Luka 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 21 (Swahili) Luke 21 (English)

Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina. Luka 21:1

He looked up, and saw the rich people who were putting their gifts into the treasury.

Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili. Luka 21:2

He saw a certain poor widow casting in two small brass coins.{literally, "two lepta." 2 lepta was about 1% of a day's wages for an agricultural laborer.}

Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote; Luka 21:3

He said, "Truly I tell you, this poor widow put in more than all of them,

maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo. Luka 21:4

for all these put in gifts for God from their abundance, but she, out of her poverty, put in all that she had to live on."

Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema, Luka 21:5

As some were talking about the temple and how it was decorated with beautiful stones and gifts, he said,

Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Luka 21:6

"As for these things which you see, the days will come, in which there will not be left here one stone on another that will not be thrown down."

Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia? Luka 21:7

They asked him, "Teacher, so when will these things be? What is the sign that these things are about to happen?"

Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao. Luka 21:8

He said, "Watch out that you don't get led astray, for many will come in my name, saying, 'I AM,' and, 'The time is at hand.' Therefore don't follow them.

Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi. Luka 21:9

When you hear of wars and disturbances, don't be terrified, for these things must happen first, but the end won't come immediately."

Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; Luka 21:10

Then he said to them, "Nation will rise against nation, and kingdom against kingdom.

kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni. Luka 21:11

There will be great earthquakes, famines, and plagues in various places. There will be terrors and great signs from heaven.

Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu. Luka 21:12

But before all these things, they will lay their hands on you and will persecute you, delivering you up to synagogues and prisons, bringing you before kings and governors for my name's sake.

Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu. Luka 21:13

It will turn out as a testimony for you.

Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu; Luka 21:14

Settle it therefore in your hearts not to meditate beforehand how to answer,

kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga. Luka 21:15

for I will give you a mouth and wisdom which all your adversaries will not be able to withstand or to contradict.

Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu. Luka 21:16

You will be handed over even by parents, brothers, relatives, and friends. Some of you they will cause to be put to death.

Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Luka 21:17

You will be hated by all men for my name's sake.

Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. Luka 21:18

And not a hair of your head will perish.

Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu. Luka 21:19

By your endurance you will win your lives.

Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Luka 21:20

"But when you see Jerusalem surrounded by armies, then know that its desolation is at hand.

Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. Luka 21:21

Then let those who are in Judea flee to the mountains. Let those who are in the midst of her depart. Let those who are in the country not enter therein.

Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa. Luka 21:22

For these are days of vengeance, that all things which are written may be fulfilled.

Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili. Luka 21:23

Woe to those who are pregnant and to those who nurse infants in those days! For there will be great distress in the land, and wrath to this people.

Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia. Luka 21:24

They will fall by the edge of the sword, and will be led captive into all the nations. Jerusalem will be trampled down by the Gentiles, until the times of the Gentiles are fulfilled.

Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake; Luka 21:25

There will be signs in the sun, moon, and stars; and on the earth anxiety of nations, in perplexity for the roaring of the sea and the waves;

watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika. Luka 21:26

men fainting for fear, and for expectation of the things which are coming on the world: for the powers of the heavens will be shaken.

Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Luka 21:27

Then they will see the Son of Man coming in a cloud with power and great glory.

Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia. Luka 21:28

But when these things begin to happen, look up, and lift up your heads, because your redemption is near."

Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote. Luka 21:29

He told them a parable. "See the fig tree, and all the trees.

Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. Luka 21:30

When they are already budding, you see it and know by your own selves that the summer is already near.

Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu. Luka 21:31

Even so you also, when you see these things happening, know that the Kingdom of God is near.

Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie. Luka 21:32

Most assuredly I tell you, this generation will not pass away until all things are accomplished.

Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. Luka 21:33

Heaven and earth will pass away, but my words will by no means pass away.

Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; Luka 21:34

"So be careful, or your hearts will be loaded down with carousing, drunkenness, and cares of this life, and that day will come on you suddenly.

kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. Luka 21:35

For it will come like a snare on all those who dwell on the surface of all the earth.

Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu. Luka 21:36

Therefore be watchful all the time, asking that you may be counted worthy to escape all these things that will happen, and to stand before the Son of Man."

Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni. Luka 21:37

Every day Jesus was teaching in the temple, and every night he would go out and spend the night on the mountain that is called Olivet.

Na watu wote walikuwa wakiamka mapema waende hekaluni ili kumsikiliza. Luka 21:38

All the people came early in the morning to him in the temple to hear him.