Luka 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 13 (Swahili) Luke 13 (English)

Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Luka 13:1

Now there were some present at the same time who told him about the Galileans, whose blood Pilate had mixed with their sacrifices.

Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Luka 13:2

Jesus answered them, "Do you think that these Galileans were worse sinners than all the other Galileans, because they suffered such things?

Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Luka 13:3

I tell you, no, but, unless you repent, you will all perish in the same way.

Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Luka 13:4

Or those eighteen, on whom the tower in Siloam fell, and killed them; do you think that they were worse offenders than all the men who dwell in Jerusalem?

Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Luka 13:5

I tell you, no, but, unless you repent, you will all perish in the same way."

Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate. Luka 13:6

He spoke this parable. "A certain man had a fig tree planted in his vineyard, and he came seeking fruit on it, and found none.

Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Luka 13:7

He said to the vine dresser, 'Behold, these three years I have come looking for fruit on this fig tree, and found none. Cut it down. Why does it waste the soil?'

Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; Luka 13:8

He answered, 'Lord, leave it alone this year also, until I dig around it, and fertilize it.

nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate. Luka 13:9

If it bears fruit, fine; but if not, after that, you can cut it down.'"

Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Luka 13:10

He was teaching in one of the synagogues on the Sabbath day.

Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Luka 13:11

Behold, there was a woman who had a spirit of infirmity eighteen years, and she was bent over, and could in no way straighten herself up.

Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Luka 13:12

When Jesus saw her, he called her, and said to her, "Woman, you are freed from your infirmity."

Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Luka 13:13

He laid his hands on her, and immediately she stood up straight, and glorified God.

Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Luka 13:14

The ruler of the synagogue, being indignant because Jesus had healed on the Sabbath, said to the multitude, "There are six days in which men ought to work. Therefore come on those days and be healed, and not on the Sabbath day!"

Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Luka 13:15

Therefore the Lord answered him, "You hypocrites! Doesn't each one of you free his ox or his donkey from the stall on the Sabbath, and lead him away to water?

Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Luka 13:16

Ought not this woman, being a daughter of Abraham, whom Satan had bound eighteen long years, be freed from this bondage on the Sabbath day?"

Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye. Luka 13:17

As he said these things, all his adversaries were disappointed, and all the multitude rejoiced for all the glorious things that were done by him.

Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini? Luka 13:18

He said, "What is the Kingdom of God like? To what shall I compare it?

Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake. Luka 13:19

It is like a grain of mustard seed, which a man took, and put in his own garden. It grew, and became a large tree, and the birds of the sky lodged in its branches."

Akasema mara ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? Luka 13:20

Again he said, "To what shall I compare the Kingdom of God?

Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachacha wote pia. Luka 13:21

It is like yeast, which a woman took and hid in three measures{literally, three sata. 3 sata is about 39 litres or a bit more than a bushel} of flour, until it was all leavened."

Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. Luka 13:22

He went on his way through cities and villages, teaching, and traveling on to Jerusalem.

Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, Luka 13:23

One said to him, "Lord, are they few who are saved?" He said to them,

Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. Luka 13:24

"Strive to enter in by the narrow door, for many, I tell you, will seek to enter in, and will not be able.

Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako; Luka 13:25

When once the master of the house has risen up, and has shut the door, and you begin to stand outside, and to knock at the door, saying, 'Lord, Lord, open to us!' then he will answer and tell you, 'I don't know you or where you come from.'

ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. Luka 13:26

Then you will begin to say, 'We ate and drink in your presence, and you taught in our streets.'

Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Luka 13:27

He will say, 'I tell you, I don't know where you come from. Depart from me, all you workers of iniquity.'

Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. Luka 13:28

There will be weeping and gnashing of teeth, when you see Abraham, Isaac, Jacob, and all the prophets, in the Kingdom of God, and yourselves being thrown outside.

Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu. Luka 13:29

They will come from the east, west, north, and south, and will sit down in the Kingdom of God.

Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho. Luka 13:30

Behold, there are some who are last who will be first, and there are some who are first who will be last."

Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. Luka 13:31

On that same day, some Pharisees came, saying to him, "Get out of here, and go away, for Herod wants to kill you."

Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika. Luka 13:32

He said to them, "Go and tell that fox, 'Behold, I cast out demons and perform cures today and tomorrow, and the third day I complete my mission.

Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu. Luka 13:33

Nevertheless I must go on my way today and tomorrow and the next day, for it can't be that a prophet perish outside of Jerusalem.'

Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka. Luka 13:34

"Jerusalem, Jerusalem, that kills the prophets, and stones those who are sent to her! How often I wanted to gather your children together, like a hen gathers her own brood under her wings, and you refused!

Angalieni, mmeachiwa nyumba yenu! Nami nawaambia, Hamtaniona tena kamwe, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Luka 13:35

Behold, your house is left to you desolate. I tell you, you will not see me, until you say, 'Blessed is he who comes in the name of the Lord!'"