Yoshua 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 9 (Swahili) Joshua 9 (English)

Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo; Yoshua 9:1

It happened, when all the kings who were beyond the Jordan, in the hill-country, and in the lowland, and on all the shore of the great sea in front of Lebanon, the Hittite, and the Amorite, the Canaanite, the Perizzite, the Hivite, and the Jebusite, heard of it;

ndipo walipojikutanisha pamoja wenyewe kwa wenyewe, ili kupigana na Yoshua, na hao Israeli, kwa nia moja. Yoshua 9:2

that they gathered themselves together, to fight with Joshua and with Israel, with one accord.

Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai, Yoshua 9:3

But when the inhabitants of Gibeon heard what Joshua had done to Jericho and to Ai,

wao wakatenda kwa hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyoraruka-raruka, na kutiwa viraka; Yoshua 9:4

they also resorted to a ruse, and went and made as if they had been ambassadors, and took old sacks on their donkeys, and wine-skins, old and torn and bound up,

na viatu vilivyotoboka na kushonwa-shonwa katika miguu yao, na mavao makuukuu waliyokuwa wanavaa; tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa umekauka na kuingia koga. Yoshua 9:5

and old and patched shoes on their feet, and old garments on them; and all the bread of their provision was dry and was become moldy.

Nao wakamwendea Yoshua hata maragoni huko Gilgali, nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi. Yoshua 9:6

They went to Joshua to the camp at Gilgal, and said to him, and to the men of Israel, We are come from a far country: now therefore make you a covenant with us.

Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mwakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi? Yoshua 9:7

The men of Israel said to the Hivites, What if you dwell among us; and how shall we make a covenant with you?

Nao wakamwambia Yoshua, Sisi tu watumishi wako. Yoshua akawauliza, Ninyi ni nani? Nanyi mwatoka wapi? Yoshua 9:8

They said to Joshua, We are your servants. Joshua said to them, Who are you? and from whence come you?

Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la Bwana, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri, Yoshua 9:9

They said to him, From a very far country your servants are come because of the name of Yahweh your God: for we have heard the fame of him, and all that he did in Egypt,

na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi. Yoshua 9:10

and all that he did to the two kings of the Amorites, who were beyond the Jordan, to Sihon king of Heshbon, and to Og king of Bashan, who was at Ashtaroth.

Kisha wazee wetu, na wenyeji wote wa nchi yetu, walinena nasi na kutuambia, Chukueni vyakula mkononi mwenu kwa ajili ya safari, mwende mkawalaki watu hao, na kuwaambia, Sisi tu watumishi wenu; basi sasa fanyeni agano nasi. Yoshua 9:11

Our elders and all the inhabitants of our country spoke to us, saying, Take provision in your hand for the journey, and go to meet them, and tell them, We are your servants: and now make you a covenant with us.

Huu mkate wetu tuliutwaa ukali moto katika nyumba zetu, siku hiyo tuliyotoka kuja kwenu, uwe chakula chetu; lakini sasa, tazama, umekauka, na kuingia koga; Yoshua 9:12

This our bread we took hot for our provision out of our houses on the day we came forth to go to you; but now, behold, it is dry, and is become moldy:

na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa ni vipya; sasa, tazama, vimeraruka-raruka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana. Yoshua 9:13

and these wine-skins, which we filled, were new; and, behold, they are torn: and these our garments and our shoes are become old by reason of the very long journey.

Basi hao watu wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa Bwana. Yoshua 9:14

The men took of their provision, and didn't ask counsel at the mouth of Yahweh.

Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia. Yoshua 9:15

Joshua made peace with them, and made a covenant with them, to let them live: and the princes of the congregation swore to them.

Kisha ikawa, mwisho wa siku ya tatu baada ya kufanya hilo agano nao, walisikia habari ya kuwa watu hao ni jirani zao, na ya kwamba waliketi kati yao. Yoshua 9:16

It happened at the end of three days after they had made a covenant with them, that they heard that they were their neighbors, and that they lived among them.

Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikilia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu. Yoshua 9:17

The children of Israel traveled, and came to their cities on the third day. Now their cities were Gibeon, and Chephirah, and Beeroth, and Kiriath Jearim.

Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung'unikia hao wakuu. Yoshua 9:18

The children of Israel didn't strike them, because the princes of the congregation had sworn to them by Yahweh, the God of Israel. All the congregation murmured against the princes.

Lakini wakuu wote waliwaambia mkutano wote, Sisi tumewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli; basi sasa hatuwezi kuwagusa watu hawa. Yoshua 9:19

But all the princes said to all the congregation, We have sworn to them by Yahweh, the God of Israel: now therefore we may not touch them.

Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho kiapo tulichowaapia. Yoshua 9:20

This we will do to them, and let them live; lest wrath be on us, because of the oath which we swore to them.

Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia. Yoshua 9:21

The princes said to them, Let them live: so they became wood cutters and drawers of water to all the congregation, as the princes had spoken to them.

Basi Yoshua akawaita, akanena nao, na kuwaambia, Mbona ninyi mmetudanganya, huku mkisema, Sisi tu mbali sana na ninyi; nanyi kumbe! Mwakaa kati yetu? Yoshua 9:22

Joshua called for them, and he spoke to them, saying, Why have you deceived us, saying, We are very far from you; when you dwell among us?

Basi sasa mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu. Yoshua 9:23

Now therefore you are cursed, and there shall never fail to be of you bondservants, both wood cutters and drawers of water for the house of my God.

Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo Bwana, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili. Yoshua 9:24

They answered Joshua, and said, Because it was certainly told your servants, how that Yahweh your God commanded his servant Moses to give you all the land, and to destroy all the inhabitants of the land from before you; therefore we were sore afraid for our lives because of you, and have done this thing.

Basi sasa, tazama, sisi tu mkononi mwako; basi kama uonavyo kuwa ni vyema na haki kwako wewe kututenda, tutende vivyo. Yoshua 9:25

Now, behold, we are in your hand: as it seems good and right to you to do to us, do.

Naye akawafanyia hivyo, na kuwaokoa na mkono wa wana wa Israeli, ili wasiwaue. Yoshua 9:26

So did he to them, and delivered them out of the hand of the children of Israel, that they didn't kill them.

Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua. Yoshua 9:27

That day Joshua made those wood cutters and drawers of water for the congregation, and for the altar of Yahweh, to this day, in the place which he should choose.