Marko 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 7 (Swahili) Mark 7 (English)

Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake, Marko 7:1

Then the Pharisees, and some of the scribes gathered together to him, having come from Jerusalem.

wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa. Marko 7:2

Now when they saw some of his disciples eating bread with defiled, that is, unwashed, hands, they found fault.

Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; Marko 7:3

(For the Pharisees, and all the Jews, don't eat unless they wash their hands and forearms, holding to the tradition of the elders.

tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba. Marko 7:4

They don't eat when they come from the marketplace, unless they bathe themselves, and there are many other things, which they have received to hold to: washings of cups, pitchers, bronze vessels, and couches.)

Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? Marko 7:5

The Pharisees and the scribes asked him, "Why don't your disciples walk according to the tradition of the elders, but eat their bread with unwashed hands?"

Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; Marko 7:6

He answered them, "Well did Isaiah prophesy of you hypocrites, as it is written, 'This people honors me with their lips, But their heart is far from me.

Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Marko 7:7

But in vain do they worship me, Teaching as doctrines the commandments of men.'

Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu. Marko 7:8

"For you set aside the commandment of God, and hold tightly to the tradition of men--the washing of pitchers and cups, and you do many other such things."

Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. Marko 7:9

He said to them, "Full well do you reject the commandment of God, that you may keep your tradition.

Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. Marko 7:10

For Moses said, 'Honor your father and your mother;' and, 'He who speaks evil of father or mother, let him be put to death.'

Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; Marko 7:11

But you say, 'If a man tells his father or his mother, "Whatever profit you might have received from me is Corban{Corban is a Hebrew word for an offering devoted to God.}, that is to say, given to God;"'

wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; Marko 7:12

then you no longer allow him to do anything for his father or his mother,

huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo. Marko 7:13

making void the word of God by your tradition, which you have handed down. You do many things like this."

Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. Marko 7:14

He called all the multitude to himself, and said to them, "Hear me, all of you, and understand.

Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. Marko 7:15

There is nothing from outside of the man, that going into him can defile him; but the things which proceed out of the man are those that defile the man.

Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.] Marko 7:16

If anyone has ears to hear, let him hear!"

Hata alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule mfano. Marko 7:17

When he had entered into a house away from the multitude, his disciples asked him about the parable.

Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; Marko 7:18

He said to them, "Are you thus without understanding also? Don't you perceive that whatever goes into the man from outside can't defile him,

kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. Marko 7:19

because it doesn't go into his heart, but into his stomach, then into the latrine, thus making all foods clean?"

Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Marko 7:20

He said, "That which proceeds out of the man, that defiles the man.

Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, Marko 7:21

For from within, out of the hearts of men, proceed evil thoughts, adulteries, sexual sins, murders, thefts,

wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Marko 7:22

covetings, wickedness, deceit, lustful desires, an evil eye, blasphemy, pride, and foolishness.

Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. Marko 7:23

All these evil things come from within, and defile the man."

Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika. Marko 7:24

From there he arose, and went away into the borders of Tyre and Sidon. He entered into a house, and didn't want anyone to know it, but he couldn't escape notice.

Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake. Marko 7:25

For a woman, whose little daughter had an unclean spirit, having heard of him, came and fell down at his feet.

Na yule mwanamke ni Myunani, kabila yake ni Msirofoinike. Akamwomba amtoe pepo katika binti yake. Marko 7:26

Now the woman was a Greek, a Syrophoenician by race. She begged him that he would cast the demon out of her daughter.

Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa. Marko 7:27

But Jesus said to her, "Let the children be filled first, for it is not appropriate to take the children's bread and throw it to the dogs."

Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto. Marko 7:28

But she answered him, "Yes, Lord. Yet even the dogs under the table eat the children's crumbs."

Akamwambia, Kwa sababu ya neno hilo, enenda zako, pepo amemtoka binti yako. Marko 7:29

He said to her, "For this saying, go your way. The demon has gone out of your daughter."

Akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka. Marko 7:30

She went away to her house, and found the child having been laid on the bed, with the demon gone out.

Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. Marko 7:31

Again he departed from the borders of Tyre and Sidon, and came to the sea of Galilee, through the midst of the region of Decapolis.

Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. Marko 7:32

They brought to him one who was deaf and had an impediment in his speech. They begged him to lay his hand on him.

Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, Marko 7:33

He took him aside from the multitude, privately, and put his fingers into his ears, and he spat, and touched his tongue.

akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. Marko 7:34

Looking up to heaven, he sighed, and said to him, "Ephphatha!" that is, "Be opened!"

Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. Marko 7:35

Immediately his ears were opened, and the impediment of his tongue was released, and he spoke clearly.

Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari; Marko 7:36

He commanded them that they should tell no one, but the more he commanded them, so much the more widely they proclaimed it.

wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme. Marko 7:37

They were astonished beyond measure, saying, "He has done all things well. He makes even the deaf hear, and the mute speak!"