Yoshua 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yoshua 15 (Swahili) Joshua 15 (English)

Kura ya kabila ya wana wa Yuda kwa kuandama jamaa zao ilikuwa kufikilia hata mpaka wa Edomu, hata bara ya Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini. Yoshua 15:1

The lot for the tribe of the children of Judah according to their families was to the border of Edom, even to the wilderness of Zin southward, at the uttermost part of the south.

Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini; Yoshua 15:2

Their south border was from the uttermost part of the Salt Sea, from the bay that looks southward;

nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hata Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafikilia Adari, na kuzunguka kwendea Karka; Yoshua 15:3

and it went out southward of the ascent of Akrabbim, and passed along to Zin, and went up by the south of Kadesh-barnea, and passed along by Hezron, and went up to Addar, and turned about to Karka;

kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini. Yoshua 15:4

and it passed along to Azmon, and went out at the brook of Egypt; and the goings out of the border were at the sea: this shall be your south border.

Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani; Yoshua 15:5

The east border was the Salt Sea, even to the end of the Jordan. The border of the north quarter was from the bay of the sea at the end of the Jordan;

na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni; Yoshua 15:6

and the border went up to Beth Hoglah, and passed along by the north of Beth Arabah; and the border went up to the stone of Bohan the son of Reuben;

kisha mpaka ukaendelea hata Debiri kutoka bonde la Akori, vivyo ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hata ukafikilia maji ya Enshemeshi, na matokeo yake yalikuwa hapo Enrogeli; Yoshua 15:7

and the border went up to Debir from the valley of Achor, and so northward, looking toward Gilgal, that is over against the ascent of Adummim, which is on the south side of the river; and the border passed along to the waters of En Shemesh, and the goings out of it were at En Rogel;

kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufikilia ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini; Yoshua 15:8

and the border went up by the valley of the son of Hinnom to the side of the Jebusite southward (the same is Jerusalem); and the border went up to the top of the mountain that lies before the valley of Hinnom westward, which is at the uttermost part of the valley of Rephaim northward;

kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hata kufikilia chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hata kufikilia Baala (ndio Kiriath-yearimu); Yoshua 15:9

and the border extended from the top of the mountain to the spring of the waters of Nephtoah, and went out to the cities of Mount Ephron; and the border extended to Baalah (the same is Kiriath Jearim);

kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hata kilima Seiri, kisha ukaendelea hata upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukatelemkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna; Yoshua 15:10

and the border turned about from Baalah westward to Mount Seir, and passed along to the side of Mount Jearim on the north (the same is Chesalon), and went down to Beth-shemesh, and passed along by Timnah;

kisha mpaka ukatokea hata kufikilia upande wa Ekroni upande wa kaskazini; tena mpaka ulipigwa hata Shikroni, na kwendelea hata kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na matokeo ya mpaka yalikuwa baharini. Yoshua 15:11

and the border went out to the side of Ekron northward; and the border extended to Shikkeron, and passed along to Mount Baalah, and went out at Jabneel; and the goings out of the border were at the sea.

Na mpaka wa upande wa magharibi ulifikilia hata bahari kubwa, na mpaka wake. Huo ndio mpaka wa wana wa Yuda kwa kuzunguka kote kote sawasawa na jamaa zao. Yoshua 15:12

The west border was to the great sea, and the border [of it]. This is the border of the children of Judah round about according to their families.

Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama Bwana alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni). Yoshua 15:13

To Caleb the son of Jephunneh he gave a portion among the children of Judah, according to the commandment of Yahweh to Joshua, even Kiriath Arba, [which Arba was] the father of Anak (the same is Hebron).

Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki. Yoshua 15:14

Caleb drove out there the three sons of Anak: Sheshai, and Ahiman, and Talmai, the children of Anak.

Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi. Yoshua 15:15

He went up there against the inhabitants of Debir: now the name of Debir before was Kiriath Sepher.

Kalebu akasema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe. Yoshua 15:16

Caleb said, He who strikes Kiriath Sepher, and takes it, to him will I give Achsah my daughter as wife.

Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe. Yoshua 15:17

Othniel the son of Kenaz, the brother of Caleb, took it: and he gave him Achsah his daughter as wife.

Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini? Yoshua 15:18

It happened, when she came [to him], that she moved him to ask of her father a field: and she alighted from off her donkey; and Caleb said, What would you?

Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini. Yoshua 15:19

She said, Give me a blessing; for that you have set me in the land of the South, give me also springs of water. He gave her the upper springs and the lower springs.

Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao. Yoshua 15:20

This is the inheritance of the tribe of the children of Judah according to their families.

Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri; Yoshua 15:21

The uttermost cities of the tribe of the children of Judah toward the border of Edom in the South were Kabzeel, and Eder, and Jagur,

na Kina, na Dimona, na Adada; Yoshua 15:22

and Kinah, and Dimonah, and Adadah,

na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani; Yoshua 15:23

and Kedesh, and Hazor, and Ithnan,

na Zifu, na Telemu, na Bealothi; Yoshua 15:24

Ziph, and Telem, and Bealoth,

na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori); Yoshua 15:25

Hazor Hadattah, Kerioth, Hezron (the same is Hazor),

na Amamu, na Shema, na Molada; Yoshua 15:26

Amam, and Shema, and Moladah,

na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti; Yoshua 15:27

and Hazar Gaddah, and Heshmon, and Beth Pelet,

na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia; Yoshua 15:28

and Hazar Shual, and Beersheba, and Biziothiah,

na Baala, na Iyimu, na Esemu; Yoshua 15:29

Baalah, and Iim, and Ezem,

na Eltoladi, na Kesili, na Horma; Yoshua 15:30

and Eltolad, and Chesil, and Hormah,

na Siklagi, na Madmana, na Sansana; Yoshua 15:31

and Ziklag, and Madmannah, and Sansannah,

na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:32

and Lebaoth, and Shilhim, and Ain, and Rimmon: all the cities are twenty-nine, with their villages.

Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna, Yoshua 15:33

In the lowland, Eshtaol, and Zorah, and Ashnah,

na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu; Yoshua 15:34

and Zanoah, and En Gannim, Tappuah, and Enam,

na Yarmuthi, na Adulamu, na Soko, na Azeka; Yoshua 15:35

Jarmuth, and Adullam, Socoh, and Azekah,

na Shaarimu, na Adithaimu, na Gedera, na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:36

and Shaaraim, and Adithaim, and Gederah, and Gederothaim; fourteen cities with their villages.

Senani, na Hadasha, na Migdal-gadi; Yoshua 15:37

Zenan, and Hadashah, and Migdal-gad,

na Dilani, na Mispe, na Yoktheeli; Yoshua 15:38

and Dilean, and Mizpeh, and Joktheel,

na Lakishi, na Boskathi, na Egloni; Yoshua 15:39

Lachish, and Bozkath, and Eglon,

na Kaboni, na Lamasi, na Kithilishi; Yoshua 15:40

and Cabbon, and Lahmam, and Chitlish,

na Gederothi, na Beth-dagoni, na Naama, na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:41

and Gederoth, Beth Dagon, and Naamah, and Makkedah; sixteen cities with their villages.

Libna, na Etheri, na Ashani; Yoshua 15:42

Libnah, and Ether, and Ashan,

na Yifta, na Ashna, na Nesibu; Yoshua 15:43

and Iphtah, and Ashnah, and Nezib,

na Keila, na Akizibu, na Maresha; miji kenda, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:44

and Keilah, and Achzib, and Mareshah; nine cities with their villages.

Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake; Yoshua 15:45

Ekron, with its towns and its villages;

kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:46

from Ekron even to the sea, all that were by the side of Ashdod, with their villages.

Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake. Yoshua 15:47

Ashdod, its towns and its villages; Gaza, its towns and its villages; to the brook of Egypt, and the great sea, and the border [of it].

Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko; Yoshua 15:48

In the hill-country, Shamir, and Jattir, and Socoh,

na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri); Yoshua 15:49

and Dannah, and Kiriath Sannah (the same is Debir),

na Anabu, na Eshtemoa, na Animu; Yoshua 15:50

and Anab, and Eshtemoh, and Anim,

na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:51

and Goshen, and Holon, and Giloh; eleven cities with their villages.

Arabu, na Duma, na Eshani; Yoshua 15:52

Arab, and Dumah, and Eshan,

na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka; Yoshua 15:53

and Janim, and Beth Tappuah, and Aphekah,

na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:54

and Humtah, and Kiriath Arba (the same is Hebron), and Zior; nine cities with their villages.

Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta; Yoshua 15:55

Maon, Carmel, and Ziph, and Jutah,

na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa; Yoshua 15:56

and Jezreel, and Jokdeam, and Zanoah,

na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:57

Kain, Gibeah, and Timnah; ten cities with their villages.

Halhuli, na Bethsuri, na Gedori; Yoshua 15:58

Halhul, Beth Zur, and Gedor,

na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:59

and Maarath, and Beth Anoth, and Eltekon; six cities with their villages.

Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake. Yoshua 15:60

Kiriath Baal (the same is Kiriath Jearim), and Rabbah; two cities with their villages.

Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka; Yoshua 15:61

In the wilderness, Beth Arabah, Middin, and Secacah,

na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake. Yoshua 15:62

and Nibshan, and the City of Salt, and En Gedi; six cities with their villages.

Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo. Yoshua 15:63

As for the Jebusites, the inhabitants of Jerusalem, the children of Judah couldn't drive them out: but the Jebusites dwell with the children of Judah at Jerusalem to this day.