Yoshua 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 13 (Swahili) Joshua 13 (English)

Basi Yoshua alipokuwa mzee, na kwendelea sana miaka yake, Bwana akamwambia, Wewe umekuwa mzee na kwendelea sana miaka yako, kisha inasalia nchi nyingi sana bado kumilikiwa. Yoshua 13:1

Now Joshua was old and well stricken in years; and Yahweh said to him, You are old and well stricken in years, and there remains yet very much land to be possessed.

Nchi iliyosalia ni hii; nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote; Yoshua 13:2

This is the land that yet remains: all the regions of the Philistines, and all the Geshurites;

kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; mashehe matano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi, Yoshua 13:3

from the Shihor, which is before Egypt, even to the border of Ekron northward, [which] is reckoned to the Canaanites; the five lords of the Philistines; the Gazites, and the Ashdodites, the Ashkelonites, the Gittites, and the Ekronites; also the Avvim,

upande wa kusini; nchi yote ya Wakanaani na Meara iliyo ya Wasidoni, mpaka Afeka, hata mpaka wa Waamori; Yoshua 13:4

on the south; all the land of the Canaanites, and Mearah that belongs to the Sidonians, to Aphek, to the border of the Amorites;

na nchi ya Wagebali na Lebanoni yote, upande wa kuelekea maawio ya jua, kutoka Baal-gadi ulio chini ya mlima wa Hermoni mpaka kufikilia maingilio ya Hamathi; Yoshua 13:5

and the land of the Gebalites, and all Lebanon, toward the sunrise, from Baal Gad under Mount Hermon to the entrance of Hamath;

na watu wote wenye kuikaa nchi ya vilima kutoka Lebanoni hata Misrefoth-maimu, maana, hao Wasidoni wote; hao wote nitawafukuza watoke mbele ya wana wa Israeli; lakini wewe uwape Israeli kuwa ni urithi wao, kama nilivyokuamuru. Yoshua 13:6

all the inhabitants of the hill-country from Lebanon to Misrephoth Maim, even all the Sidonians; them will I drive out from before the children of Israel: only allot you it to Israel for an inheritance, as I have commanded you.

Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila kenda, na nusu ya kabila ya Manase. Yoshua 13:7

Now therefore divide this land for an inheritance to the nine tribes, and the half-tribe of Manasseh.

Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa Bwana alivyowapa; Yoshua 13:8

With him the Reubenites and the Gadites received their inheritance, which Moses gave them, beyond the Jordan eastward, even as Moses the servant of Yahweh gave them:

kutoka huko Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulio pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni; Yoshua 13:9

from Aroer, that is on the edge of the valley of the Arnon, and the city that is in the middle of the valley, and all the plain of Medeba to Dibon;

na miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni, hata mpaka wa wana wa Amoni; Yoshua 13:10

and all the cities of Sihon king of the Amorites, who reigned in Heshbon, to the border of the children of Ammon;

na Gileadi na mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na mlima wa Hermoni wote, na Bashani yote mpaka Saleka; Yoshua 13:11

and Gilead, and the border of the Geshurites and Maacathites, and all Mount Hermon, and all Bashan to Salecah;

ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza. Yoshua 13:12

all the kingdom of Og in Bashan, who reigned in Ashtaroth and in Edrei (the same was left of the remnant of the Rephaim); for these did Moses strike, and drove them out.

Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hata siku hii ya leo. Yoshua 13:13

Nevertheless the children of Israel didn't drive out the Geshurites, nor the Maacathites: but Geshur and Maacath dwell in the midst of Israel to this day.

Lakini hakuwapa watu wa kabila ya Lawi urithi uwao wote; maana sadaka za Bwana, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia. Yoshua 13:14

Only to the tribe of Levi he gave no inheritance; the offerings of Yahweh, the God of Israel, made by fire are his inheritance, as he spoke to him.

Musa akawapa kabila ya wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao. Yoshua 13:15

Moses gave to the tribe of the children of Reuben according to their families.

Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba; Yoshua 13:16

Their border was from Aroer, that is on the edge of the valley of the Arnon, and the city that is in the middle of the valley, and all the plain by Medeba;

na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni; Yoshua 13:17

Heshbon, and all its cities that are in the plain; Dibon, and Bamoth Baal, and Beth Baal Meon,

na Yahasa, na Kedemothi, na Mefaathi; Yoshua 13:18

and Jahaz, and Kedemoth, and Mephaath,

na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde; Yoshua 13:19

and Kiriathaim, and Sibmah, and Zereth-shahar in the mount of the valley,

na Beth-peori, na nchi za matelemko ya Pisga, na Beth-yeshimothi; Yoshua 13:20

and Beth Peor, and the slopes of Pisgah, and Beth-jeshimoth,

na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao mashehe wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo. Yoshua 13:21

and all the cities of the plain, and all the kingdom of Sihon king of the Amorites, who reigned in Heshbon, whom Moses struck with the chiefs of Midian, Evi, and Rekem, and Zur, and Hur, and Reba, the princes of Sihon, who lived in the land.

Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua. Yoshua 13:22

Balaam also the son of Beor, the soothsayer, did the children of Israel kill with the sword among the rest of their slain.

Na mpaka wa wana wa Reubeni ulikuwa ni mto wa Yordani, na mpaka wake. Huo ndio urithi wa wana wa Reubeni sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake. Yoshua 13:23

The border of the children of Reuben was the Jordan, and the border [of it]. This was the inheritance of the children of Reuben according to their families, the cities and the villages of it.

Musa akawapa kabila ya Gadi, hao wana wa Gadi, kwa kadiri ya jamaa zao. Yoshua 13:24

Moses gave to the tribe of Gad, to the children of Gad, according to their families.

Mpaka wao ulikuwa ni Yazeri, na miji hiyo ya Gileadi, na nusu ya nchi ya wana wa Amoni, mpaka Aroeri uliokabili Raba; Yoshua 13:25

Their border was Jazer, and all the cities of Gilead, and half the land of the children of Ammon, to Aroer that is before Rabbah;

tena kutoka Heshboni mpaka Ramath-Mizpe, na Betonimu; tena kutoka Mahanaimu hata mpaka wa Debiri; Yoshua 13:26

and from Heshbon to Ramath Mizpeh, and Betonim; and from Mahanaim to the border of Debir;

tena katika bonde, Beth-haramu, na Bethnimira, na Sukothi, na Safoni, hiyo iliyosalia ya ufalme wa Sihoni mfalme wa Heshboni, yaani mto wa Yordani na mpaka wake, mpaka mwisho wa bahari ya Kinerethi ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki. Yoshua 13:27

and in the valley, Beth Haram, and Beth Nimrah, and Succoth, and Zaphon, the rest of the kingdom of Sihon king of Heshbon, the Jordan and the border [of it], to the uttermost part of the sea of Chinnereth beyond the Jordan eastward.

Huo ndio urithi wa wana wa Gadi sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake. Yoshua 13:28

This is the inheritance of the children of Gad according to their families, the cities and the villages of it.

Kisha Musa akawapa hao wa nusu ya kabila ya Manase urithi wao; ulikuwa ni wa hiyo nusu ya kabila ya wana wa Manase sawasawa na jamaa zao. Yoshua 13:29

Moses gave [inheritance] to the half-tribe of Manasseh: and it was for the half-tribe of the children of Manasseh according to their families.

Na mpaka wao ulikuwa kutoka huko Mahanaimu, Bashani yote, na ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini; Yoshua 13:30

Their border was from Mahanaim, all Bashan, all the kingdom of Og king of Bashan, and all the towns of Jair, which are in Bashan, sixty cities:

na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao. Yoshua 13:31

and half Gilead, and Ashtaroth, and Edrei, the cities of the kingdom of Og in Bashan, were for the children of Machir the son of Manasseh, even for the half of the children of Machir according to their families.

Hizi ndizo mirathi ambazo Musa alizigawanya katika nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya pili ya Yordani, kukabili Yeriko, upande wa mashariki. Yoshua 13:32

These are the inheritances which Moses distributed in the plains of Moab, beyond the Jordan at Jericho, eastward.

Lakini Musa hakuwapa kabila ya Lawi urithi uwao wote; yeye Bwana, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia. Yoshua 13:33

But to the tribe of Levi Moses gave no inheritance: Yahweh, the God of Israel, is their inheritance, as he spoke to them.