Sifa Lyrics

Mungu Mkuu - Zaidi Ya Yote by Evelyn Wanjiru cover art

Evelyn Wanjiru - Mungu Mkuu - Zaidi Ya Yote Lyrics

Artist:
Evelyn Wanjiru

Lyrics

Zaidi ya yote
Utabaki kuwa Mungu mkuu
Alfa na Omega
Hubadiliki kamwe x2


Nikitazama nyuma na mbele
Naona ukuu wako
Kaskazini, kusini pia
naona ukuu wako
Magharibi nako mashariki pia
Naona ukuu wako


Zaidi ya yote
Utabaki kuwa Mungu mkuu
Alfa na Omega
Hubadiliki kamwe


Hakuna mkamilifu katika wanadamu
Zaidi ya ewe Mungu wangu
Kila goti lipigwe, kila ulimi ukiri
Kuwa wewe ni Mungu pekee


Zaidi ya yote
Utabaki kuwa Mungu mkuu
Alfa na Omega
Hubadiliki kamwe


Umenipigania vita vikali
Ambavyo mimi singeweza pekee yangu
Maadui waliniandama
Lakini ukawatawanya kwa njia saba
Usifiwe, uabudiwe


Zaidi ya yote
Utabaki kuwa Mungu mkuu
Alfa na Omega
Hubadiliki kamwe


@ EVERLYNE WANJIRU Zaidi Ya Yote


Translation:
Above all, you will still be God, The beginning and the end, you never change


Video