Marko 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 9 (Swahili) Mark 9 (English)

Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu. Marko 9:1

He said to them, "Most assuredly I tell you, there are some standing here who will in no way taste death until they see the Kingdom of God come with power."

Hata baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao; Marko 9:2

After six days Jesus took with him Peter, James, and John, and brought them up onto a high mountain privately by themselves, and he was changed into another form in front of them.

mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe. Marko 9:3

His clothing became glistening, exceedingly white, like snow, such as no launderer on earth can whiten them.

Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu. Marko 9:4

Elijah and Moses appeared to them, and they were talking with Jesus.

Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Marko 9:5

Peter answered Jesus, "Rabbi, it is good for us to be here. Let's make three tents: one for you, one for Moses, and one for Elijah."

Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi. Marko 9:6

For he didn't know what to say, for they were very afraid.

Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. Marko 9:7

A cloud came, overshadowing them, and a voice came out of the cloud, "This is my beloved Son. Listen to him."

Mara hiyo walipotazama huku na huku, hawakuona mtu pamoja nao ila Yesu peke yake. Marko 9:8

Suddenly looking around, they saw no one with them any more, except Jesus only.

Na walipokuwa wakishuka mlimani aliwakataza wasimweleze mtu waliyoyaona, hata Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu. Marko 9:9

As they were coming down from the mountain, he charged them that they should tell no one what things they had seen, until after the Son of Man had risen from the dead.

Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huko kufufuka katika wafu maana yake nini? Marko 9:10

They kept this saying to themselves, questioning what the "rising from the dead" meant.

Wakamwuliza, wakisema, Mbona waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? Marko 9:11

They asked him, saying, "Why do the scribes say that Elijah must come first?"

Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejeza upya yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharauliwa? Marko 9:12

He said to them, "Elijah indeed comes first, and restores all things. How is it written about the Son of Man, that he should suffer many things and be despised?

Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa. Marko 9:13

But I tell you that Elijah has come, and they have also done to him whatever they wanted to, even as it is written about him."

Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; Marko 9:14

Coming to the disciples, he saw a great multitude around them, and scribes questioning them.

mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. Marko 9:15

Immediately all the multitude, when they saw him, were greatly amazed, and running to him greeted him.

Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? Marko 9:16

He asked the scribes, "What are you asking them?"

Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; Marko 9:17

One of the multitude answered, "Teacher, I brought to you my son, who has a mute spirit;

na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. Marko 9:18

and wherever it seizes him, it throws him down, and he foams at the mouth, and grinds his teeth, and wastes away. I asked your disciples to cast it out, and they weren't able."

Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. Marko 9:19

He answered him, "Unbelieving generation, how long shall I be with you? How long shall I bear with you? Bring him to me."

Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. Marko 9:20

They brought him to him, and when he saw him, immediately the spirit convulsed him, and he fell on the ground, wallowing and foaming at the mouth.

Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Marko 9:21

He asked his father, "How long has it been since this has come to him?" He said, "From childhood.

Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Marko 9:22

Often it has cast him both into the fire and into the water, to destroy him. But if you can do anything, have compassion on us, and help us."

Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Marko 9:23

Jesus said to him, "If you can believe, all things are possible to him who believes."

Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Marko 9:24

Immediately the father of the child cried out with tears, "I believe. Help my unbelief!"

Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Marko 9:25

When Jesus saw that a multitude came running together, he rebuked the unclean spirit, saying to him, "You mute and deaf spirit, I command you, come out of him, and never enter him again!"

Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Marko 9:26

Having cried out, and convulsed greatly, it came out of him. The boy became like one dead; so much that most of them said, "He is dead."

Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. Marko 9:27

But Jesus took him by the hand, and raised him up; and he arose.

Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Marko 9:28

When he had come into the house, his disciples asked him privately, "Why couldn't we cast it out?"

Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba. Marko 9:29

He said to them, "This kind can come out by nothing, except by prayer and fasting."

Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua. Marko 9:30

They went out from there, and passed through Galilee. He didn't want anyone to know it.

Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hata akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. Marko 9:31

For he was teaching his disciples, and said to them, "The Son of Man is being handed over to the hands of men, and they will kill him; and when he is killed, on the third day he will rise again."

Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza. Marko 9:32

But they didn't understand the saying, and were afraid to ask him.

Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani? Marko 9:33

He came to Capernaum, and when he was in the house he asked them, "What were you arguing among yourselves on the way?"

Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. Marko 9:34

But they were silent, for they had disputed one with another on the way about who was the greatest.

Akaketi chini, akawaita wale Thenashara akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. Marko 9:35

He sat down, and called the twelve; and he said to them, "If any man wants to be first, he shall be last of all, and servant of all."

Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, Marko 9:36

He took a little child, and set him in the midst of them. Taking him in his arms, he said to them,

Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma. Marko 9:37

"Whoever receives one such little child in my name, receives me, and whoever receives me, doesn't receive me, but him who sent me."

Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. Marko 9:38

John said to him, "Teacher, we saw someone who doesn't follow us casting out demons in your name; and we forbade him, because he doesn't follow us."

Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu akaweza mara kuninenea mabaya; Marko 9:39

But Jesus said, "Don't forbid him, for there is no one who will do a mighty work in my name, and be able quickly to speak evil of me.

kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu. Marko 9:40

For whoever is not against us is on our side.

Kwa kuwa ye yote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake. Marko 9:41

For whoever will give you a cup of water to drink in my name, because you are Christ's, most assuredly I tell you, he will in no way lose his reward.

Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. Marko 9:42

Whoever will cause one of these little ones who believe in me to stumble, it would be better for him if he was thrown into the sea with a millstone hung around his neck.

Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; Marko 9:43

If your hand causes you to stumble, cut it off. It is better for you to enter into life maimed, rather than having your two hands to go into Gehenna,{Gehenna is a word for Hell that originated as the name for a place where live babies were thrown crying into the fire under the arms of the idol, Moloch, to die. This place was so despised by the people after the righteous King Josiah abolished this hideous practice, that not only was it made into a garbage heap, but dead bodies of diseased animals and executed criminals were thrown there and burned.} into the unquenchable fire,

ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
45 Marko 9:44

'where their worm doesn't die, and the fire is not quenched.'

ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Marko 9:46

'where their worm doesn't die, and the fire is not quenched.'

Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; Marko 9:47

If your eye causes you to stumble, cast it out. It is better for you to enter into the Kingdom of God with one eye, rather than having two eyes to be cast into the Gehenna of fire,

ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. Marko 9:48

'where their worm doesn't die, and the fire is not quenched.'

Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto. Marko 9:49

For everyone will be salted with fire, and every sacrifice will be seasoned with salt.

Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi. Marko 9:50

Salt is good, but if the salt has lost its saltiness, with what will you season it? Have salt in yourselves, and be at peace with one another."