Marko 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 14 (Swahili) Mark 14 (English)

Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua. Marko 14:1

It was now two days before the feast of the Passover and the unleavened bread, and the chief priests and the scribes sought how they might sieze him by deception, and kill him.

Kwa maana walisema, Isiwe kwa wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu. Marko 14:2

For they said, "Not during the feast, because there might be a riot of the people."

Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake. Marko 14:3

While he was at Bethany, in the house of Simon the leper, as he sat at the table, a woman came having an alabaster jar of ointment of pure nard-- very costly. She broke the jar, and poured it over his head.

Palikuwa na watu waliochukizwa katika nafsi zao wakisema, Kwani kupoteza marhamu namna hii? Marko 14:4

But there were some who were indignant among themselves, saying, "Why has this ointment been wasted?

Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung'unikia sana yule mwanamke. Marko 14:5

For this might have been sold for more than three hundred denarii,{300 denarii was about a years wages for an agricultural laborer.} and given to the poor." They grumbled against her.

Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema; Marko 14:6

But Jesus said, "Leave her alone. Why do you trouble her? She has done a good work for me.

maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote. Marko 14:7

For you always have the poor with you, and whenever you want to, you can do them good; but you will not always have me.

Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko. Marko 14:8

She has done what she could. She has anointed my body beforehand for the burying.

Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake. Marko 14:9

Most assuredly I tell you, wherever this Gospel may be preached throughout the whole world, that which this woman has done will also be spoken of for a memorial of her."

Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale Thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao. Marko 14:10

Judas Iscariot, who was one of the twelve, went away to the chief priests, that he might deliver him to them.

Nao waliposikia walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa. Marko 14:11

They, when they heard it, were glad, and promised to give him money. He sought how he might conveniently deliver him.

Hata siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka? Marko 14:12

On the first day of unleavened bread, when they sacrificed the Passover, his disciples asked him, "Where do you want us to go and make ready that you may eat the Passover?"

Akatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji; mfuateni; Marko 14:13

He sent two of his disciples, and said to them, "Go into the city, and there you will meet a man carrying a pitcher of water. Follow him,

na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, Ki wapi chumba changu cha wageni, niile pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu? Marko 14:14

and wherever he enters in, tell the master of the house, 'The Teacher says, "Where is the guest room, where I may eat the Passover with my disciples?"'

Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni. Marko 14:15

He will himself show you a large upper room furnished and ready. Make ready for us there."

Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka. Marko 14:16

His disciples went out, and came into the city, and found things as he had said to them, and they prepared the Passover.

Basi ilipokuwa jioni yuaja pamoja na wale Thenashara. Marko 14:17

When it was evening he came with the twelve.

Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti. Marko 14:18

As they sat and were eating, Jesus said, "Most assuredly I tell you, one of you will betray me -- he who eats with me."

Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi? Marko 14:19

They began to be sorrowful, and to ask him one by one, "Surely not I?" And another said, "Surely not I?"

Akawaambia, Ni mmoja wa hao Thenashara, ambaye achovya pamoja nami katika kombe. Marko 14:20

He answered them, "It is one of the twelve, he who dips with me in the dish.

Kwa maana Mwana wa Adamu aenda zake kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu; ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. Marko 14:21

For the Son of Man goes, even as it is written about him, but woe to that man by whom the Son of Man is betrayed! It would be better for that man if he had not been born."

Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa, akasema, Twaeni; huu ndio mwili wangu. Marko 14:22

As they were eating, Jesus took bread, and when he had blessed, he broke it, and gave to them, and said, "Take, eat. This is my body."

Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Marko 14:23

He took the cup, and when he had given thanks, he gave to them. They all drank of it.

Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Marko 14:24

He said to them, "This is my blood of the new covenant, which is poured out for many.

Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu. Marko 14:25

Most assuredly I tell you, I will no more drink of the fruit of the vine, until that day when I drink it anew in the Kingdom of God."

Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni. Marko 14:26

When they had sung a hymn, they went out to the Mount of Olives.

Yesu akawaambia, Mtakunguwazwa ninyi nyote kwa ajili yangu usiku huu; kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo watatawanyika. Marko 14:27

Jesus said to them, "All of you will be made to stumble because of me tonight, for it is written, 'I will strike the shepherd, and the sheep will be scattered.'

Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya. Marko 14:28

However, after I am raised up, I will go before you into Galilee."

Petro akamwambia, Hata wajapokunguwazwa wote, lakini siyo mimi. Marko 14:29

But Peter said to him, "Although all will be offended, yet I will not."

Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Marko 14:30

Jesus said to him, "Most assuredly I tell you, that you today, even this night, before the rooster crows twice, you will deny me three times."

Naye akazidi sana kusema, Ijaponipasa kufa nawe, hata hivyo sitakukana kamwe. Na wote wakasema vile vile. Marko 14:31

But he spoke all the more, "If I must die with you, I will not deny you." They all said the same thing.

Kisha wakaja mpaka bustani iitwayo Gethsemane; akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa muda niombapo. Marko 14:32

They came to a place which was named Gethsemane. He said to his disciples, "Sit here, while I pray."

Akamtwaa Petro na Yakobo na Yohana pamoja naye, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika. Marko 14:33

He took with him Peter, James, and John, and began to be greatly troubled and distressed.

Akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe. Marko 14:34

He said to them, "My soul is exceedingly sorrowful, even to death. Stay here, and watch."

Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba ya kuwa, ikiwezekana, saa hiyo imwepuke. Marko 14:35

He went forward a little, and fell on the ground, and prayed that, if it were possible, the hour might pass away from him.

Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe. Marko 14:36

He said, "Abba, Father, all things are possible to you. Please remove this cup from me. However, not what I desire, but what you desire."

Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja? Marko 14:37

He came and found them sleeping, and said to Peter, "Simon, are you sleeping? Couldn't you watch one hour?

Kesheni mwombe, msije mkaingia majaribuni, roho i radhi ila mwili ni dhaifu. Marko 14:38

Watch and pray, that you may not enter into temptation. The spirit indeed is willing, but the flesh is weak."

Akaenda zake tena, akaomba, akisema neno lilo hilo. Marko 14:39

Again he went away, and prayed, saying the same words.

Akaja tena akawakuta wamelala, maana macho yao yamekuwa mazito, wala hawakujua la kumjibu. Marko 14:40

Again he returned, and found them sleeping, for their eyes were very heavy, and they didn't know what to answer him.

Akaja mara ya tatu, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja; tazama, Mwana wa Adamu anatiwa mikononi mwao wenye dhambi. Marko 14:41

He came the third time, and said to them, "Sleep on now, and take your rest. It is enough. The hour has come. Behold, the Son of Man is betrayed into the hands of sinners.

Ondokeni, twendeni zetu; tazama, yule anayenisaliti amekaribia. Marko 14:42

Arise, let us be going. Behold, he who betrays me is at hand."

Basi alipokuwa katika kusema, mara Yuda alifika, mmoja wa wale Thenashara, na pamoja naye mkutano, wana panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani, na waandishi, na wazee. Marko 14:43

Immediately, while he was still speaking, Judas, one of the twelve, came--and with him a multitude with swords and clubs, from the chief priests, the scribes, and the elders.

Na yule anayemsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni, mkamchukue salama. Marko 14:44

Now he who betrayed him had given them a sign, saying, "Whoever I will kiss, that is he. Seize him, and lead him away safely."

Basi alipokuja, mara akamwendea, akasema, Rabi, akambusu. Marko 14:45

When he had come, immediately he came to him, and said, "Rabbi! Rabbi!" and kissed him.

Wakanyosha mikono yao wakamkamata. Marko 14:46

They laid their hands on him, and seized him.

Na mmoja wao waliokuwapo akafuta upanga, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. Marko 14:47

But a certain one of those who stood by drew his sword, and struck the servant of the high priest, and cut off his ear.

Yesu akajibu, akawaambia, Je! Ni kama juu ya mnyang'anyi mmetoka wenye panga na marungu, kunitwaa mimi? Marko 14:48

Jesus answered them, "Have you come out, as against a robber, with swords and clubs to seize me?

Kila siku nalikuwa mbele yenu hekaluni nikifundisha, msinikamate; lakini haya yamekuwa ili maandiko yapate kutimia. Marko 14:49

I was daily with you in the temple teaching, and you didn't arrest me. But this is so that the Scriptures might be fulfilled."

Ndipo wakamwacha, wakakimbia wote. Marko 14:50

They all left him, and fled.

Na kijana mmoja alimfuata, amejitanda mwili wake nguo ya kitani; wakamkamata; Marko 14:51

A certain young man followed him, having a linen cloth thrown around himself, over his naked body. The young men grabbed him,

naye akaiacha ile nguo ya kitani, akakimbia yu uchi. Marko 14:52

but he left the linen cloth, and fled from them naked.

Nao wakamchukua Yesu kwa Kuhani Mkuu; wakamkusanyikia wote, wakuu wa makuhani na wazee na waandishi. Marko 14:53

They led Jesus away to the high priest. All the chief priests, the elders, and the scribes came together with him.

Naye Petro akamfuata kwa mbali, hata ndani katika behewa ya Kuhani Mkuu; akawa ameketi pamoja na watumishi, anakota moto mwangani. Marko 14:54

Peter had followed him from a distance, until he came into the court of the high priest. He was sitting with the officers, and warming himself in the light of the fire.

Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda juu ya Yesu wapate kumwua; wasione. Marko 14:55

Now the chief priests and the whole council sought witnesses against Jesus to put him to death, and found none.

Kwa maana wengi walimshuhudia uongo, walakini ushuhuda wao haukupatana. Marko 14:56

For many gave false testimony against him, and their testimony didn't agree with each other.

Hata wengine wakasimama, wakamshuhudia uongo, wakisema, Marko 14:57

Some stood up, and gave false testimony against him, saying,

Sisi tulimsikia akisema, Mimi nitalivunja hekalu hili lililofanyika kwa mikono, na katika siku tatu nitajenga jingine lisilofanyika kwa mikono. Marko 14:58

"We heard him say, 'I will destroy this temple that is made with hands, and in three days I will build another made without hands.'"

Wala hata hivi ushuhuda wao haukupatana. Marko 14:59

Even so, their testimony did not agree.

Kisha Kuhani Mkuu akasimama katikati, akamwuliza Yesu, akisema, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? Marko 14:60

The high priest stood up in the midst, and asked Jesus, "Have you no answer? What is it which these testify against you?"

Lakini akanyamaza, wala hakujibu neno. Kuhani Mkuu akamwuliza tena, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mtukufu? Marko 14:61

But he stayed quiet, and answered nothing. Again the high priest asked him, "Are you the Christ, the Son of the Blessed?"

Yesu akasema, Mimi ndiye, nanyi mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija na mawingu ya mbinguni. Marko 14:62

Jesus said, "I AM. You will see the Son of Man sitting at the right hand of Power, and coming with the clouds of the sky."

Kuhani Mkuu akararua nguo zake, akisema, Tuna haja gani tena ya mashahidi? Marko 14:63

The high priest tore his clothes, and said, "What further need have we of witnesses?

Mmesikia kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wote wakamhukumu kuwa imempasa kuuawa. Marko 14:64

You have heard the blasphemy! What do you think?" They all condemned him to be worthy of death.

Wengine wakaanza kumtemea mate, wakamfunika uso, na kumpiga makonde, na kumwambia, tabiri. Hata watumishi nao wakampiga makofi. Marko 14:65

Some began to spit on him, and to cover his face, and to beat him with fists, and to tell him, "Prophesy!" The officers struck him with the palms of their hands.

Na Petro alikuwa chini behewani; akaja mmoja wa vijakazi wa Kuhani Mkuu, Marko 14:66

As Peter was in the courtyard below, one of the maids of the high priest came,

akamwona Petro akikota moto; akamkazia macho, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na yule Mnazareti, Yesu. Marko 14:67

and seeing Peter warming himself, she looked at him, and said, "You were also with the Nazarene, Jesus!"

Akakana, akasema, Sijui wala sisikii unayoyasema wewe. Akatoka nje hata ukumbini; jogoo akawika. Marko 14:68

But he denied it, saying, "I neither know, nor understand what you are saying." He went out on the porch, and the rooster crowed.

Na yule kijakazi akamwona tena, akaanza tena kuwaambia waliosimama pale, Huyu ni mmoja wao. Marko 14:69

The maid saw him, and began again to tell those who stood by, "This is one of them."

Akakana tena. Kitambo kidogo tena wale waliosimama pale wakamwambia Petro, Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe. Marko 14:70

But he again denied it. After a little while again those who stood by said to Peter, "You truly are one of them, for you are a Galilean, and your speech shows it."

Akaanza kulaani na kuapiza, Simjui mtu huyu mnayemnena. Marko 14:71

But he began to curse, and to swear, "I don't know this man of whom you speak!"

Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia. Marko 14:72

The rooster crowed the second time. Peter remembered the word, how that Jesus said to him, "Before the rooster crows twice, you will deny me three times." When he thought about that, he wept.