Sifa Lyrics

UNIREHEMU by Neema Gospel Choir cover art

Neema Gospel Choir - UNIREHEMU Lyrics

Artist:
Neema Gospel Choir

Lyrics

Unirehemu Mungu unirehemu,


Mimi Bwana MUNGU wangu naja,


Maana nafsi yangu imekukimbilia wewe Bwana,


Nafsi yangu ikatikati ya Simba


Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale. .


Na ndimi zao ni upanga mkali peke yangu mimi siwezi.


wameweka wavu iii kuninasa. .


Nafsi yangu imeinama


Wamechimba shimo mbele yangu, wametumbukia ndani yake.


(Bwana uniumbie moyo safi


iii ni-kutumikie )


Bwana uniumbie moyo safi


Ili ni-kutumikie


Nimekukimbilia wewe Bwana wangu,


Ili nisiahibike milele, kwa haki yako uniponye uniokoe.


Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,


Uwe kwangu baba yangu, niumbie moyo safi


Nakuhitaji 


Bwana Yesu maishani mwangu.


Niumbie moyo safi, Ili nitembee katika kweli yako


Hii ndo haja ya moyo wangu Bwana unisikie,


Niumbie moyo safi, niko mbele zako Bwana ninakuomba


Bwana uniumbie Moyo safi


Bwana uniumbie moyo safi,


Ili nikutumikie


Walinizunguka, naam walinizunguka, watesi wangu.


Lakini kwa jina la Yesu, naliwakatilia mbali.


Yesu wewe unaweza


Yesu wewe unatosha,


Watumishi wako wote.


Utawalinda na kuwatunza.


Video