Christ Ambassadors - Yatupasa Kushukuru Lyrics

Yatupasa Kushukuru Lyrics

Hebu tu tafakari
Mungu atutendeayo
Jinsi anavyo tujali
Jinsi anayo nilinda
Uhai wetu upitao tumsifu ungalipo

Ni ya ajabu sana
Matendo ya bwana Mungu
Kinachosikitisha hatuyadhamini kabisa
Lakini bwana ni mwema kwetu
Hawezi tuacha

Japo mengi hayajakwisha 
Yatubidishayo tumshukuru Mungu wetu 
Japo twapita majaribu mengi 
Bado yapo mengi yakushukuriwa 
Eeh ee jiunge nasi 
Tulisisitize jambo hili la muhimu 
Yale yote tujiulizayo moyoni 
Majibu anayo Mungu wetu

Tuwapo safarini
Kifo kina tuandama
Tafakari safari zote
Kumbuka ile ajali
Ulifanya nini mpendwa ukatoka umzima

Ni ya ajabu sana
Matendo ya bwana Mungu
Kinachosikitisha hatuyadhamini kabisa
Lakini bwana ni mwema kwetu
Hawezi tuacha

Ni ya ajabu sana
Matendo ya bwana Mungu
Twapasa kushukuru kwa baraka anazotupa
Hakuna kitu wacha uhai ni yeye Mungu pekee

Tulalapo usiku
Twalala kama wafuu
Asubuhi kunapo kucha
Twadumu kuwa wazima
Ni ratiba yake tusifu
Ni mipango yake kwetu

Ni ya ajabu sana
Matendo ya bwana Mungu
Kinachosikitisha hatuyadhamini kabisa
Lakini bwana ni mwema kwetu
Hawezi tuacha

Ni ya ajabu sana
Matendo ya bwana Mungu
Twapasa kushukuru
Kwa baraka anazotupa
Hakuna kitu wacha uhai ni ye Mungu pekee

Ohh bwana ni mwema kwetu
Hawezi tuacha 3


Yatupasa Kushukuru Video

Yatupasa Kushukuru Lyrics -  Christ Ambassadors

Christ Ambassadors Songs

Related Songs