Yoshua 17 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 17 (Swahili) Joshua 17 (English)

Kisha hii ndiyo kura iliyoiangukia kabila ya Manase; maana, yeye alikuwa ni mzaliwa wa kwanza, wa Yusufu. Katika habari za Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, babaye Gileadi, kwa sababu alikuwa mtu wa vita, basi alikuwa na Gileadi na Bashani. Yoshua 17:1

[This] was the lot for the tribe of Manasseh; for he was the firstborn of Joseph. As for Machir the firstborn of Manasseh, the father of Gilead, because he was a man of war, therefore he had Gilead and Bashan.

Na kura ilikuwa ni ya hao wana wa Manase waliosalia kwa kuandama jamaa zao; kwa wana wa Abiezeri, na kwa wana wa Heleki, na kwa wana wa Asrieli, na kwa wana wa Shekemu, na kwa wana wa Heferi, na kwa wana wa Shemida; hao ndio wana waume wa Manase, mwana wa Yusufu, kwa kuandama jamaa zao. Yoshua 17:2

So [the lot] was for the rest of the children of Manasseh according to their families: for the children of Abiezer, and for the children of Helek, and for the children of Asriel, and for the children of Shechem, and for the children of Hepher, and for the children of Shemida: these were the male children of Manasseh the son of Joseph according to their families.

Lakini Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, hakuwa na wana waume ila binti; na majina ya hao binti zake walikuwa wakiitwa Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa. Yoshua 17:3

But Zelophehad, the son of Hepher, the son of Gilead, the son of Machir, the son of Manasseh, had no sons, but daughters: and these are the names of his daughters: Mahlah, and Noah, Hoglah, Milcah, and Tirzah.

Nao wakakaribia mbele ya Eleazari, kuhani, na mbele ya Yoshua, mwana wa Nuni, na mbele ya mashehe, wakasema, Bwana alimwamuru Musa kutupa sisi urithi kati ya ndugu zetu; basi kwa kuiandama hiyo amri ya Bwana akawapa urithi kati ya ndugu za baba yao. Yoshua 17:4

They came near before Eleazar the priest, and before Joshua the son of Nun, and before the princes, saying, Yahweh commanded Moses to give us an inheritance among our brothers: therefore according to the commandment of Yahweh he gave them an inheritance among the brothers of their father.

Kisha kura zilizomwangukia Manase zilikuwa ni sehemu kumi, mbali na nchi ya Gileadi na Bashani, iliyo ng'ambo ya Yordani; Yoshua 17:5

There fell ten parts to Manasseh, besides the land of Gilead and Bashan, which is beyond the Jordan;

kwa sababu hao binti za Manase walikuwa na urithi katika wanawe waume; na nchi ya Gileadi ilikuwa ni mali ya hao wana waume wa Manase waliosalia. Yoshua 17:6

because the daughters of Manasseh had an inheritance among his sons. The land of Gilead belonged to the rest of the sons of Manasseh.

Mpaka wa Manase ulikuwa kutoka Asheri hata Mikmeta, ulioelekea Shekemu; tena mpaka ukaendelea upande wa kuume, hata kuwafikilia wenyeji wa Entapua. Yoshua 17:7

The border of Manasseh was from Asher to Michmethath, which is before Shechem; and the border went along to the right hand, to the inhabitants of En Tappuah.

Hiyo nchi ya Tapua ilikuwa ni mali ya Manase; lakini ule mji wa Tapua uliokuwa katika mpaka wa Manase ulikuwa ni mali ya wana wa Efraimu. Yoshua 17:8

The land of Tappuah belonged to Manasseh; but Tappuah on the border of Manasseh belonged to the children of Ephraim.

Tena mpaka ulitelemkia mpaka kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na matokeo yake yalikuwa baharini; Yoshua 17:9

The border went down to the brook of Kanah, southward of the brook: these cities belonged to Ephraim among the cities of Manasseh: and the border of Manasseh was on the north side of the brook, and the goings out of it were at the sea:

upande wa kusini ilikuwa ni mali ya Efraimu, na upande wa kaskazini ilikuwa ni mali ya Manase, na bahari ilikuwa mpaka wake; nao wakafikilia hata Asheri upande wa kaskazini, na kufikilia hata Isakari upande wa mashariki. Yoshua 17:10

southward it was Ephraim's, and northward it was Manasseh's, and the sea was his border; and they reached to Asher on the north, and to Issachar on the east.

Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Bethsheani na vijiji vyake, na Ibleamu na miji yake, na wenyeji wa Dori na miji yake, na wenyeji wa Endori na miji yake, na wenyeji wa Taanaki na miji yake, na wenyeji wa Megido na miji yake, hata mahali patatu palipoinuka. Yoshua 17:11

Manasseh had in Issachar and in Asher Beth-shean and its towns, and Ibleam and its towns, and the inhabitants of Dor and its towns, and the inhabitants of En-dor and its towns, and the inhabitants of Taanach and its towns, and the inhabitants of Megiddo and its towns, even the three heights.

Lakini wana wa Manase hawakuweza kuwafukuza wenyeji wa miji hiyo; bali hao Wakanaani walijikaza ili wakae katika nchi hiyo. Yoshua 17:12

Yet the children of Manasseh couldn't drive out [the inhabitants of] those cities; but the Canaanites would dwell in that land.

Kisha ikawa, hapo hao wana wa Israeli walipokuwa wamepata nguvu zaidi, ndipo wakawatenza nguvu hao Wakanaani wafanye kazi ya shokoa, wala hawakuwafukuza kabisa. Yoshua 17:13

It happened, when the children of Israel had grown strong, that they put the Canaanites to forced labor, and didn't utterly drive them out.

Kisha wana wa Yusufu wakanena na Yoshua, wakasema, Kwa nini umenipa mimi kura moja tu na fungu moja kuwa ni urithi wangu, kwa kuwa mimi ni taifa kubwa la watu, kwa sababu Bwana amenibarikia hata hivi sasa? Yoshua 17:14

The children of Joseph spoke to Joshua, saying, Why have you given me but one lot and one part for an inheritance, seeing I am a great people, because hitherto Yahweh has blessed me?

Yoshua akawaambia, Kwamba wewe u taifa kubwa la watu, haya, kwea uende mwituni, ujikatie mahali hapo kwa ajili ya nafsi yako katika nchi ya Waperizi, na ya hao Warefai; ikiwa hiyo nchi ya vilima ya Efraimu ni nyembamba, haikutoshi. Yoshua 17:15

Joshua said to them, If you are a great people, go up to the forest, and cut down for yourself there in the land of the Perizzites and of the Rephaim; since the hill-country of Ephraim is too narrow for you.

Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Bethsheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia. Yoshua 17:16

The children of Joseph said, The hill-country is not enough for us: and all the Canaanites who dwell in the land of the valley have chariots of iron, both they who are in Beth-shean and its towns, and they who are in the valley of Jezreel.

Kisha Yoshua alinena na nyumba ya Yusufu, maana, ni Efraimu na Manase, akawaambia, Wewe u taifa kubwa la watu, nawe una uwezo mwingi; hutapata kura moja tu; Yoshua 17:17

Joshua spoke to the house of Joseph, even to Ephraim and to Manasseh, saying, You are a great people, and have great power; you shall not have one lot only:

lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa ni mwitu, wewe utaukata, na matokeo yake yatakuwa ni yako; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo. Yoshua 17:18

but the hill-country shall be yours; for though it is a forest, you shall cut it down, and the goings out of it shall be yours; for you shall drive out the Canaanites, though they have chariots of iron, and though they are strong.