Luka 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 6 (Swahili) Luke 6 (English)

Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao. Luka 6:1

Now it happened on the second Sabbath after the first, that he was going through the grain fields. His disciples plucked the heads of grain, and ate, rubbing them in their hands.

Basi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato? Luka 6:2

But some of the Pharisees said to them, "Why do you do that which is not lawful to do on the Sabbath day?"

Yesu akawajibu akawaambia, Hamkulisoma hata hilo alilolifanya Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wale aliokuwa nao? Luka 6:3

Jesus, answering them, said, "Haven't you read what David did when he was hungry, he, and those who were with him;

Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya Wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao. Luka 6:4

how he entered into the house of God, and took and ate the show bread, and gave also to those who were with him, which is not lawful to eat except for the priests alone?"

Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato. Luka 6:5

He said to them, "The Son of Man is lord of the Sabbath."

Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza. Luka 6:6

It also happened on another Sabbath that he entered into the synagogue and taught. There was a man there, and his right hand was withered.

Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia. Luka 6:7

The scribes and the Pharisees watched him, to see whether he would heal on the Sabbath, that they might find an accusation against him.

Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama. Luka 6:8

But he knew their thoughts; and he said to the man who had the withered hand, "Rise up, and stand in the middle." He arose and stood.

Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza? Luka 6:9

Then Jesus said to them, "I will ask you something: Is it lawful on the Sabbath to do good, or to do harm? To save a life, or to kill?"

Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Luka 6:10

He looked around at them all, and said to the man, "Stretch out your hand." He did, and his hand was restored as sound as the other.

Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu. Luka 6:11

But they were filled with rage, and talked with one another about what they might do to Jesus.

Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Luka 6:12

It happened in these days, that he went out to the mountain to pray, and he continued all night in prayer to God.

Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume; Luka 6:13

When it was day, he called his disciples, and from them he chose twelve, whom he also named apostles:

Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na Andrea nduguye, na Yakobo na Yohana, na Filipo na Bartolomayo, Luka 6:14

Simon, whom he also named Peter; Andrew, his brother; James; John; Philip; Bartholomew;

na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote, Luka 6:15

Matthew; Thomas; James, the son of Alphaeus; Simon, who was called the Zealot;

na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa msaliti. Luka 6:16

Judas the son of James; and Judas Iscariot, who also became a traitor.

Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Uyahudi wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao; Luka 6:17

He came down with them, and stood on a level place, with a crowd of his disciples, and a great number of the people from all Judea and Jerusalem, and the sea coast of Tyre and Sidon, who came to hear him and to be healed of their diseases;

na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu; waliponywa. Luka 6:18

as well as those who were troubled by unclean spirits, and they were being healed.

Na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote. Luka 6:19

All the multitude sought to touch him, for power came out from him and healed them all.

Akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu. Luka 6:20

He lifted up his eyes to his disciples, and said, "Blessed are you who are poor, For yours is the Kingdom of God.

Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka. Luka 6:21

Blessed are you who hunger now, For you will be filled. Blessed are you who weep now, For you will laugh.

Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Luka 6:22

Blessed are you when men shall hate you, and when they shall exclude and mock you, and throw out your name as evil, for the Son of Man's sake.

Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo. Luka 6:23

Rejoice in that day, and leap for joy, for behold, your reward is great in heaven, for their fathers did the same thing to the prophets.

Lakini, ole wenu ninyi mlio na mali, kwa kuwa faraja yenu mmekwisha kuipata. Luka 6:24

"But woe to you who are rich! For you have received your consolation.

Ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, kwa kuwa mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia. Luka 6:25

Woe to you, you who are full now! For you will be hungry. Woe to you who laugh now! For you will mourn and weep.

Ole wenu ninyi watu wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo. Luka 6:26

Woe,{TR adds "to you"} when{TR adds "all"} men speak well of you! For their fathers did the same thing to the false prophets.

Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, Luka 6:27

"But I tell you who hear: love your enemies, do good to those who hate you,

wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi. Luka 6:28

bless those who curse you, and pray for those who mistreat you.

Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu. Luka 6:29

To him who strikes you on the cheek, offer also the other; and from him who takes away your cloak, don't withhold your coat also.

Mpe kila akuombaye, na akunyang'anyaye vitu vyako, usitake akurudishie. Luka 6:30

Give to everyone who asks you, and don't ask him who takes away your goods to give them back again.

Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo. Luka 6:31

"As you would like people to do to you, do exactly so to them.

Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao. Luka 6:32

If you love those who love you, what credit is that to you? For even sinners love those who love them.

Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo. Luka 6:33

If you do good to those who do good to you, what credit is that to you? For even sinners do the same.

Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile. Luka 6:34

If you lend to those from whom you hope to receive, what credit is that to you? Even sinners lend to sinners, to receive back as much.

Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu. Luka 6:35

But love your enemies, and do good, and lend, expecting nothing back; and your reward will be great, and you will be children of the Most High; for he is kind toward the unthankful and evil.

Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Luka 6:36

Therefore be merciful, Even as your Father is also merciful.

Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. Luka 6:37

Don't judge, And you won't be judged. Don't condemn, And you won't be condemned. Set free, And you will be set free.

Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa. Luka 6:38

"Give, and it will be given to you: good measure, pressed down, shaken together, and running over, will be given to you.{literally, into your bosom.} For with the same measure you measure it will be measured back to you."

Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili? Luka 6:39

He spoke a parable to them. "Can the blind guide the blind? Won't they both fall into a pit?

Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake. Luka 6:40

A disciple is not above his teacher, but everyone when he is fully trained will be like his teacher.

Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Luka 6:41

Why do you see the speck of chaff that is in your brother's eye, but don't consider the beam that is in your own eye?

Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako. Luka 6:42

Or how can you tell your brother, 'Brother, let me remove the speck of chaff that is in your eye,' when you yourself don't see the beam that is in your own eye? You hypocrite! First remove the beam from your own eye, and then you can see clearly to remove the speck of chaff that is in your brother's eye.

Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; Luka 6:43

For there is no good tree that brings forth rotten fruit; nor again a rotten tree that brings forth good fruit.

kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Luka 6:44

For each tree is known by its own fruit. For people don't gather figs from thorns, nor do they gather grapes from a bramble bush.

Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake. Luka 6:45

The good man out of the good treasure of his heart brings out that which is good, and the evil man out of the evil treasure of his heart brings out that which is evil, for out of the abundance of the heart, his mouth speaks.

Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? Luka 6:46

"Why do you call me, 'Lord, Lord,' and don't do the things which I say?

Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonyesha mfano wake. Luka 6:47

Everyone who comes to me, and hears my words, and does them, I will show you who he is like.

Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Luka 6:48

He is like a man building a house, who dug and went deep, and laid a foundation on the rock. When a flood arose, the stream broke against that house, and could not shake it, because it was founded on the rock.

Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa. Luka 6:49

But he who hears, and doesn't do, is like a man who built a house on the earth without a foundation, against which the stream broke, and immediately it fell, and the ruin of that house was great."