Luka 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 4 (Swahili) Luke 4 (English)

Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, Luka 4:1

Jesus, full of the Holy Spirit, returned from the Jordan, and was led by the Spirit into the wilderness

akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. Luka 4:2

for forty days, being tempted by the devil. He ate nothing in those days. Afterward, when they were completed, he was hungry.

Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Luka 4:3

The devil said to him, "If you are the Son of God, command this stone to become bread."

Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Luka 4:4

Jesus answered him, saying, "It is written, 'Man shall not live by bread alone, but by every word of God.'"

Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Luka 4:5

The devil, leading him up on a high mountain, showed him all the kingdoms of the world in a moment of time.

Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Luka 4:6

The devil said to him, "I will give you all this authority, and their glory, for it has been delivered to me; and I give it to whomever I want.

Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Luka 4:7

If you therefore will worship before me, it will all be yours."

Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Luka 4:8

Jesus answered him, "Get behind me Satan! For it is written, 'You shall worship the Lord your God, and him only shall you serve.'"

Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; Luka 4:9

He led him to Jerusalem, and set him on the pinnacle of the temple, and said to him, "If you are the Son of God, cast yourself down from here,

kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; Luka 4:10

for it is written, 'He will give his angels charge concerning you, to guard you;'

na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Luka 4:11

and, 'On their hands they will bear you up, Lest perhaps you dash your foot against a stone.'"

Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Luka 4:12

Jesus answering, said to him, "It has been said, 'You shall not tempt the Lord your God.'"

Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda. Luka 4:13

When the devil had completed every temptation, he departed from him until another time.

Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. Luka 4:14

Jesus returned in the power of the Spirit into Galilee, and news about him spread through all the surrounding area.

Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. Luka 4:15

He taught in their synagogues, being glorified by all.

Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Luka 4:16

He came to Nazareth, where he had been brought up. He entered, as was his custom, into the synagogue on the Sabbath day, and stood up to read.

Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Luka 4:17

The book of the prophet Isaiah was handed to him. He opened the book, and found the place where it was written,

Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Luka 4:18

"The Spirit of the Lord is on me, Because he has anointed me to preach good news to the poor. He has sent me to heal the brokenhearted, To proclaim release to the captives, Recovering of sight to the blind, To deliver those who are crushed,

Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Luka 4:19

And to proclaim the acceptable year of the Lord."

Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Luka 4:20

He closed the book, gave it back to the attendant, and sat down. The eyes of all in the synagogue were fastened on him.

Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Luka 4:21

He began to tell them, "Today, this Scripture has been fulfilled in your hearing."

Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? Luka 4:22

All testified about him, and wondered at the gracious words which proceeded out of his mouth, and they said, "Isn't this Joseph's son?"

Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. Luka 4:23

He said to them, "Doubtless you will tell me this parable, 'Physician, heal yourself! Whatever we have heard done at Capernaum, do also here in your hometown.'"

Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. Luka 4:24

He said, "Most assuredly I tell you, no prophet is acceptable in his hometown.

Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; Luka 4:25

But truly I tell you, there were many widows in Israel in the days of Elijah, when the sky was shut up three years and six months, when a great famine came over all the land.

wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. Luka 4:26

Elijah was sent to none of them, except to Zarephath, in the land of Sidon, to a woman who was a widow.

Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu. Luka 4:27

There were many lepers in Israel in the time of Elisha the prophet, yet not one of them was cleansed, except Naaman, the Syrian."

Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. Luka 4:28

They were all filled with wrath in the synagogue, as they heard these things.

Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; Luka 4:29

They rose up, threw him out of the city, and led him to the brow of the hill that their city was built on, that they might throw him off the cliff.

lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake. Luka 4:30

But he, passing through the midst of them, went his way.

Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato; Luka 4:31

He came down to Capernaum, a city of Galilee. He was teaching them on the Sabbath day,

wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. Luka 4:32

and they were astonished at his teaching, for his word was with authority.

Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, Luka 4:33

In the synagogue there was a man who had a spirit of an unclean demon, and he cried out with a loud voice,

akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Luka 4:34

saying, "Ah! what have we to do with you, Jesus of Nazareth? Have you come to destroy us? I know you who you are: the Holy One of God!"

Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno. Luka 4:35

Jesus rebuked him, saying, "Be silent, and come out of him!" When the demon had thrown him down in their midst, he came out of him, having done him no harm.

Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka. Luka 4:36

Amazement came on all, and they spoke together, one with another, saying, "What is this word? For with authority and power he commands the unclean spirits, and they come out!"

Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile. Luka 4:37

News about him went out into every place of the surrounding region.

Akatoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwomba kwa ajili yake. Luka 4:38

He rose up from the synagogue, and entered into Simon's house. Simon's mother-in-law was afflicted with a great fever, and they begged him for her.

Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia. Luka 4:39

He stood over her, and rebuked the fever; and it left her. Immediately she rose up and served them.

Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya. Luka 4:40

When the sun was setting, all those who had any sick with various diseases brought them to him; and he laid his hands on every one of them, and healed them.

Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo. Luka 4:41

Demons also came out from many, crying out, and saying, "You are the Christ, the Son of God!" Rebuking them, he didn't allow them to speak, because they knew that he was the Christ.

Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafuta-tafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao. Luka 4:42

When it was day, he departed and went into an uninhabited place, and the multitudes looked for him, and came to him, and held on to him, so that he wouldn't go away from them.

Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. Luka 4:43

But he said to them, "I must preach the good news of the Kingdom of God to the other cities also. For this reason I have been sent."

Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya. Luka 4:44

He was preaching in the synagogues of Galilee.