Yoshua 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 6 (Swahili) Joshua 6 (English)

Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Yoshua 6:1

Now Jericho was tightly shut up because of the children of Israel: none went out, and none came in.

Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. Yoshua 6:2

Yahweh said to Joshua, Behold, I have given into your hand Jericho, and the king of it, and the mighty men of valor.

Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. Yoshua 6:3

You shall compass the city, all the men of war, going about the city once. Thus shall you do six days.

Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao. Yoshua 6:4

Seven priests shall bear seven trumpets of rams' horns before the ark: and the seventh day you shall compass the city seven times, and the priests shall blow the trumpets.

Kisha itakuwa watakapopiga hizo pembe za kondoo waume kwa nguvu, nanyi mtakaposikia sauti ya tarumbeta, watu wote watapiga kelele kwa sauti kuu; na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale, na hao watu watapanda, kila mtu akiendelea mbele kukabili. Yoshua 6:5

It shall be that when they make a long blast with the ram's horn, and when you hear the sound of the trumpet, all the people shall shout with a great shout; and the wall of the city shall fall down flat, and the people shall go up every man straight before him.

Bali Yoshua, mwana wa Nuni, akawaita makuhani, akawaambia, Lichukueni sanduku la agano, tena makuhani saba na wachukue tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana. Yoshua 6:6

Joshua the son of Nun called the priests, and said to them, Take up the ark of the covenant, and let seven priests bear seven trumpets of rams' horns before the ark of Yahweh.

Naye akawaambia watu, Piteni mbele, mkauzunguke mji, na hao watu wenye silaha na watangulie mbele ya sanduku la Bwana. Yoshua 6:7

They said to the people, Pass on, and compass the city, and let the armed men pass on before the ark of Yahweh.

Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele za Bwana, wakatangulia, wakazipiga hizo tarumbeta; nalo sanduku la agano la Bwana likawafuata. Yoshua 6:8

It was so, that when Joshua had spoken to the people, the seven priests bearing the seven trumpets of rams' horns before Yahweh passed on, and blew the trumpets: and the ark of the covenant of Yahweh followed them.

Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao makuhani waliozipiga tarumbeta, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo sanduku; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. Yoshua 6:9

The armed men went before the priests who blew the trumpets, and the rearward went after the ark, [the priests] blowing the trumpets as they went.

Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lo lote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele. Yoshua 6:10

Joshua commanded the people, saying, You shall not shout, nor let your voice be heard, neither shall any word proceed out of your mouth, until the day I bid you shout; then shall you shout.

Basi akalipeleka sanduku la Bwana liuzunguke huo mji, likauzunguka mara moja, kisha wakaenda kambini wakakaa kambini. Yoshua 6:11

So he caused the ark of Yahweh to compass the city, going about it once: and they came into the camp, and lodged in the camp.

Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichukua sanduku la Bwana. Yoshua 6:12

Joshua rose early in the morning, and the priests took up the ark of Yahweh.

Na wale makuhani saba wakazichukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Bwana, wakaendelea wakazipiga tarumbeta; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la Bwana; makuhani wakizipiga tarumbeta walipokuwa wakienda. Yoshua 6:13

The seven priests bearing the seven trumpets of rams' horns before the ark of Yahweh went on continually, and blew the trumpets: and the armed men went before them; and the rearward came after the ark of Yahweh, [the priests] blowing the trumpets as they went.

Siku ya pili wakauzunguka mji mara moja, wakarejea kambini; ndivyo walivyofanya siku sita. Yoshua 6:14

The second day they compassed the city once, and returned into the camp: so they did six days.

Ikawa siku ya saba wakaondoka asubuhi na mapema wakati wa mapambazuko, wakauzunguka mji vivyo hivyo mara saba; ila siku hiyo waliuzunguka huo mji mara saba. Yoshua 6:15

It happened on the seventh day, that they rose early at the dawning of the day, and compassed the city after the same manner seven times: only on the day they compassed the city seven times.

Hata mara ya saba makuhani walipozipiga tarumbeta, Yoshua akawaambia watu, Pigeni kelele; kwa maana Bwana amewapeni mji huu. Yoshua 6:16

It happened at the seventh time, when the priests blew the trumpets, Joshua said to the people, Shout; for Yahweh has given you the city.

Na mji huu utakuwa wakfu kwa Bwana, mji wenyewe na vitu vyote vilivyomo; isipokuwa Rahabu, yule kahaba, ataishi, yeye na watu wote walio pamoja naye nyumbani, kwa sababu aliwaficha hao wapelelezi tuliowatuma. Yoshua 6:17

The city shall be devoted, even it and all that is therein, to Yahweh: only Rahab the prostitute shall live, she and all who are with her in the house, because she hid the messengers that we sent.

Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha. Yoshua 6:18

But as for you, only keep yourselves from the devoted thing, lest when you have devoted it, you take of the devoted thing; so would you make the camp of Israel accursed, and trouble it.

Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa Bwana; vitaletwa katika hazina ya Bwana. Yoshua 6:19

But all the silver, and gold, and vessels of brass and iron, are holy to Yahweh: they shall come into the treasury of Yahweh.

Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia sauti ya tarumbeta hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka nchi kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akiendelea kukabili mbele; wakautwaa huo mji. Yoshua 6:20

So the people shouted, and [the priests] blew the trumpets; and it happened, when the people heard the sound of the trumpet, that the people shouted with a great shout, and the wall fell down flat, so that the people went up into the city, every man straight before him, and they took the city.

Basi wakaangamiza kabisa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji, wanaume na wanawake, watoto na wazee, na ng'ombe, na kondoo, na punda, kwa makali ya upanga. Yoshua 6:21

They utterly destroyed all that was in the city, both man and woman, both young and old, and ox, and sheep, and donkey, with the edge of the sword.

Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia. Yoshua 6:22

Joshua said to the two men who had spied out the land, Go into the prostitute's house, and bring out there the woman, and all that she has, as you swore to her.

Basi wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli. Yoshua 6:23

The young men the spies went in, and brought out Rahab, and her father, and her mother, and her brothers, and all that she had; all her relatives also they brought out; and they set them outside of the camp of Israel.

Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake; bali fedha, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na vya chuma, wakavitia katika hazina ya nyumba ya Bwana. Yoshua 6:24

They burnt the city with fire, and all that was therein; only the silver, and the gold, and the vessels of brass and of iron, they put into the treasury of the house of Yahweh.

Lakini Yoshua akamhifadhi Rahabu, yule kahaba, na watu wa nyumba ya baba yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo; naye akakaa kati ya Israeli hata leo; kwa sababu aliwaficha wale wajumbe aliowatuma Yoshua ili kuupeleleza mji wa Yeriko. Yoshua 6:25

But Rahab the prostitute, and her father's household, and all that she had, did Joshua save alive; and she lived in the midst of Israel to this day, because she hid the messengers, whom Joshua sent to spy out Jericho.

Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo. Yoshua 6:26

Joshua charged them with an oath at that time, saying, Cursed be the man before Yahweh, that rises up and builds this city Jericho: with the loss of his firstborn shall he lay the foundation of it, and with the loss of his youngest son shall he set up the gates of it.

Basi Bwana alikuwa pamoja na Yoshua; sifa zake zikaenea katika nchi ile yote. Yoshua 6:27

So Yahweh was with Joshua; and his fame was in all the land.