Luka 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 22 (Swahili) Luke 22 (English)

Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka. Luka 22:1

Now the feast of unleavened bread, which is called the Passover, drew near.

Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu. Luka 22:2

The chief priests and the scribes sought how they might put him to death, for they feared the people.

Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. Luka 22:3

Satan entered into Judas, who was surnamed Iscariot, who was numbered with the twelve.

Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. Luka 22:4

He went away, and talked with the chief priests and captains about how he might deliver him to them.

Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha. Luka 22:5

They were glad, and agreed to give him money.

Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano. Luka 22:6

He consented, and sought an opportunity to deliver him to them in the absence of the multitude.

Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka. Luka 22:7

The day of unleavened bread came, on which the Passover must be sacrificed.

Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila. Luka 22:8

He sent Peter and John, saying, "Go and prepare the Passover for us, that we may eat."

Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? Luka 22:9

They said to him, "Where do you want us to prepare?"

Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. Luka 22:10

He said to them, "Behold, when you have entered into the city, a man carrying a pitcher of water will meet you. Follow him into the house which he enters.

Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? Luka 22:11

Tell the master of the house, 'The Teacher says to you, "Where is the guest room, where I may eat the Passover with my disciples?"'

Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo. Luka 22:12

He will show you a large, furnished upper room. Make preparations there."

Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka. Luka 22:13

They went, found things as he had told them, and they prepared the Passover.

Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. Luka 22:14

When the hour had come, he sat down with the twelve apostles.

Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; Luka 22:15

He said to them, "I have earnestly desired to eat this Passover with you before I suffer,

kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. Luka 22:16

for I tell you, I will no longer by any means eat of it until it is fulfilled in the Kingdom of God."

Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Luka 22:17

He received a cup, and when he had given thanks, he said, "Take this, and share it among yourselves,

Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. Luka 22:18

for I tell you, I will not drink at all again from the fruit of the vine, until the Kingdom of God comes."

Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Luka 22:19

He took bread, and when he had given thanks, he broke it, and gave to them, saying, "This is my body which is given for you. Do this in memory of me."

Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.] Luka 22:20

Likewise, he took the cup after supper, saying, "This cup is the new covenant in my blood, which is poured out for you.

Walakini, tazama, mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani, Luka 22:21

But behold, the hand of him who betrays me is with me on the table.

Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye! Luka 22:22

The Son of Man indeed goes, as it has been determined, but woe to that man through whom he is betrayed!"

Wakaanza kuulizana wao kwa wao, ni yupi miongoni mwao atakayelitenda jambo hilo. Luka 22:23

They began to question among themselves, which of them it was who would do this thing.

Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa. Luka 22:24

There arose also a contention among them, which of them was considered to be greatest.

Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa Wenye fadhili; Luka 22:25

He said to them, "The kings of the Gentiles lord it over them, and those who have authority over them are called 'benefactors.'

lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. Luka 22:26

But not so with you. But one who is the greater among you, let him become as the younger, and one who is governing, as one who serves.

Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye. Luka 22:27

For who is greater, one who sits at the table, or one who serves? Isn't it he who sits at the table? But I am in the midst of you as one who serves.

Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Luka 22:28

But you are those who have continued with me in my trials.

Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; Luka 22:29

I confer on you a kingdom, even as my Father conferred on me,

mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. Luka 22:30

that you may eat and drink at my table in my Kingdom. You will sit on thrones, judging the twelve tribes of Israel."

Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; Luka 22:31

The Lord said, "Simon, Simon, behold, Satan asked to have you, that he might sift you as wheat,

lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. Luka 22:32

but I prayed for you, that your faith wouldn't fail. You, when once you have turned again, establish your brothers{The word for "brothers" here may be also correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."}."

Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni. Luka 22:33

He said to him, "Lord, I am ready to go with you both to prison and to death!"

Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui. Luka 22:34

He said, "I tell you, Peter, the rooster will by no means crow today until you deny that you know me three times."

Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La! Luka 22:35

He said to them, "When I sent you out without purse, and wallet, and shoes, did you lack anything?" They said, "Nothing."

Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho yake akanunue. Luka 22:36

Then he said to them, "But now, whoever has a purse, let him take it, and likewise a wallet. Whoever has none, let him sell his cloak, and buy a sword.

Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake. Luka 22:37

For I tell you that this which is written must still be fulfilled in me: 'He was counted with the lawless.' For that which concerns me has an end."

Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi. Luka 22:38

They said, "Lord, behold, here are two swords." He said to them, "That is enough."

Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye. Luka 22:39

He came out, and went, as his custom was, to the Mount of Olives. His disciples also followed him.

Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. Luka 22:40

When he was at the place, he said to them, "Pray that you don't enter into temptation."

Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, Luka 22:41

He was withdrawn from them about a stone's throw, and he knelt down and prayed,

akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Luka 22:42

saying, "Father, if you are willing, remove this cup from me. Nevertheless, not my will, but yours, be done."

Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Luka 22:43

An angel from heaven appeared to him, strengthening him.

Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.] Luka 22:44

Being in agony he prayed more earnestly. His sweat became like great drops of blood falling down on the ground.

Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni. Luka 22:45

When he rose up from his prayer, he came to the disciples, and found them sleeping because of grief,

Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni. Luka 22:46

and said to them, "Why do you sleep? Rise and pray that you may not enter into temptation."

Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. Luka 22:47

While he was still speaking, behold, a multitude, and he who was called Judas, one of the twelve, was leading them. He came near to Jesus to kiss him.

Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? Luka 22:48

But Jesus said to him, "Judas, do you betray the Son of Man with a kiss?"

Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga? Luka 22:49

When those who were around him saw what was about to happen, they said to him, "Lord, shall we strike with the sword?"

Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Luka 22:50

A certain one of them struck the servant of the high priest, and cut off his right ear.

Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya. Luka 22:51

But Jesus answered, "Let me at least do this"--and he touched his ear, and healed him.

Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi? Luka 22:52

Jesus said to the chief priests, captains of the temple, and elders, who had come against him, "Have you come out as against a robber, with swords and clubs?

Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza. Luka 22:53

When I was with you in the temple daily, you didn't stretch out your hands against me. But this is your hour, and the power of darkness."

Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali. Luka 22:54

They seized him, and led him away, and brought him into the high priest's house. But Peter followed from a distance.

Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye Petro akaketi kati yao. Luka 22:55

When they had kindled a fire in the middle of the courtyard, and had sat down together, Peter sat among them.

Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye. Luka 22:56

A certain servant girl saw him as he sat in the light, and looking intently at him, said, "This man also was with him."

Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. Luka 22:57

He denied Jesus, saying, "Woman, I don't know him."

Baadaye kitambo mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi. Luka 22:58

After a little while someone else saw him, and said, "You also are one of them!" But Peter answered, "Man, I am not!"

Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya. Luka 22:59

After about one hour passed, another confidently affirmed, saying, "Truly this man also was with him, for he is a Galilean!"

Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika. Luka 22:60

But Peter said, "Man, I don't know what you are talking about!" Immediately, while he was still speaking, a rooster crowed.

Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu. Luka 22:61

The Lord turned, and looked at Peter. Then Peter remembered the Lord's word, how he said to him, "Before the rooster crows you will deny me three times."

Akatoka nje akalia kwa majonzi. Luka 22:62

He went out, and wept bitterly.

Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. Luka 22:63

The men who held Jesus mocked him and beat him.

Wakamfunika macho, kisha wakamwuliza-uliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga? Luka 22:64

Having blindfolded him, they struck him on the face and asked him, "Prophesy! Who is the one who struck you?"

Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana. Luka 22:65

They spoke many other things against him, insulting him.

Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema, Luka 22:66

As soon as it was day, the assembly of the elders of the people was gathered together, both chief priests and scribes, and they led him away into their council, saying,

Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa. Luka 22:67

"If you are the Christ, tell us." But he said to them, "If I tell you, you won't believe,

Tena, nikiwauliza, hamtajibu. Luka 22:68

and if I ask, you will in no way answer me or let me go.

Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi. Luka 22:69

From now on, the Son of Man will be seated at the right hand of the power of God."

Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. Luka 22:70

They all said, "Are you then the Son of God?" He said to them, "You say it, because I AM."

Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake. Luka 22:71

They said, "Why do we need any more witness? For we ourselves have heard from his own mouth!"