Luka 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 7 (Swahili) Luke 7 (English)

Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu. Luka 7:1

After he had finished speaking in the hearing of the people, he entered into Capernaum.

Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana. Luka 7:2

A certain centurion's servant, who was dear to him, was sick and at the point of death.

Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake. Luka 7:3

When he heard about Jesus, he sent to him elders of the Jews, asking him to come and save his servant.

Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili; Luka 7:4

When they came to Jesus, they begged him earnestly, saying, "He is worthy for you to do this for him,

maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi. Luka 7:5

for he loves our nation, and he built our synagogue for us."

Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; Luka 7:6

Jesus went with them. When he was now not far from the house, the centurion sent friends to him, saying to him, "Lord, don't trouble yourself, for I am not worthy for you to come under my roof.

kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona. Luka 7:7

Therefore I didn't even think myself worthy to come to you; but say the word, and my servant will be healed.

Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. Luka 7:8

For I also am a man placed under authority, having under myself soldiers. I tell this one, 'Go!' and he goes; and to another, 'Come!' and he comes; and to my servant, 'Do this,' and he does it."

Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona imani kubwa namna hii. Luka 7:9

When Jesus heard these things, he marveled at him, and turned and said to the multitude who followed him, "I tell you, I have not found such great faith, no, not in Israel."

Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima. Luka 7:10

Those who were sent, returning to the house, found that the servant who had been sick was well.

Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. Luka 7:11

It happened soon afterwards, that he went to a city called Nain. Many of his disciples, along with a great multitude, went with him.

Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye. Luka 7:12

Now when he drew near to the gate of the city, behold, one who was dead was carried out, the only son of his mother, and she was a widow. Many people of the city were with her.

Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. Luka 7:13

When the Lord saw her, he had compassion on her, and said to her, "Don't cry."

Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. Luka 7:14

He came near and touched the coffin, and the bearers stood still. He said, "Young man, I tell you, arise!"

Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. Luka 7:15

He who was dead sat up, and began to speak. And he gave him to his mother.

Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. Luka 7:16

Fear took hold of all, and they glorified God, saying, "A great prophet has arisen among us!" and, "God has visited his people!"

Habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote, na katika nchi zote za kando kando. Luka 7:17

This report went out concerning him in the whole of Judea, and in all the surrounding region.

Wanafunzi wa Yohana wakamletea habari za hayo yote. Luka 7:18

The disciples of John told him about all these things.

Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? Luka 7:19

John, calling to himself two of his disciples, sent them to Jesus, saying, "Are you the one who is coming, or should we look for another?"

Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? Luka 7:20

When the men had come to him, they said, "John the Baptizer has sent us to you, saying, 'Are you he who comes, or should we look for another?'"

Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona. Luka 7:21

In that hour he cured many of diseases and plagues and evil spirits; and to many who were blind he gave sight.

Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema. Luka 7:22

Jesus answered them, "Go and tell John the things which you have seen and heard: that the blind receive their sight, the lame walk, the lepers are cleansed, the deaf hear, the dead are raised up, and the poor have good news preached to them.

Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami. Luka 7:23

Blessed is he who is not offended by me."

Basi, wajumbe wa Yohana walipokwisha ondoka, alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? Luka 7:24

When John's messengers had departed, he began to tell the multitudes about John, "What did you go out into the wilderness to see? A reed shaken by the wind?

Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokula raha, wamo katika majumba ya kifalme. Luka 7:25

But what did you go out to see? A man clothed in soft clothing? Behold, those who are gorgeously dressed, and live delicately, are in kings' courts.

Lakini, mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawaambia, na aliye zaidi ya nabii. Luka 7:26

But what did you go out to see? A prophet? Yes, I tell you, and much more than a prophet.

Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako. Luka 7:27

This is he of whom it is written, 'Behold, I send my messenger before your face, Who will prepare your way before you.'

Nami nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana; lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye. Luka 7:28

"For I tell you, among those who are born of women there is not a greater prophet than John the Baptizer, yet he who is least in the Kingdom of God is greater than he."

Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana. Luka 7:29

When all the people and the tax collectors heard this, they declared God to be just, having been baptized with John's baptism.

Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye. Luka 7:30

But the Pharisees and the lawyers rejected the counsel of God, not being baptized by him themselves.

Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini? Luka 7:31

But the Lord said,{So reads TR. MT omits "But the Lord said,"} "To what then will I liken the people of this generation? What are they like?

Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia. Luka 7:32

They are like children who sit in the marketplace, and call one to another, saying, 'We piped to you, and you didn't dance. We mourned, and you didn't weep.'

Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Luka 7:33

For John the Baptizer came neither eating bread nor drinking wine, and you say, 'He has a demon.'

Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi. Luka 7:34

The Son of Man has come eating and drinking, and you say, 'Behold, a gluttonous man, and a drunkard; a friend of tax collectors and sinners!'

Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote. Luka 7:35

Wisdom is justified by all her children."

Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. Luka 7:36

One of the Pharisees invited him to eat with him. He entered into the Pharisee's house, and sat at the table.

Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. Luka 7:37

Behold, a woman in the city who was a sinner, when she knew that he was reclining in the Pharisee's house, she brought an alabaster jar of ointment.

Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu. Luka 7:38

Standing behind at his feet weeping, she began to wet his feet with her tears, and she wiped them with the hair of her head, kissed his feet, and anointed them with the ointment.

Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi. Luka 7:39

Now when the Pharisee who had invited him saw it, he said to himself, "This man, if he were a prophet, would have perceived who and what kind of woman this is who touches him, that she is a sinner."

Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena. Luka 7:40

Jesus answered him, "Simon, I have something to tell you." He said, "Teacher, say on."

Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini. Luka 7:41

"A certain lender had two debtors. The one owed five hundred denarii, and the other fifty.

Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi? Luka 7:42

When they couldn't pay, he forgave them both. Which of them therefore will love him most?"

Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki. Luka 7:43

Simon answered, "He, I suppose, to whom he forgave the most." He said to him, "You have judged correctly."

Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake. Luka 7:44

Turning to the woman, he said to Simon, "Do you see this woman? I entered into your house, and you gave me no water for my feet, but she has wet my feet with her tears, and wiped them with the hair of her head.

Wewe hukunibusu; lakini huyu tangu nilipoingia hakuacha kunibusu sana miguu yangu. Luka 7:45

You gave me no kiss, but she, since the time I came in, has not ceased to kiss my feet.

Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu. Luka 7:46

You didn't anoint my head with oil, but she has anointed my feet with ointment.

Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo. Luka 7:47

Therefore I tell you, her sins, which are many, are forgiven, for she loved much. But to whom little is forgiven, the same loves little."

Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako. Luka 7:48

He said to her, "Your sins are forgiven."

Ndipo wale walioketi chakulani pamoja naye walianza kusema mioyoni mwao, Ni nani huyu hata asamehe dhambi? Luka 7:49

Those who sat at the table with him began to say to themselves, "Who is this who even forgives sins?"

Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani. Luka 7:50

He said to the woman, "Your faith has saved you. Go in peace."