1
Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,
While Peter and John were speaking to the people, the priests and the captain of the temple guard and the Sadducees came up to them,
2
wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.
greatly disturbed that they were teaching the people and proclaiming in Jesus the resurrection of the dead.
3
Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.
They seized Peter and John, and because it was evening, they put them in custody until the next day.
4
Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.
But many who heard the message believed, and the number of men grew to about five thousand.
5
Hata asubuhi wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu,
The next day the rulers, elders, and scribes assembled in Jerusalem,
6
na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu.
along with Annas the high priest, Caiaphas, John, Alexander, and many others from the high priest’s family.
7
Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya?
They had Peter and John brought in and began to question them: “By what power or what name did you do this?”
8
Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,
Then Peter, filled with the Holy Spirit, said to them, “Rulers and elders of the people!
9
kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa,
If we are being examined today about a kind service to a man who was lame, to determine how he was healed,
10
jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.
then let this be known to all of you and to all the people of Israel: It is by the name of Jesus Christ of Nazareth, whom you crucified but whom God raised from the dead, that this man stands before you healed.
11
Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.
This Jesus is ‘the stone you builders rejected, which has become the cornerstone.’
12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Salvation exists in no one else, for there is no other name under heaven given to men by which we must be saved.”
13
Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
When they saw the boldness of Peter and John and realized that they were unschooled, ordinary men, they marveled and took note that these men had been with Jesus.
14
Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu.
And seeing the man who had been healed standing there with them, they had nothing to say in response.
15
Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri wao kwa wao,
So they ordered them to leave the Sanhedrin and then conferred together.
16
wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana.
“What shall we do with these men?” they asked. “It is clear to everyone living in Jerusalem that a remarkable miracle has occurred through them, and we cannot deny it.
17
Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu awaye yote kwa jina hili.
But to keep this message from spreading any further among the people, we must warn them not to speak to anyone in this name.”
18
Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.
Then they called them in again and commanded them not to speak or teach at all in the name of Jesus.
19
Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
But Peter and John replied, “Judge for yourselves whether it is right in God’s sight to listen to you rather than God.
20
maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
For we cannot stop speaking about what we have seen and heard.”
21
Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka;
After further threats they let them go. They could not find a way to punish them, because all the people were glorifying God for what had happened.
22
maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arobaini.
For the man who was miraculously healed was over forty years old.
23
Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee.
On their release, Peter and John returned to their own people and reported everything that the chief priests and elders had said to them.
24
Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
When the believers heard this, they lifted up their voices to God with one accord. “Sovereign Lord,” they said, “You made the heaven and the earth and the sea and everything in them.
25
nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
You spoke by the Holy Spirit through the mouth of Your servant, our father David: ‘Why do the nations rage and the peoples plot in vain?
26
Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
The kings of the earth take their stand and the rulers gather together against the Lord and against His Anointed One.’
27
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
In fact, this is the very city where Herod and Pontius Pilate conspired with the Gentiles and the people of Israel against Your holy servant Jesus, whom You anointed.
28
ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.
They carried out what Your hand and will had decided beforehand would happen.
29
Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote,
And now, Lord, consider their threats, and enable Your servants to speak Your word with complete boldness,
30
ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
as You stretch out Your hand to heal and perform signs and wonders through the name of Your holy servant Jesus.”
31
Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
After they had prayed, their meeting place was shaken, and they were all filled with the Holy Spirit and spoke the word of God boldly.
32
Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.
The multitude of believers was one in heart and soul. No one claimed that any of his possessions was his own, but they shared everything they owned.
33
Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
With great power the apostles continued to give their testimony about the resurrection of the Lord Jesus. And abundant grace was upon them all.
34
Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,
There were no needy ones among them, because those who owned lands or houses would sell their property, bring the proceeds from the sales,
35
wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.
and lay them at the apostles’ feet for distribution to anyone as he had need.
36
Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro,
Joseph, a Levite from Cyprus, whom the apostles called Barnabas (meaning Son of Encouragement),
37
alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.
sold a field he owned, brought the money, and laid it at the apostles’ feet.