Sifa Lyrics

Ipo Neema by Miriam Lukindo cover art

Miriam Lukindo - Ipo Neema Lyrics

Artist:
Miriam Lukindo

Lyrics

Umenikumbuka
Umenikumbuka
kwenye lile nililokuomba
leo umenikumbuka


Nasema ipo neema
Ipo neema 
kwenye kila ninalopitia 
Ipo neema


Nasema kipo kibali
kipo kibali
kwenye kila ninalo lifanya
kipo kibali


Tena kupo kuvushwa 
kupo kuvushwa 
kwenye kila ninalopitia 
kupo kuvushwa 


Nasema kupo kustareheshwa 
kupo kustareheshwa 
kwa yale ninayopitia
kupo kustareheshwa 


Yupo amalizae 
Nasema yupo amalizae 
kwenye yale ninayopitia
yupo amalizae 


Yeye aniponyae 
yupo aniponyae
kalituma neno lake ili nipone
upo aniponyae


Amenisamehe
Amenisamehe 
kwenye yale unayonihukumu kwayo
yeye amenisamehe


Damu yake imenipa uhalali
Damu yake imenipa uhalali
ilipomwagika pale msalabani
amenipa uhalali


Nasema mimi ni mwana wake 
mimi ni mwana wake
amenifungua na kuniweka huru
mimi ni mwana wake


Tena amenipa jina 
jina linipalo ushindi
ninapo liita napata ushindi
amenipa jina 


Yeye ndiye Bwana 
mashariki sikia 
yeye ndiye Bwana 
amelituma neno nami nipone
yeye ndiye Bwana 


Ndio maana nasema
Amen Hallelujah
Amen Hallelujah
najua uko nami hautaniacha
Amen Hallelujah


Video