Kwetu Pazuri nimeshapakumbuka

Ninayo hamu kurudi nyumbani
Nyumbani kwetu ambapo hatutatengana
Hapo nyumbani kwetu hakuna makaburi
Wala hakuna vyandarua maana hakuna malaria
Kwetu ni pazuri ni pazuri nakuambia
Najua nawe ndugu yangu unayo hamu ya kufika huko

Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni

Hii dunina imejaa shida kama
Hujui nenda hospitali kaone
Lakini kwetu hakuna fani ya tabibu
Watakatifu watachuma
Majani ya mti wa uzima wawe na afya
Hawataugua magonjwa tabu
Tutaziacha zote hapa duniani


Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni

Mpendwa njoo turudi nyumbani
Asubuhi yaja tuyakimbie ya dunia
Atakayekosa hapo kweli ni hasara
Aya matatizo ni mitego ya shetani
Ili tushindwe kufika nyumbani
Kwetu pazuri
Lakini kwa jina jina la yesu
Tumemshinda tunaenda

Kwetu pazuri nimeshapakumbuka
Ninayo hamu kuishi na mwokozi wangu
Kwa amani na furaha tena ya ajabu
Sipati picha kwa watakaofika
kwetu mbinguni


Share:

Write a review of Kwetu Pazuri Nimeshapakumbuka:

0 Comments/Reviews


Christ Ambassadors

@christ-ambassadors

Bio

View all songs, albums & biography of Christ Ambassadors

View Profile

Bible Verses for Kwetu Pazuri nimeshapakumbuka

No verses added for this song, suggest a verse to be included in the comments section

Mp3 Songs & Download from iTunes

  • listen on Itunes Music