Yoshua 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 22 (Swahili) Joshua 22 (English)

Wakati huo Yoshua akawaita Wareubeni, na Wagadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, Yoshua 22:1

Then Joshua called the Reubenites, and the Gadites, and the half-tribe of Manasseh,

naye akawaambia, Ninyi mmeyaandama hayo yote mliyoamriwa na Musa, mtumishi wa Bwana, nanyi mmeisikia sauti yangu katika yote niliyowaamuru mimi; Yoshua 22:2

and said to them, You have kept all that Moses the servant of Yahweh commanded you, and have listened to my voice in all that I commanded you:

hamkuwaacha hao ndugu zenu siku hizi nyingi hata hivi leo, lakini mmeyashika mausia ya amri ya Bwana, Mungu wenu. Yoshua 22:3

you have not left your brothers these many days to this day, but have kept the charge of the commandment of Yahweh your God.

Na sasa yeye Bwana, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa Bwana, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani. Yoshua 22:4

Now Yahweh your God has given rest to your brothers, as he spoke to them: therefore now turn you, and get you to your tents, to the land of your possession, which Moses the servant of Yahweh gave you beyond the Jordan.

Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa Bwana, aliwaamuru, kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote. Yoshua 22:5

Only take diligent heed to do the commandment and the law which Moses the servant of Yahweh commanded you, to love Yahweh your God, and to walk in all his ways, and to keep his commandments, and to cleave to him, and to serve him with all your heart and with all your soul.

Basi Yoshua akawabarikia, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao. Yoshua 22:6

So Joshua blessed them, and sent them away; and they went to their tents.

Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila ya Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowapeleka waende zao mahemani kwao, akawabarikia, Yoshua 22:7

Now to the one half-tribe of Manasseh Moses had given [inheritance] in Bashan; but to the other half gave Joshua among their brothers beyond the Jordan westward; moreover when Joshua sent them away to their tents, he blessed them,

kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng'ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavao mengi sana; mzigawanye na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu. Yoshua 22:8

and spoke to them, saying, Return with much wealth to your tents, and with very much cattle, with silver, and with gold, and with brass, and with iron, and with very much clothing: divide the spoil of your enemies with your brothers.

Basi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase wakarudi, wakatoka kwa wana wa Israeli katika Shilo, ulioko nchi ya Kanaani, ili waende nchi ya Gileadi, hiyo nchi ya milki yao, waliyokuwa wanaimiliki, sawasawa na amri ya Bwana kwa mkono wa Musa. Yoshua 22:9

The children of Reuben and the children of Gad and the half-tribe of Manasseh returned, and departed from the children of Israel out of Shiloh, which is in the land of Canaan, to go to the land of Gilead, to the land of their possession, which they owned, according to the commandment of Yahweh by Moses.

Nao walipofika pande za Yordani, zilizo katika nchi ya Kanaani, hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na nusu ya kabila ya Manase, wakajenga madhabahu huko karibu na Yordani, iliyoonekana kuwa ni madhabahu kubwa. Yoshua 22:10

When they came to the region about the Jordan, that is in the land of Canaan, the children of Reuben and the children of Gad and the half-tribe of Manasseh built there an altar by the Jordan, a great altar to look on.

Wana wa Israeli walisikia ikinenwa, Tazama, wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wamejenga madhabahu huko upande wa mbele wa nchi ya Kanaani, katika nchi iliyo karibu na Yordani, kwa upande huo ulio milki ya wana wa Israeli. Yoshua 22:11

The children of Israel heard say, Behold, the children of Reuben and the children of Gad and the half-tribe of Manasseh have built an altar in the forefront of the land of Canaan, in the region about the Jordan, on the side that pertains to the children of Israel.

Basi, wana wa Israeli waliposikia habari hiyo, mkutano wote wa wana wa Israeli wakakutanika pamoja huko Shilo, ili waende kupigana nao. Yoshua 22:12

When the children of Israel heard of it, the whole congregation of the children of Israel gathered themselves together at Shiloh, to go up against them to war.

Kisha wana wa Israeli wakatuma wajumbe waende kwa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, hata nchi ya Gileadi; nao ni hawa, Finehasi mwana wa Eleazari kuhani; Yoshua 22:13

The children of Israel sent to the children of Reuben, and to the children of Gad, and to the half-tribe of Manasseh, into the land of Gilead, Phinehas the son of Eleazar the priest,

na pamoja naye wakuu kumi, mkuu mmoja wa nyumba ya mababa kwa ajili ya kila kabila ya Israeli; nao kila mmoja alikuwa ni kichwa cha nyumba ya mababa katika maelfu ya Israeli. Yoshua 22:14

and with him ten princes, one prince of a fathers' house for each of the tribes of Israel; and they were everyone of them head of their fathers' houses among the thousands of Israel.

Nao wakawafikilia hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakasema nao, wakinena, Yoshua 22:15

They came to the children of Reuben, and to the children of Gad, and to the half-tribe of Manasseh, to the land of Gilead, and they spoke with them, saying,

Mkutano wote wa Bwana wanena, Ni kosa gani hili mlilolikosa juu ya Mungu wa Israeli, hata mkakengeuka hivi leo na kuacha kumwandama Bwana, katika kujijengea madhabahu, na kuasi hivi leo juu ya Bwana? Yoshua 22:16

Thus says the whole congregation of Yahweh, What trespass is this that you have committed against the God of Israel, to turn away this day from following Yahweh, in that you have built you an altar, to rebel this day against Yahweh?

Je! Ule uovu wa Peori haututoshi, ambao hamjajitakasa nafsi zenu katika huo hata hivi leo, ijapokuwa ilikuja tauni juu ya mkutano wa Bwana, Yoshua 22:17

Is the iniquity of Peor too little for us, from which we have not cleansed ourselves to this day, although there came a plague on the congregation of Yahweh,

hata ikawa hamna budi hivi leo kugeuka na kuacha kumwandama Bwana? Kisha itakuwa, kwa kuwa ninyi mwamwasi Bwana hivi leo, kwamba kesho yeye atakasirika na mkutano wote wa Israeli. Yoshua 22:18

that you must turn away this day from following Yahweh? and it will be, seeing you rebel today against Yahweh, that tomorrow he will be angry with the whole congregation of Israel.

Basi kwamba hiyo nchi ya milki yenu si tohara, ndipo ninyi vukeni na kuingia nchi ya milki yake Bwana, ambayo maskani ya Bwana inakaa ndani yake, nanyi twaeni milki kati yetu; lakini msimwasi Bwana, wala msituasi sisi, kwa kujijengea madhabahu zaidi ya hiyo madhabahu ya Bwana, Mungu wetu. Yoshua 22:19

However, if the land of your possession be unclean, then pass over to the land of the possession of Yahweh, in which Yahweh's tent dwells, and take possession among us: but don't rebel against Yahweh, nor rebel against us, in building you an altar besides the altar of Yahweh our God.

Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake? Yoshua 22:20

Didn't Achan the son of Zerah commit a trespass in the devoted thing, and wrath fell on all the congregation of Israel? and that man didn't perish alone in his iniquity.

Ndipo hapo wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wakajibu, na kuwaambia hao waliokuwa ni vichwa vya maelfu ya Israeli, wakasema, Yoshua 22:21

Then the children of Reuben and the children of Gad and the half-tribe of Manasseh answered, and spoke to the heads of the thousands of Israel,

Mungu, Mungu Bwana, naam, Mungu, Mungu Bwana, yeye yuajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika uasi, au kama ni katika kosa juu ya Bwana, (usituokoe hivi leo); Yoshua 22:22

The Mighty One, God, Yahweh, the Mighty One, God, Yahweh, he knows; and Israel he shall know: if it be in rebellion, or if in trespass against Yahweh (don't save us this day),

sisi kujijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumwandama Bwana; au kama ni kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye Bwana mwenyewe na alitake jambo hili; Yoshua 22:23

that we have built us an altar to turn away from following Yahweh; or if to offer thereon burnt offering or meal-offering, or if to offer sacrifices of peace-offerings thereon, let Yahweh himself require it;

au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hadhari sana, tena makusudi, huku tukisema, Katika siku zijazo wana wenu yamkini wakanena na wana wetu, na kusema, Ninyi mna nini na Bwana, yeye Mungu wa Israeli? Yoshua 22:24

and if we have not [rather] out of carefulness done this, [and] of purpose, saying, In time to come your children might speak to our children, saying, What have you to do with Yahweh, the God of Israel?

Kwa kuwa yeye Bwana ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati ya sisi na ninyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika Bwana; basi hivyo wana wenu wangewakomesha wana wetu wasimche Bwana. Yoshua 22:25

for Yahweh has made the Jordan a border between us and you, you children of Reuben and children of Gad; you have no portion in Yahweh: so might your children make our children cease from fearing Yahweh.

Kwa ajili ya hayo tulisema, Na tufanye tayari ili kujijengea madhabahu, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala kwa sadaka yo yote; Yoshua 22:26

Therefore we said, Let us now prepare to build us an altar, not for burnt offering, nor for sacrifice:

bali itakuwa ni ushahidi kati ya sisi na ninyi, tena kati ya vizazi vyetu baada yetu, ili kwamba tufanye huo utumishi wa Bwana mbele yake kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika zamani zijazo, Ninyi hamna fungu katika Bwana. Yoshua 22:27

but it shall be a witness between us and you, and between our generations after us, that we may do the service of Yahweh before him with our burnt offerings, and with our sacrifices, and with our peace-offerings; that your children may not tell our children in time to come, You have no portion in Yahweh.

Kwa hiyo tulisema, Itakuwa, hapo watakapotuambia neno kama hilo, au kuwaambia watu wa vizazi vyetu katika zamani zijazo neno kama hilo, ndipo sisi tutawaambia, Angalieni huu mfano wa madhabahu ya Bwana, walioufanya baba zetu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wala kwa ajili ya dhabihu; lakini ni ushahidi kati ya sisi na ninyi. Yoshua 22:28

Therefore said we, It shall be, when they so tell us or to our generations in time to come, that we shall say, Behold the pattern of the altar of Yahweh, which our fathers made, not for burnt offering, nor for sacrifice; but it is a witness between us and you.

Mungu na atuzuie msimwasi Bwana, na kukengeuka hivi leo na kuacha kumwandama Bwana, hata mkajenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, au sadaka za unga, au dhabihu, mbali na ile madhabahu ya Bwana, Mungu wetu, iliyo huko mbele ya maskani yake. Yoshua 22:29

Far be it from us that we should rebel against Yahweh, and turn away this day from following Yahweh, to build an altar for burnt-offering, for meal-offering, or for sacrifice, besides the altar of Yahweh our God that is before his tent.

Basi Finehasi kuhani, na wakuu wa mkutano, maana, ni hao waliokuwa vichwa vya maelfu ya Israeli waliokuwa pamoja naye, hapo walipoyasikia hayo maneno waliyoyasema hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, maneno hayo yaliwaridhia sana. Yoshua 22:30

When Phinehas the priest, and the princes of the congregation, even the heads of the thousands of Israel that were with him, heard the words that the children of Reuben and the children of Gad and the children of Manasseh spoke, it pleased them well.

Naye Finehasi, mwana wa Eleazari, kuhani, akawaambia wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na wana wa Manase, akasema, Siku hii ya leo twajua ya kwamba Bwana yu kati yetu, kwa sababu hamkukosa katika jambo hili mbele ya Bwana; sasa ninyi mmewaokoa wana wa Israeli na mkono wa Bwana. Yoshua 22:31

Phinehas the son of Eleazar the priest said to the children of Reuben, and to the children of Gad, and to the children of Manasseh, This day we know that Yahweh is in the midst of us, because you have not committed this trespass against Yahweh: now have you delivered the children of Israel out of the hand of Yahweh.

Kisha Finehasi, mwana wa Eleazari, kuhani, na hao wakuu, wakarudi na kuwaacha wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakatoka katika nchi ya Gileadi, na kuingia nchi ya Kanaani; wakawarudia wana wa Israeli, wakawapa habari. Yoshua 22:32

Phinehas the son of Eleazar the priest, and the princes, returned from the children of Reuben, and from the children of Gad, out of the land of Gilead, to the land of Canaan, to the children of Israel, and brought them word again.

Wana wa Israeli nao wakaliridhia jambo hilo; nao wana wa Israeli wakamhimidi Mungu, wala hawakusema tena habari ya kuwaendea juu yao kupigana nao, wala kuiharibu nchi waliyoikaa wana wa Reubeni, na wana wa Gadi. Yoshua 22:33

The thing pleased the children of Israel; and the children of Israel blessed God, and spoke no more of going up against them to war, to destroy the land in which the children of Reuben and the children of Gad lived.

Basi hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, wakaiita madhabahu hiyo Edi; wakasema, Kwa kuwa ni ushahidi kati yetu ya kwamba yeye Bwana ndiye Mungu. Yoshua 22:34

The children of Reuben and the children of Gad called the altar [Ed]: For, [said they], it is a witness between us that Yahweh is God.