Sifa Lyrics

Mimi ni Nani by Sifaeli Mwabuka cover art

Sifaeli Mwabuka - Mimi ni Nani Lyrics

Artist:
Sifaeli Mwabuka
Album:
Mimi ni Nani - Single
Official Release:
01 Jan 2018

Lyrics

Intro


Mimi ni nani Mungu wangu
Mimi ni nani?
Mimi ni nani Yesu wangu
Mimi ni nani?


(x2)


Verse 1


Umenipa upendeleo Baba
Mimi ni nani?
Umenipa upendeleo Baba
Mimi ni nani?


Kati ya wale wengi walikuwa wa kuomba
Mimi ni nani umenikumbuka Baba
Kati ya wale wengi walikuwa wa kuomba
Mimi ni nani umejibu maombi yangu


Wengi waliomba uzima umenipa mimi Baba
Mimi ni nani?
Ni wengi waliomba kuishi ata sasa hawako sasa 
Mimi ni nani?


Ni wengi waliomba amani ndoa zao kila siku vita
Mimi ni nani?
Ni wengi waliomba watoto kila siku wanalia
Mimi ni nani?


Prayer


Wengine wanalia Baba wanahitaji uponyaji
Baba wakumbuke
Wengine wanalia Baba wapi wapate furaha
Yesu wakumbuke


Wengine wanalia Baba wanahitaji watoto
Yesu wakumbuke
Wengine wanalia Baba wanahitaji amani 
Yesu usinyamaze 


Chorus


Mimi ni nani?(Aah)
Mimi ni nani?(Mimi ni nani Baba, oooh)
Mimi ni nani eeh Baba


Mimi ni nani?(Umenipendelea)
Mimi ni nani?(Umenipendelea)
Mimi ni nani eeh Baba


Mimi ni nani?(Na wengine wanalia)
Mimi ni nani?(Umenipa amani, Jehovah)
Mimi ni nani eeh Baba


Mimi ni nani?(Umenipa mke mwema)
Mimi ni nani?(Umenipa watoto)
Mimi ni nani?(Umenipa afya njema baba)
Mimi ni nani eeh Baba


Verse 2


Moyo wangu acha nikushukuru vile nilivyo Baba
Moyo wangu acha nikushukuru vile nilivyo Baba
Wengine hawapo umenifanya mimi niwepo
Acha nikushukuru


Vile nilivyo Baba umenifanya mimi nifurahi
Mimi ni nani?
Vyote nilivyonavyo Mungu wangu wewe umenipa
Mimi ni nani?


Umenipa mume mwema sio kwa ujanja wangu
Mimi ni nani?
Umenipa amani, ata sasa ninaimba 
Asante Mungu wangu


Outro


Eeeh...
Mimi ni nani?(Aah)
Mimi ni nani?(Mimi ni nani Baba, oooh)
Mimi ni nani eeh Baba


Mimi ni nani?(Umenipendelea)
Mimi ni nani?(Umenipendelea)
Mimi ni nani eeh Baba


Mimi ni nani?(Na wengine wanalia)
Mimi ni nani?(Umenipa amani, Jehovah)
Mimi ni nani eeh Baba


Mimi ni nani?(Umenipa mke mwema)
Mimi ni nani?(Umenipa watoto)
Mimi ni nani?(Umenipa afya njema baba)
Mimi ni nani eeh Baba


Credits & Song Information

Release Date
January 1, 2018
Community reviewed · Apple Music

Add song information · Add a supporting source

Video

Meaning & Inspiration

Mimi ni Nani is a reflection on undeserved favor and gratitude. Sifaeli Mwabuka moves from personal thanksgiving to concern for people still waiting for healing, children, peace, and joy, giving the repeated title question a humble rather than self-celebrating tone.