM}

Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Marko 15:34

At the ninth hour Jesus cried with a loud voice, saying, "Eloi, Eloi, lama sabachthani?" which is, being interpreted, "My God, my God, why have you forsaken me?"

Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya. Marko 15:35

Some of those who stood by, when they heard it, said, "Behold, he is calling Elijah."

Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha. Marko 15:36

One ran, and filling a sponge full of vinegar, put it on a reed, and gave it to him to drink, saying, "Let him be. Let's see whether Elijah comes to take him down."

Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. Marko 15:37

Jesus cried out with a loud voice, and gave up the spirit.

Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini. Marko 15:38

The veil of the temple was torn in two from the top to the bottom.

Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu. Marko 15:39

When the centurion, who stood by opposite him, saw that he cried out like this and breathed his last, he said, "Truly this man was the Son of God!"

Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome; Marko 15:40

There were also women watching from afar, among whom were both Mary Magdalene, and Mary the mother of James the less and of Joses, and Salome;

hao ndio waliofuatana naye huko Galilaya, na kumtumikia; na wengine wengi waliopanda pamoja naye mpaka Yerusalemu. Marko 15:41

who, when he was in Galilee, followed him, and served him; and many other women who came up with him to Jerusalem.

Hata ikiisha kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato, Marko 15:42

When evening had now come, because it was the Preparation Day, that is, the day before the Sabbath,

akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza ya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu. Marko 15:43

Joseph of Arimathaea, a prominent council member who also himself was looking for the Kingdom of God, came. He boldly went in to Pilate, and asked for Jesus' body.

Lakini Pilato akastaajabu, kwamba amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. Marko 15:44

Pilate marveled if he were already dead; and summoning the centurion, he asked him whether he had been dead long.

Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti. Marko 15:45

When he found out from the centurion, he granted the body to Joseph.

Naye akanunua sanda ya kitani, akamtelemsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi. Marko 15:46

He bought a linen cloth, and taking him down, wound him in the linen cloth, and laid him in a tomb which had been cut out of a rock. He rolled a stone against the door of the tomb.

Nao Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose wakapatazama mahali alipowekwa. Marko 15:47

Mary Magdalene and Mary, the mother of Joses, saw where he was laid.