Yoshua 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 12 (Swahili) Joshua 12 (English)

Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao wana wa Israeli waliwapiga na kuimiliki nchi yao ng'ambo ya pili ya Yordani, upande wa maawio ya jua, kutoka bonde la Amoni mpaka mlima wa Hermoni, na nchi yote ya Araba upande wa mashariki; Yoshua 12:1

Now these are the kings of the land, whom the children of Israel struck, and possessed their land beyond the Jordan toward the sunrise, from the valley of the Arnon to Mount Hermon, and all the Arabah eastward:

Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekaa huko Heshboni, naye ndiye aliyetawala toka Aroeri, ulioko kando ya bonde la Arnoni, na toka huo mji ulio katikati ya bonde, na nusu ya Gileadi, hata kuufikilia mto wa Yaboki, mpaka wa hao wana wa Amoni; Yoshua 12:2

Sihon king of the Amorites, who lived in Heshbon, and ruled from Aroer, which is on the edge of the valley of the Arnon, and [the city that is in] the middle of the valley, and half Gilead, even to the river Jabbok, the border of the children of Ammon;

na nchi ya Araba mpaka bahari ya Kinerethi, kuelekea mashariki, tena mpaka bahari ya Ataba, mpaka Bahari ya Chumvi, kwendea mashariki, njia ya kwendea Beth-yeshimothi; tena upande wa kusini, chini ya matelemko ya Pisga; Yoshua 12:3

and the Arabah to the sea of Chinneroth, eastward, and to the sea of the Arabah, even the Salt Sea, eastward, the way to Beth-jeshimoth; and on the south, under the slopes of Pisgah:

tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei, Yoshua 12:4

and the border of Og king of Bashan, of the remnant of the Rephaim, who lived at Ashtaroth and at Edrei,

naye alitawala katika mlima wa Hermoni, na katika Saleka, na katika Bashani yote, hata mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na nusu ya Gileadi, mpaka wa huyo Sihoni mfalme wa Heshboni. Yoshua 12:5

and ruled in Mount Hermon, and in Salecah, and in all Bashan, to the border of the Geshurites and the Maacathites, and half Gilead, the border of Sihon king of Heshbon.

Musa mtumishi wa Bwana na wana wa Israeli wakawapiga; naye Musa mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase iwe urithi wao. Yoshua 12:6

Moses the servant of Yahweh and the children of Israel struck them: and Moses the servant of Yahweh gave it for a possession to the Reubenites, and the Gadites, and the half-tribe of Manasseh.

Hawa ni wafalme wa hiyo nchi ambao Yoshua na wana wa Israeli waliwapiga ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa magharibi, kutoka Baal-gadi katika bonde la Lebanoni mpaka kilima cha Halaki, kilichoelekea Seiri; Yoshua naye akawapa kabila za Israeli iwe milki yao sawasawa na magawanyo yao; Yoshua 12:7

These are the kings of the land whom Joshua and the children of Israel struck beyond the Jordan westward, from Baal Gad in the valley of Lebanon even to Mount Halak, that goes up to Seir; and Joshua gave it to the tribes of Israel for a possession according to their divisions;

katika nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika nchi ya Araba, na katika matelemko, na katika bara, na katika Negebu; nchi ya Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi; Yoshua 12:8

in the hill-country, and in the lowland, and in the Arabah, and in the slopes, and in the wilderness, and in the South; the Hittite, the Amorite, and the Canaanite, the Perizzite, the Hivite, and the Jebusite:

mfalme wa Yeriko, mmoja; mfalme wa Ai, ulio karibu na Betheli, mmoja; Yoshua 12:9

the king of Jericho, one; the king of Ai, which is beside Bethel, one;

mfalme wa Yerusalemu, mmoja; mfalme wa Hebroni, mmoja; Yoshua 12:10

the king of Jerusalem, one; the king of Hebron, one;

mfalme wa Yarmuthi, mmoja; na mfalme wa Lakishi, mmoja; Yoshua 12:11

the king of Jarmuth, one; the king of Lachish, one;

mfalme wa Egloni, mmoja; na mfalme wa Gezeri, mmoja; Yoshua 12:12

the king of Eglon, one; the king of Gezer, one;

mfalme wa Debiri, mmoja; na mfalme wa Gederi, mmoja; Yoshua 12:13

the king of Debir, one; the king of Geder, one;

mfalme wa Horma, mmoja; na mfalme wa Aradi, mmoja; Yoshua 12:14

the king of Hormah, one; the king of Arad, one;

mfalme wa Libna, mmoja; na mfalme wa Adulamu, mmoja; Yoshua 12:15

the king of Libnah, one; the king of Adullam, one;

mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja; Yoshua 12:16

the king of Makkedah, one; the king of Bethel, one;

mfalme wa Tapua, mmoja; na mfalme wa Heferi, mmoja; Yoshua 12:17

the king of Tappuah, one; the king of Hepher, one;

mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja; Yoshua 12:18

the king of Aphek, one; the king of Lassharon, one;

mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja; Yoshua 12:19

the king of Madon, one; the king of Hazor, one;

mfalme wa Shimron-meroni, mmoja; na mfalme wa Akshafu, mmoja; Yoshua 12:20

the king of Shimron-meron, one; the king of Achshaph, one;

mfalme wa Taanaki, mmoja; na mfalme wa Megido, mmoja; Yoshua 12:21

the king of Taanach, one; the king of Megiddo, one;

na mfalme wa Kedeshi, mmoja; mfalme wa Yokneamu wa Karmeli, mmoja; Yoshua 12:22

the king of Kedesh, one; the king of Jokneam in Carmel, one;

mfalme wa Dori katika kilima cha Dori, mmoja; na mfalme wa makabila katika Gilgali, mmoja; Yoshua 12:23

the king of Dor in the height of Dor, one; the king of Goiim in Gilgal, one;

na mfalme wa Tirsa, mmoja; wafalme hao wote walikuwa ni thelathini na mmoja. Yoshua 12:24

the king of Tirzah, one: all the kings thirty-one.