Marko 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Marko 12 (Swahili) Mark 12 (English)

Akaanza kusema nao kwa mifano; Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akazungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Marko 12:1

He began to speak to them in parables. "A man planted a vineyard, put a hedge around it, dug a pit for the winepress, built a tower, rented it out to a farmer, and went into another country.

Hata kwa wakati wake akatuma mtumwa kwa wale wakulima, ili apokee kwa wakulima katika matunda ya mizabibu. Marko 12:2

When it was time, he sent a servant to the farmer to get from the farmer his share of the fruit of the vineyard.

Wakamtwaa, wakampiga, wakamtoa nje, hana kitu. Marko 12:3

They took him, beat him, and sent him away empty.

Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, na huyo wakamtia jeraha za kichwa, wakamfanyia jeuri. Marko 12:4

Again, he sent another servant to them; and they threw stones at him, wounded him in the head, and sent him away shamefully treated.

Akamtuma mwingine, huyo wakamwua; na wengine wengi, hawa wakiwapiga na hawa wakiwaua. Marko 12:5

Again he sent another; and they killed him; and many others, beating some, and killing some.

Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu. Marko 12:6

Therefore still having one, his beloved son, he sent him last to them, saying, 'They will respect my son.'

Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. Marko 12:7

But those farmers said among themselves, 'This is the heir. Come, let's kill him, and the inheritance will be ours.'

Wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu. Marko 12:8

They took him, killed him, and cast him out of the vineyard.

basi atafanyaje yule bwana wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine. Marko 12:9

What therefore will the lord of the vineyard do? He will come and destroy the farmers, and will give the vineyard to others.

Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni. Marko 12:10

Haven't you even read this Scripture: 'The stone which the builders rejected, The same was made the head of the corner.

Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu? Marko 12:11

This was from the Lord, It is marvelous in our eyes'?"

Nao wakatafuta kumkamata, wakaogopa mkutano; maana walitambua ya kwamba ule mfano amewanenea wao. Wakamwacha wakaenda zao. Marko 12:12

They tried to seize him, but they feared the multitude; for they perceived that he spoke the parable against them. They left him, and went away.

Wakatuma kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno. Marko 12:13

They sent some of the Pharisees and of the Herodians to him, that they might trap him with words.

Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo? Marko 12:14

When they had come, they asked him, "Teacher, we know that you are honest, and don't defer to anyone; for you aren't partial to anyone, but truly teach the way of God. Is it lawful to pay taxes to Caesar, or not?

Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione. Marko 12:15

Shall we give, or shall we not give?" But he, knowing their hypocrisy, said to them, "Why do you test me? Bring me a denarius, that I may see it."

Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Marko 12:16

They brought it. He said to them, "Whose is this image and inscription?" They said to him, "Caesar's."

Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana. Marko 12:17

Jesus answered them, "Render to Caesar the things that are Caesar's, and to God the things that are God's." They marveled greatly at him.

Kisha Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza na kusema, Marko 12:18

There came to him Sadducees, who say that there is no resurrection. They asked him, saying,

Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao. Marko 12:19

"Teacher, Moses wrote to us, 'If a man's brother dies, and leaves a wife behind him, and leaves no children, that his brother should take his wife, and raise up offspring for his brother.'

Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao. Marko 12:20

There were seven brothers. The first took a wife, and dying left no offspring.

Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika; Marko 12:21

The second took her, and died, leaving no children behind him. The third likewise;

hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. Marko 12:22

and the seven took her and left no children. Last of all the woman also died.

Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye. Marko 12:23

In the resurrection, when they rise, whose wife will she be of them? For the seven had her as a wife."

Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu? Marko 12:24

Jesus answered them, "Isn't this because you are mistaken, not knowing the Scriptures, nor the power of God?

Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni. Marko 12:25

For when they will rise from the dead, they neither marry, nor are given in marriage, but are like angels in heaven.

Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Marko 12:26

But about the dead, that they are raised; haven't you read in the book of Moses, about the Bush, how God spoke to him, saying, 'I am the God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob?'

Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana. Marko 12:27

He is not the God of the dead, but of the living. You are therefore badly mistaken."

Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Marko 12:28

One of the scribes came, and heard them questioning together. Knowing that he had answered them well, asked him, "Which commandment is the greatest of all?"

Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; Marko 12:29

Jesus answered, "The greatest is, 'Hear, Israel, the Lord our God, the Lord is one:

nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Marko 12:30

you shall love the Lord your God with all your heart, and with all your soul, and with all your mind, and with all your strength.' This is the first commandment.

Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Marko 12:31

The second is like this, 'You shall love your neighbor as yourself.' There is no other commandment greater than these."

Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye; Marko 12:32

The scribe said to him, "Truly, teacher, you have said well that he is one, and there is none other but he,

na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia. Marko 12:33

and to love him with all the heart, and with all the understanding, with all the soul, and with all the strength, and to love his neighbor as himself, is more important than all whole burnt offerings and sacrifices."

Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo. Marko 12:34

When Jesus saw that he answered wisely, he said to him, "You are not far from the Kingdom of God." No one dared ask him any question after that.

Hata Yesu alipokuwa akifundisha katika hekalu, alijibu, akasema, Husemaje waandishi ya kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? Marko 12:35

Jesus responded, as he taught in the temple, "How is it that the scribes say that the Christ is the son of David?

Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. Marko 12:36

For David himself said in the Holy Spirit, 'The Lord said to my Lord, Sit at my right hand, Until I make your enemies the footstool of your feet.'

Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha. Marko 12:37

Therefore David himself calls him Lord, so how can he be his son?" The common people heard him gladly.

Akawaambia katika mafundisho yake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, Marko 12:38

In his teaching he said to them, "Beware of the scribes, who like to walk in long robes, and to get greetings in the marketplaces,

na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele katika karamu; Marko 12:39

and the best seats in the synagogues, and the best places at feasts:

ambao hula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu; hawa watapata hukumu iliyo kubwa. Marko 12:40

those who devour widows' houses, and for a pretense make long prayers. These will receive greater condemnation."

Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Marko 12:41

Jesus sat down opposite the treasury, and saw how the multitude cast money into the treasury. Many who were rich cast in much.

Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Marko 12:42

A poor widow came, and she cast in two small brass coins,{Literally, lepta (or widow's mites). Lepta are very small brass coins worth half a quadrans each, which is a quarter of the copper assarion. Lepta are worth less than 1% of an agricultural worker's daily wages.} which equal a quadrans coin.{A quadrans is a coin worth about 1/64 of a denarius. A denarius is about one day's wages for an agricultural laborer.}

Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina; Marko 12:43

He called his disciples to himself, and said to them, "Most assuredly I tell you, this poor widow gave more than all those who are giving into the treasury,

maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia. Marko 12:44

for they all gave out of their abundance, but she, out of her poverty, gave all that she had to live on."