Luka 23 Swahili & English
Listen/Download AudioLuka 23 (Swahili) | Luke 23 (English) |
---|---|
Wakasimama mkutano wote, wakampeleka kwa Pilato. Luka 23:1 |
The whole company of them rose up and brought him before Pilate. |
Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme. Luka 23:2 |
They began to accuse him, saying, "We found this man perverting the nation, forbidding paying taxes to Caesar, and saying that he himself is Christ, a king." |
Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu akamwambia, Wewe wasema. Luka 23:3 |
Pilate asked him, "Are you the King of the Jews?" He answered him, "So you say." |
Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo ovu katika mtu huyu. Luka 23:4 |
Pilate said to the chief priests and the multitudes, "I find no basis for a charge against this man." |
Nao walikaza sana, wakisema, Huwataharakisha watu, akifundisha katika Uyahudi yote, tokea Galilaya mpaka huku. Luka 23:5 |
But they insisted, saying, "He stirs up the people, teaching throughout all Judea, beginning from Galilee even to this place." |
Pilato aliposikia hayo aliuliza kama huyu ni mtu wa Galilaya. Luka 23:6 |
But when Pilate heard Galilee mentioned, he asked if the man was a Galilean. |
Na alipopata habari ya kuwa yu chini ya mamlaka ya Herode, alimpeleka kwa Herode, kwa kuwa yeye naye alikuwapo Yerusalemu siku zile. Luka 23:7 |
When he found out that he was in Herod's jurisdiction, he sent him to Herod, who was also in Jerusalem during those days. |
Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye. Luka 23:8 |
Now when Herod saw Jesus, he was exceedingly glad, for he had wanted to see him for a long time, because he had heard many things about him. He hoped to see some miracle done by him. |
Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote. Luka 23:9 |
He questioned him with many words, but he gave no answers. |
Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana. Luka 23:10 |
The chief priests and the scribes stood, vehemently accusing him. |
Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato. Luka 23:11 |
Herod with his soldiers humiliated him and mocked him. Dressing him in luxurious clothing, they sent him back to Pilate. |
Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao. Luka 23:12 |
Herod and Pilate became friends with each other that very day, for before that they were enemies with each other. |
Na Pilato akawakutanisha wakuu wa makuhani, na wakubwa, na watu, Luka 23:13 |
Pilate called together the chief priests and the rulers and the people, |
akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki; Luka 23:14 |
and said to them, "You brought this man to me as one that perverts the people, and see, I have examined him before you, and found no basis for a charge against this man concerning those things of which you accuse him. |
wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lo lote alilolitenda lipasalo kufa. Luka 23:15 |
Neither has Herod, for I sent you to him, and see, nothing worthy of death has been done by him. |
Kwa hiyo nitamrudi, kisha nitamfungua. [ Luka 23:16 |
I will therefore chastise him and release him." |
Maana ilimlazimu kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa sikukuu.] Luka 23:17 |
Now he had to release one prisoner to them at the feast. |
Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba. Luka 23:18 |
But they all cried out together, saying, "Away with this man! Release to us Barabbas!" -- |
Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina iliyotokea mjini, na kwa uuaji Luka 23:19 |
one who was thrown into prison for a certain revolt in the city, and for murder. |
Basi Pilato alisema nao mara ya pili, kwa vile alivyotaka kumfungua Yesu. Luka 23:20 |
Then Pilate spoke to them again, wanting to release Jesus, |
Lakini wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe. Msulibishe. Luka 23:21 |
but they shouted, saying, "Crucify! Crucify him!" |
Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua. Luka 23:22 |
He said to them the third time, "Why? What evil has this man done? I have found no capital crime in him. I will therefore chastise him and release him." |
Lakini wakatoa sauti zao kwa nguvu sana, wakitaka asulibiwe. Sauti zao zikashinda. Luka 23:23 |
But they were urgent with loud voices, asking that he might be crucified. Their voices and the voices of the chief priests prevailed. |
Pilato akahukumu kwamba haja yao ifanyike. Luka 23:24 |
Pilate decreed that what they asked for should be done. |
Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo. Luka 23:25 |
He released him who had been thrown into prison for insurrection and murder, for whom they asked, but he delivered Jesus up to their will. |
Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu. Luka 23:26 |
When they led him away, they grabbed one Simon of Cyrene, coming from the country, and laid on him the cross, to carry it after Jesus. |
Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea. Luka 23:27 |
A great multitude of the people followed him, including women who also mourned and lamented him. |
Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu. Luka 23:28 |
But Jesus, turning to them, said, "Daughters of Jerusalem, don't weep for me, but weep for yourselves and for your children. |
Kwa maana tazama, siku zitakuja watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. Luka 23:29 |
For behold, the days are coming in which they will say, 'Blessed are the barren, the wombs that never bore, and the breasts that never nursed.' |
Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni. Luka 23:30 |
Then they will begin to tell the mountains, 'Fall on us!' and tell the hills, 'Cover us.' |
Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu? Luka 23:31 |
For if they do these things in the green tree, what will be done in the dry?" |
Wakapelekwa na wawili wengine, wahalifu, wauawe pamoja naye. Luka 23:32 |
There were also others, two criminals, led with him to be put to death. |
Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Luka 23:33 |
When they came to the place that is called The Skull, they crucified him there with the criminals, one on the right and the other on the left. |
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. Luka 23:34 |
Jesus said, "Father, forgive them, for they don't know what they are doing." Dividing his garments among them, they cast lots. |
Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake. Luka 23:35 |
The people stood watching. The rulers with them also scoffed at him, saying, "He saved others. Let him save himself, if this is the Christ of God, his chosen one!" |
Wale askari nao wakamfanyia dhihaka, wakimwendea na kumletea siki, Luka 23:36 |
The soldiers also mocked him, coming to him and offering him vinegar, |
huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe. Luka 23:37 |
and saying, "If you are the King of the Jews, save yourself!" |
Na juu yake palikuwa na anwani; HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Luka 23:38 |
An inscription was also written over him in letters of Greek, Latin, and Hebrew: "THIS IS THE KING OF THE JEWS." |
Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Luka 23:39 |
One of the criminals who was hanged insulted him, saying, "If you are the Christ, save yourself and us!" |
Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Luka 23:40 |
But the other answered, and rebuking him said, "Don't you even fear God, seeing you are under the same condemnation? |
Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Luka 23:41 |
And we indeed justly, for we receive the due reward for our deeds, but this man has done nothing wrong." |
Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Luka 23:42 |
He said to Jesus, "Lord, remember me when you come into your Kingdom." |
Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. Luka 23:43 |
Jesus said to him, "Assuredly I tell you, today you will be with me in Paradise." |
Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, Luka 23:44 |
It was now about the sixth hour{Time was counted from sunrise, so the sixth hour was about noon.}, and darkness came over the whole land until the ninth hour.{3:00 PM} |
jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati. Luka 23:45 |
The sun was darkened, and the veil of the temple was torn in two. |
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu. Luka 23:46 |
Jesus, crying with a loud voice, said, "Father, into your hands I commit my spirit!" Having said this, he breathed his last. |
Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki. Luka 23:47 |
When the centurion saw what was done, he glorified God, saying, "Certainly this was a righteous man." |
Na makutano yote ya watu waliokuwa wamekutanika kutazama mambo hayo, walipoona yaliyotendeka, wakaenda zao kwao, wakijipiga-piga vifua. Luka 23:48 |
All the multitudes that came together to see this, when they saw the things that were done, returned home beating their breasts. |
Na wote waliojuana naye, na wale wanawake walioandamana naye toka Galilaya, wakasimama kwa mbali, wakitazama mambo hayo. Luka 23:49 |
All his acquaintances, and the women who followed with him from Galilee, stood at a distance, watching these things. |
Na tazama, akatoka mtu mmoja, jina lake Yusufu, ambaye ni mtu wa baraza, mtu mwema, mwenye haki; Luka 23:50 |
Behold, a man named Joseph, who was a member of the council, a good and righteous man |
(wala hakulikubali shauri na tendo lao), naye ni mtu wa Arimathaya, mji mmoja wa Wayahudi, tena anautazamia ufalme wa Mungu; Luka 23:51 |
(he had not consented to their counsel and deed), from Arimathaea, a city of the Jews, who was also waiting for the Kingdom of God: |
mtu huyo alikwenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu. Luka 23:52 |
this man went to Pilate, and asked for Jesus' body. |
Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake. Luka 23:53 |
He took it down, and wrapped it in a linen cloth, and laid him in a tomb that was cut in stone, where no one had ever been laid. |
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia. Luka 23:54 |
It was the day of the Preparation, and the Sabbath was drawing near. |
Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa. Luka 23:55 |
The women, who had come with him out of Galilee, followed after, and saw the tomb, and how his body was laid. |
Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa. Luka 23:56 |
They returned, and prepared spices and ointments. On the Sabbath they rested according to the commandment. |