Yoshua 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 20 (Swahili) Joshua 20 (English)

Kisha Bwana akanena na Yoshua, na kumwambia, Yoshua 20:1

Yahweh spoke to Joshua, saying,

Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Haya, toeni hiyo miji ya makimbilio, ambayo niliwaambia habari zake kwa mkono wa Musa; Yoshua 20:2

Speak to the children of Israel, saying, Assign you the cities of refuge, of which I spoke to you by Moses,

ili kwamba mwenye kuua mtu, aliyemwua mtu awaye yote pasipo kukusudia, na pasipo kujua, apate kukimbilia kuko; nayo itakuwa ni mahali pa kukimbilia kwenu, kumkimbia huyo ajilipizaye kisasi cha damu. Yoshua 20:3

that the manslayer who kills any person unwittingly [and] unawares may flee there: and they shall be to you for a refuge from the avenger of blood.

Naye ataikimbilia miji hiyo mmojawapo, naye atasimama hapo penye maingilio ya lango la huo mji, kisha atanena neno lake masikioni mwa wazee wa mji; nao watamtia kwao ndani ya mji, na kumpa mahali, ili apate kukaa kati yao. Yoshua 20:4

He shall flee to one of those cities, and shall stand at the entrance of the gate of the city, and declare his cause in the ears of the elders of that city; and they shall take him into the city to them, and give him a place, that he may dwell among them.

Na kama huyo mwenye kujilipiza kisasi cha damu akimwandamia, ndipo hawatamtoa huyo mwuaji kumtia mkononi mwake huyo; kwa sababu alimpiga mwenziwe naye hakujua, wala hakumchukia tangu hapo. Yoshua 20:5

If the avenger of blood pursue after him, then they shall not deliver up the manslayer into his hand; because he struck his neighbor unawares, and didn't hate him before.

Naye atakaa katika mji huo, hata hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hata kifo chake kuhani mkuu mwenye kuwapo siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi, na kuuendea mji wake mwenyewe, na nyumba yake mwenyewe, hata mji huo alioutoka hapo alipokimbia. Yoshua 20:6

He shall dwell in that city, until he stand before the congregation for judgment, until the death of the high priest that shall be in those days: then shall the manslayer return, and come to his own city, and to his own house, to the city from whence he fled.

Nao wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya vilima ya Yuda. Yoshua 20:7

They set apart Kedesh in Galilee in the hill-country of Naphtali, and Shechem in the hill-country of Ephraim, and Kiriath Arba (the same is Hebron) in the hill-country of Judah.

Tena ng'ambo ya pili ya Yordani pande za Yeriko upande wa kuelekea mashariki wakaweka Bezeri ulioko nyikani, katika nchi tambarare ya kabila ya Reubeni, na Ramothi katika Gileadi katika kabila ya Gadi, na Golani katika Bashani katika kabila ya Manase. Yoshua 20:8

Beyond the Jordan at Jericho eastward, they assigned Bezer in the wilderness in the plain out of the tribe of Reuben, and Ramoth in Gilead out of the tribe of Gad, and Golan in Bashan out of the tribe of Manasseh.

Miji hiyo ndiyo miji iliyoamriwa kwa ajili ya wana wa Israeli wote, na kwa ajili ya mgeni akaaye kati yao ugenini, ili kwamba mtu awaye yote atakayemwua mtu pasipo kukusudia apate kimbilia huko, asife kwa mkono wa mwenye kujilipiza kisasi cha damu, hata hapo atakapokuwa amekwisha simama mbele ya mkutano. Yoshua 20:9

These were the appointed cities for all the children of Israel, and for the stranger who sojourns among them, that whoever kills any person unwittingly might flee there, and not die by the hand of the avenger of blood, until he stood before the congregation.