Luka 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 14 (Swahili) Luke 14 (English)

Ikawa alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. Luka 14:1

It happened, when he went into the house of one of the rulers of the Pharisees on a Sabbath to eat bread, that they were watching him.

Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye ugonjwa wa safura. Luka 14:2

Behold, a certain man who had dropsy was in front of him.

Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo? Luka 14:3

Jesus, answering, spoke to the lawyers and Pharisees, saying, "Is it lawful to heal on the Sabbath?"

Wao wakanyamaza. Akamshika, akamponya, akamruhusu aende zake. Luka 14:4

But they were silent. He took him, and healed him, and let him go.

Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa ng'ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya sabato? Luka 14:5

He answered them, "Which of you, if your son{TR reads "donkey" instead of "son"} or an ox fell into a well, wouldn't immediately pull him out on a Sabbath day?"

Nao hawakuweza kujibu maneno haya. Luka 14:6

They couldn't answer him regarding these things.

Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Luka 14:7

He spoke a parable to those who were invited, when he noticed how they chose the best seats, and said to them,

Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, Luka 14:8

"When you are invited by anyone to a marriage feast, don't sit in the best seat, since perhaps someone more honorable than you might be invited by him,

akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Luka 14:9

and he who invited both of you would come and tell you, 'Make room for this person.' Then you would begin, with shame, to take the lowest place.

Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Luka 14:10

But when you are invited, go and sit in the lowest place, so that when he who invited you comes, he may tell you, 'Friend, move up higher.' Then you will be honored in the presence of all who sit at the table with you.

Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Luka 14:11

For everyone who exalts himself will be humbled, and whoever humbles himself will be exalted."

Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Luka 14:12

He also said to the one who had invited him, "When you make a dinner or a supper, don't call your friends, nor your brothers, nor your kinsmen, nor rich neighbors, or perhaps they might also return the favor, and pay you back.

Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, Luka 14:13

But when you make a feast, ask the poor, the maimed, the lame, or the blind;

nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki. Luka 14:14

and you will be blessed, because they don't have the resources to repay you. For you will be repaid in the resurrection of the righteous."

Basi aliposikia hayo mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu. Luka 14:15

When one of those who sat at the table with him heard these things, he said to him, "Blessed is he who will feast in the Kingdom of God!"

Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa akaalika watu wengi, Luka 14:16

But he said to him, "A certain man made a great supper, and he invited many people.

akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Luka 14:17

He sent out his servant at supper time to tell those who were invited, 'Come, for everything is ready now.'

Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Luka 14:18

They all as one began to make excuses. "The first said to him, 'I have bought a field, and I must go and see it. Please have me excused.'

Mwingine akasema, Nimenunua ng'ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Luka 14:19

"Another said, 'I have bought five yoke of oxen, and I must go try them out. Please have me excused.'

Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja. Luka 14:20

"Another said, 'I have married a wife, and therefore I can't come.'

Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya mji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. Luka 14:21

"That servant came, and told his lord these things. Then the master of the house, being angry, said to his servant, 'Go out quickly into the streets and lanes of the city, and bring in the poor, maimed, blind, and lame.'

Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa ingaliko nafasi. Luka 14:22

"The servant said, 'Lord, it is done as you commanded, and there is still room.'

Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. Luka 14:23

"The lord said to the servant, 'Go out into the highways and hedges, and compel them to come in, that my house may be filled.

Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu. Luka 14:24

For I tell you that none of those men who were invited will taste of my supper.'"

Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, Luka 14:25

Now great multitudes were going with him. He turned and said to them,

Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Luka 14:26

"If anyone comes to me, and doesn't hate his own father, mother, wife, children, brothers, and sisters, yes, and his own life also, he can't be my disciple.

Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Luka 14:27

Whoever doesn't bear his own cross, and come after me, can't be my disciple.

Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Luka 14:28

For which of you, desiring to build a tower, doesn't first sit down and count the cost, to see if he has enough to complete it?

Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, Luka 14:29

Or perhaps, when he has laid a foundation, and is not able to finish, everyone who sees begins to mock him,

wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. Luka 14:30

saying, 'This man began to build, and wasn't able to finish.'

Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? Luka 14:31

Or what king, as he goes to encounter another king in war, will not sit down first and consider whether he is able with ten thousand to meet him who comes against him with twenty thousand?

Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali. Luka 14:32

Or else, while the other is yet a great way off, he sends an envoy, and asks for conditions of peace.

Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Luka 14:33

So therefore whoever of you who doesn't renounce all that he has, he can't be my disciple.

Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee? Luka 14:34

Salt is good, but if the salt becomes flat and tasteless, with what do you season it?

Haiifai nchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Luka 14:35

It is fit neither for the soil nor for the manure pile. It is thrown out. He who has ears to hear, let him hear."