Luka 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 1 (Swahili) Luke 1 (English)

Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu, Luka 1:1

Since many have undertaken to set in order a narrative concerning those matters which have been fulfilled among us,

kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo, Luka 1:2

even as those who from the beginning were eyewitnesses and ministers of the word delivered them to us,

nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu, Luka 1:3

it seemed good to me also, having traced the course of all things accurately from the first, to write to you in order, most excellent Theophilus;

upate kujua hakika ya mambo yale uliyofundishwa. Luka 1:4

that you might know the certainty concerning the things in which you were instructed.

Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti. Luka 1:5

There was in the days of Herod, the king of Judea, a certain priest named Zacharias, of the priestly division of Abijah. He had a wife of the daughters of Aaron, and her name was Elizabeth.

Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. Luka 1:6

They were both righteous before God, walking blamelessly in all the commandments and ordinances of the Lord.

Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Luka 1:7

But they had no child, because Elizabeth was barren, and they both were well advanced in years.

Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, Luka 1:8

Now it happened, while he executed the priest's office before God in the order of his division,

kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. Luka 1:9

according to the custom of the priest's office, his lot was to enter into the temple of the Lord and burn incense.

Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. Luka 1:10

The whole multitude of the people were praying outside at the hour of incense.

Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. Luka 1:11

An angel of the Lord appeared to him, standing on the right side of the altar of incense.

Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. Luka 1:12

Zacharias was troubled when he saw him, and fear fell upon him.

Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Luka 1:13

But the angel said to him, "Don't be afraid, Zacharias, because your request has been heard, and your wife, Elizabeth, will bear you a son, and you shall call his name John.

Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. Luka 1:14

You will have joy and gladness; and many will rejoice at his birth.

Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Luka 1:15

For he will be great in the sight of the Lord, and he will drink no wine nor strong drink. He will be filled with the Holy Spirit, even from his mother's womb.

Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. Luka 1:16

He will turn many of the children of Israel to the Lord, their God.

Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. Luka 1:17

He will go before him in the spirit and power of Elijah, 'to turn the hearts of the fathers to the children,' and the disobedient to the wisdom of the just; to make ready a people prepared for the Lord."

Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi. Luka 1:18

Zacharias said to the angel, "How can I be sure of this? For I am an old man, and my wife is well advanced in years."

Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. Luka 1:19

The angel answered him, "I am Gabriel, who stands in the presence of God. I was sent to speak to you, and to bring you this good news.

Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake. Luka 1:20

Behold, you will be silent and not able to speak, until the day that these things will happen, because you didn't believe my words, which will be fulfilled in their proper time."

Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni. Luka 1:21

The people were waiting for Zacharias, and they marveled that he delayed in the temple.

Alipotoka hali hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu. Luka 1:22

When he came out, he could not speak to them, and they perceived that he had seen a vision in the temple. He continued making signs to them, and remained mute.

Ikawa siku za huduma yake zilipokuwa zimetimia akaenda nyumbani kwake. Luka 1:23

It happened, when the days of his service were fulfilled, he departed to his house.

Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema, Luka 1:24

After these days Elizabeth, his wife, conceived, and she hid herself five months, saying,

Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu. Luka 1:25

"Thus has the Lord done to me in the days in which he looked at me, to take away my reproach among men."

Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, Luka 1:26

Now in the sixth month, the angel Gabriel was sent from God to a city of Galilee, named Nazareth,

kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Luka 1:27

to a virgin pledged to be married to a man whose name was Joseph, of the house of David. The virgin's name was Mary.

Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Luka 1:28

Having come in, the angel said to her, "Rejoice, you highly favored one! The Lord is with you. Blessed are you among women!"

Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Luka 1:29

But when she saw him, she was greatly troubled at the saying, and considered what kind of salutation this might be.

Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Luka 1:30

The angel said to her, "Don't be afraid, Mary, for you have found favor with God.

Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Luka 1:31

Behold, you will conceive in your womb, and bring forth a son, and will call his name 'Jesus.'

Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Luka 1:32

He will be great, and will be called the Son of the Most High. The Lord God will give him the throne of his father, David,

Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. Luka 1:33

and he will reign over the house of Jacob forever. There will be no end to his Kingdom."

Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Luka 1:34

Mary said to the angel, "How can this be, seeing I am a virgin?"

Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Luka 1:35

The angel answered her, "The Holy Spirit will come on you, and the power of the Most High will overshadow you. Therefore also the holy one who is born from you will be called the Son of God.

Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; Luka 1:36

Behold, Elizabeth, your relative, also has conceived a son in her old age; and this is the sixth month with her who was called barren.

kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. Luka 1:37

For everything spoken by God is possible."

Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake. Luka 1:38

Mary said, "Behold, the handmaid of the Lord; be it to me according to your word." The angel departed from her.

Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, Luka 1:39

Mary arose in those days and went into the hill country with haste, into a city of Judah,

akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Luka 1:40

and entered into the house of Zacharias and greeted Elizabeth.

Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; Luka 1:41

It happened, when Elizabeth heard Mary's greeting, that the baby leaped in her womb, and Elizabeth was filled with the Holy Spirit.

akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Luka 1:42

She called out with a loud voice, and said, "Blessed are you among women, and blessed is the fruit of your womb!

Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Luka 1:43

Why am I so favored, that the mother of my Lord should come to me?

Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. Luka 1:44

For behold, when the voice of your greeting came into my ears, the baby leaped in my womb for joy!

Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana. Luka 1:45

Blessed is she who believed, for there will be a fulfillment of the things which have been spoken to her from the Lord!"

Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Luka 1:46

Mary said, "My soul magnifies the Lord.

Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; Luka 1:47

My spirit has rejoiced in God my Savior,

Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Luka 1:48

For he has looked at the humble state of his handmaid. For behold, from now on, all generations will call me blessed.

Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. Luka 1:49

For he who is mighty has done great things for me. Holy is his name.

Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. Luka 1:50

His mercy is for generations of generations on those who fear him.

Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Luka 1:51

He has shown strength with his arm. He has scattered the proud in the imagination of their heart.

Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza. Luka 1:52

He has put down princes from their thrones. And has exalted the lowly.

Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Luka 1:53

He has filled the hungry with good things. He has sent the rich away empty.

Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Luka 1:54

He has given help to Israel, his servant, that he might remember mercy,

Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele. Luka 1:55

As he spoke to our fathers, To Abraham and his seed forever."

Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake. Luka 1:56

Mary stayed with her about three months, and then returned to her house.

Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia, alizaa mtoto mwanamume. Luka 1:57

Now the time that Elizabeth should give birth was fulfilled, and she brought forth a son.

Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye. Luka 1:58

Her neighbors and her relatives heard that the Lord had magnified his mercy towards her, and they rejoiced with her.

Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Luka 1:59

It happened on the eighth day, that they came to circumcise the child; and they would have called him Zacharias, after the name of the father.

Mamaye akajibu akasema La, sivyo; bali, ataitwa Yohana. Luka 1:60

His mother answered, "Not so; but he will be called John."

Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo. Luka 1:61

They said to her, "There is no one among your relatives who is called by this name."

Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita. Luka 1:62

They made signs to his father, what he would have him called.

Akataka kibao, akaandika ya kwamba, Jina lake ni Yohana. Wakastaajabu wote. Luka 1:63

He asked for a writing tablet, and wrote, "His name is John." They all marveled.

Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kunena akimsifu Mungu. Luka 1:64

His mouth was opened immediately, and his tongue freed, and he spoke, blessing God.

Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima milima ya Uyahudi. Luka 1:65

Fear came on all who lived around them, and all these sayings were talked about throughout all the hill country of Judea.

Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu atakuwa wa namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye. Luka 1:66

All who heard them laid them up in their heart, saying, "What then will this child be?" The hand of the Lord was with him.

Na Zakaria, baba yake, akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema, Luka 1:67

His father, Zacharias, was filled with the Holy Spirit, and prophesied, saying,

Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa. Luka 1:68

"Blessed be the Lord, the God of Israel, For he has visited and worked redemption for his people;

Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Luka 1:69

And has raised up a horn of salvation for us in the house of his servant David

Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; Luka 1:70

(As he spoke by the mouth of his holy prophets who have been from of old),

Tuokolewe na adui zetu Na mikononi mwao wote wanaotuchukia; Luka 1:71

Salvation from our enemies, and from the hand of all who hate us;

Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu; Luka 1:72

To show mercy towards our fathers, To remember his holy covenant,

Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu, Luka 1:73

The oath which he spoke to Abraham, our father,

Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu, Luka 1:74

To grant to us that we, being delivered out of the hand of our enemies, should serve him without fear,

Kwa utakatifu na kwa haki Mbele zake siku zetu zote. Luka 1:75

In holiness and righteousness before him all the days of our life.

Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake Aliye juu, Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake; Luka 1:76

And you, child, will be called a prophet of the Most High, For you will go before the face of the Lord to make ready his ways,

Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao. Luka 1:77

To give knowledge of salvation to his people by the remission of their sins,

Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia, Luka 1:78

Because of the tender mercy of our God, Whereby the dawn from on high will visit us,

Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani. Luka 1:79

To shine on those who sit in darkness and the shadow of death; To guide our feet into the way of peace."

Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli. Luka 1:80

The child was growing, and becoming strong in spirit, and was in the desert until the day of his public appearance to Israel.