Nadia Mukami - Roho Mbaya Lyrics

Contents:

Roho Mbaya Lyrics

Nisha kuwa na rafiki zamani
Nikamwambia siri zangu za ndani
Akaziweka hadharani

Tena nikakuwa na rafiki wa kufa kuzikana
Pale pesa zilipokwisha naye akanikwepa
Nishachumbia mpenzi wangu
Nilipopata mimba akasema sio yangu

Leo mi nacheka na ninakula nao
Ila wananitendea
Ninajenga kwao ninaimba nao
Ila wamenigeukia

Mi nacheka na ninakula nao
Ila wananitendea
Ninajenga kwao ninaimba nao
Ila wamenigeukia

Roho mbaya, ila tu naishi nao wee
Roho mbaya, hata wengine damu zetu wee
Roho mbaya, ila tu naishi nao wee
Roho mbaya, hata wengine damu zetu wee

Wameniwekea mitego 
Nisisonge mbele
Wanatamani vyangu viwe vyao 
Wananionea gere

Wamengoja nisote wacheke
Nisote wasema
Wanangoja nishuke mziki waseme
Ooh waseme

Leo mi nacheka na ninakula nao
Ila wananitendea
Ninajenga kwao ninaimba nao
Ila wamenigeukia

Mi nacheka na ninakula nao
Ila wananitendea
Ninajenga kwao ninaimba nao
Ila wamenigeukia

Roho mbaya, ila tu naishi nao wee
Roho mbaya, hata wengine damu zetu wee
Roho mbaya, ila tu naishi nao wee
Roho mbaya, hata wengine damu zetu wee

Cheza kama umepata kazi wee
Cheza wakuone umenunua gari
Cheza kama umepata kanyumba wee
Cheza kama una pesa za kwako

Roho mbaya, ila tu naishi nao wee
Roho mbaya, hata wengine damu zetu wee
Roho mbaya, ila tu naishi nao wee
Roho mbaya, hata wengine damu zetu wee


Nadia Mukami Songs

Related Songs