Luka 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 8 (Swahili) Luke 8 (English)

Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, Luka 8:1

It happened soon afterwards, that he went about through cities and villages, preaching and bringing the good news of the Kingdom of God. With him were the twelve,

na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, Luka 8:2

and certain women who had been healed of evil spirits and infirmities: Mary who was called Magdalene, from whom seven demons had gone out;

na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao. Luka 8:3

and Joanna, the wife of Chuzas, Herod's steward; Susanna; and many others; who ministered to them{TR reads "him" instead of "them"} from their possessions.

Mkutano mkuu ulipokutanika, na wale waliotoka kila mji wakimjia, alisema kwa mfano; Luka 8:4

When a great multitude came together, and people from every city were coming to him, he spoke by a parable.

Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Luka 8:5

"The farmer went out to sow his seed. As he sowed, some fell along the road, and it was trampled under foot, and the birds of the sky devoured it.

Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. Luka 8:6

Other seed fell on the rock, and as soon as it grew, it withered away, because it had no moisture.

Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Luka 8:7

Other fell amid the thorns, and the thorns grew with it, and choked it.

Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Luka 8:8

Other fell into the good ground, and grew, and brought forth fruit one hundred times." As he said these things, he called out, "He who has ears to hear, let him hear!"

Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo? Luka 8:9

Then his disciples asked him, "What does this parable mean?"

Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe. Luka 8:10

He said, "To you it is given to know the mysteries of the Kingdom of God, but to the rest in parables; that 'seeing they may not see, and hearing they may not understand.'

Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. Luka 8:11

Now the parable is this: The seed is the word of God.

Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka. Luka 8:12

Those along the road are those who hear, then the devil comes, and takes away the word from their heart, that they may not believe and be saved.

Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Luka 8:13

Those on the rock are they who, when they hear, receive the word with joy; but these have no root, who believe for a while, then fall away in time of temptation.

Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. Luka 8:14

That which fell among the thorns, these are those who have heard, and as they go on their way they are choked with cares, riches, and pleasures of life, and bring no fruit to maturity.

Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia. Luka 8:15

That in the good ground, these are such as in an honest and good heart, having heard the word, hold it tightly, and bring forth fruit with patience.

Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake. Luka 8:16

"No one, when he has lit a lamp, covers it with a container, or puts it under a bed; but puts it on a stand, that those who enter in may see the light.

Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi. Luka 8:17

For nothing is hidden, that will not be revealed; nor anything secret, that will not be known and come to light.

Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho. Luka 8:18

Be careful therefore how you hear. For whoever has, to him will be given; and whoever doesn't have, from him will be taken away even that which he thinks he has."

Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Luka 8:19

His mother and brothers came to him, and they could not come near him for the crowd.

Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe. Luka 8:20

It was told him by some saying, "Your mother and your brothers stand outside, desiring to see you."

Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya. Luka 8:21

But he answered them, "My mother and my brothers are these who hear the word of God, and do it."

Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. Luka 8:22

Now it happened on one of those days, that he entered into a boat, himself and his disciples, and he said to them, "Let's go over to the other side of the lake." So they launched out.

Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. Luka 8:23

But as they sailed, he fell asleep. A wind storm came down on the lake, and they were taking on dangerous amounts of water.

Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari. Luka 8:24

They came to him, and awoke him, saying, "Master, master, we are dying!" He awoke, and rebuked the wind and the raging of the water, and they ceased, and it was calm.

Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii? Luka 8:25

He said to them, "Where is your faith?" Being afraid they marveled, saying one to another, "Who is this, then, that he commands even the winds and the water, and they obey him?"

Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. Luka 8:26

They arrived at the country of the Gadarenes, which is opposite Galilee.

Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini. Luka 8:27

When Jesus stepped ashore, a certain man out of the city who had demons for a long time met him. He wore no clothes, and didn't live in a house, but in the tombs.

Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese. Luka 8:28

When he saw Jesus, he cried out, and fell down before him, and with a loud voice said, "What do I have to do with you, Jesus, you Son of the Most High God? I beg you, don't torment me!"

Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. Luka 8:29

For Jesus was commanding the unclean spirit to come out of the man. For the unclean spirit had often seized the man. He was kept under guard, and bound with chains and fetters. Breaking the bands apart, he was driven by the demon into the desert.

Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. Luka 8:30

Jesus asked him, "What is your name?" He said, "Legion," for many demons had entered into him.

Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni. Luka 8:31

They begged him that he would not command them to go into the abyss.

Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa. Luka 8:32

Now there was there a herd of many pigs feeding on the mountain, and they begged him that he would allow them to enter into those. He allowed them.

Pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, nalo kundi lilitelemka gengeni kwa kasi, wakaingia ziwani, wakafa maji. Luka 8:33

The demons came out from the man, and entered into the pigs, and the herd rushed down the steep bank into the lake, and were drowned.

Wachungaji walipoona lililotokea walikimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Luka 8:34

When those who fed them saw what had happened, they fled, and told it in the city and in the country.

Watu wakatoka kwenda kuliona lililotokea, wakamwendea Yesu, wakamwona mtu yule aliyetokwa na pepo ameketi miguuni pa Yesu, amevaa nguo, ana akili zake; wakaogopa. Luka 8:35

People went out to see what had happened. They came to Jesus, and found the man from whom the demons had gone out, sitting at Jesus' feet, clothed and in his right mind; and they were afraid.

Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza jinsi alivyoponywa yule aliyepagawa na pepo. Luka 8:36

Those who saw it told them how he who had been possessed by demons was healed.

Na jamii ya watu wa nchi ya Wagerasi iliyo kando kando walimwomba aondoke kwao, kwa kuwa walishikwa na hofu nyingi; basi akapanda chomboni, akarudi. Luka 8:37

All the people of the surrounding country of the Gadarenes asked him to depart from them, for they were very much afraid. He entered into the boat, and returned.

Na mtu yule aliyetokwa na pepo alimwomba ruhusa afuatane naye; lakini yeye alimwaga akisema, Luka 8:38

But the man from whom the demons had gone out begged him that he might go with him, but Jesus sent him away, saying,

Rudi nyumbani kwako, ukahubiri yalivyo makuu Mungu aliyokutendea. Akaenda zake, akihubiri katika mji wote, yalivyo makuu mambo aliyotendewa na Yesu. Luka 8:39

"Return to your house, and declare what great things God has done for you." He went his way, proclaiming throughout the whole city what great things Jesus had done for him.

Basi Yesu aliporudi mkutano ulimkaribisha kwa furaha, maana walikuwa wakimngojea wote. Luka 8:40

It happened, when Jesus returned, that the multitude welcomed him, for they were all waiting for him.

Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake; Luka 8:41

Behold, there came a man named Jairus, and he was a ruler of the synagogue. He fell down at Jesus' feet, and begged him to come into his house,

kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga. Luka 8:42

for he had an only daughter, about twelve years of age, and she was dying. But as he went, the multitudes pressed against him.

Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote, Luka 8:43

A woman who had a flow of blood for twelve years, who had spent all her living on physicians, and could not be healed by any,

alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma. Luka 8:44

came behind him, and touched the fringe of his cloak, and immediately the flow of her blood stopped.

Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga. Luka 8:45

Jesus said, "Who touched me?" When all denied it, Peter and those with him said, "Master, the multitudes press and jostle you, and you say, 'Who touched me?'"

Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka. Luka 8:46

But Jesus said, "Someone did touch me, for I perceived that power has gone out of me."

Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara. Luka 8:47

When the woman saw that she was not hidden, she came trembling, and falling down before him declared to him in the presence of all the people the reason why she had touched him, and how she was healed immediately.

Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani. Luka 8:48

He said to her, "Daughter, cheer up. Your faith has made you well. Go in peace."

Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu. Luka 8:49

While he still spoke, one from the ruler of the synagogue's house came, saying to him, "Your daughter is dead. Don't trouble the Teacher."

Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa. Luka 8:50

But Jesus hearing it, answered him, "Don't be afraid. Only believe, and she will be healed."

Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye. Luka 8:51

When he came to the house, he didn't allow anyone to enter in, except Peter, John, James, the father of the child, and her mother.

Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu. Luka 8:52

All were weeping and mourning her, but he said, "Don't weep. She isn't dead, but sleeping."

Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa. Luka 8:53

They were ridiculing him, knowing that she was dead.

Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka. Luka 8:54

But he put them all outside, and taking her by the hand, he called, saying, "Child, arise!"

Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula. Luka 8:55

Her spirit returned, and she rose up immediately. He commanded that something be given to her to eat.

Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia. Luka 8:56

Her parents were amazed, but he charged them to tell no one what had been done.