Mambo ya Walawi 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 7 (Swahili) Leviticus 7 (English)

Na sheria ya hiyo sadaka ya hatia ni hii; ni takatifu sana. Mambo ya Walawi 7:1

"'This is the law of the trespass offering. It is most holy.

Wataichinja sadaka ya hatia pale pale waichinjapo sadaka ya kuteketezwa; na damu yake atainyunyiza katika madhabahu pande zote. Mambo ya Walawi 7:2

In the place where they kill the burnt offering, he shall kill the trespass offering; and its blood he shall sprinkle on the altar round about.

Katika sadaka hiyo atasongeza mafuta yake yote; yaani, mkia wake wenye mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, Mambo ya Walawi 7:3

He shall offer all of its fat: the fat tail, and the fat that covers the innards,

na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno chake, na kitambi kilicho katika ini, pamoja na figo zake mbili, hayo yote atayaondoa; Mambo ya Walawi 7:4

and the two kidneys, and the fat that is on them, which is by the loins, and the cover on the liver, with the kidneys, shall he take away;

na kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kuwa dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto; ni sadaka ya hatia. Mambo ya Walawi 7:5

and the priest shall burn them on the altar for an offering made by fire to Yahweh: it is a trespass offering.

Kila mtu mume miongoni mwa makuhani atakula katika sadaka hiyo; italiwa katika mahali patakatifu; ni takatifu sana. Mambo ya Walawi 7:6

Every male among the priests may eat of it. It shall be eaten in a holy place. It is most holy.

Kama hiyo sadaka ya dhambi ilivyo, na sadaka ya hatia ni vivyo; sheria yake ni moja; huyo kuhani afanyaye upatanisho kwayo, ndiye atakayekuwa nayo. Mambo ya Walawi 7:7

"'As is the sin offering, so is the trespass offering; there is one law for them. The priest who makes atonement with them shall have it.

Tena kuhani atakayesongeza sadaka ya kuteketezwa ya mtu awaye yote, huyo kuhani atatwaa awe nayo ngozi ya huyo mnyama wa sadaka ya kuteketezwa aliyemsongeza. Mambo ya Walawi 7:8

The priest who offers any man's burnt offering, even the priest shall have for himself the skin of the burnt offering which he has offered.

Na kila sadaka ya unga iliyookwa mekoni, na yote yaliyoandaliwa chunguni, au kaangoni, yote yatakuwa ya huyo kuhani aliyeyasongeza. Mambo ya Walawi 7:9

Every meal offering that is baked in the oven, and all that is dressed in the frying pan, and on the baking pan, shall be the priest's who offers it.

Na kila sadaka ya unga, kama umeandaliwa na mafuta, au kama ni mkavu, watautwaa wana wote wa Haruni kuutumia, kila mtu sawasawa. Mambo ya Walawi 7:10

Every meal offering, mixed with oil or dry, belongs to all the sons of Aaron, one as well as another.

Na sheria ya matoleo ya sadaka za amani, atakazosongeza mtu kwa Bwana, ni hii. Mambo ya Walawi 7:11

"'This is the law of the sacrifice of peace offerings, which one shall offer to Yahweh.

Kwamba aitoa kwa ajili ya shukrani, ndipo atakaposongeza pamoja na hiyo sadaka ya shukrani mikate isiyotiwa chachu, iliyoandaliwa na mafuta, na mikate ya kaki isiyochachwa iliyopakwa mafuta, na mikate ya unga mwembamba uliolowama mafuta. Mambo ya Walawi 7:12

If he offers it for a thanksgiving, then he shall offer with the sacrifice of thanksgiving unleavened cakes mixed with oil, and unleavened wafers anointed with oil, and cakes mixed with oil.

Ataleta matoleo yake, pamoja na mikate iliyotiwa chachu, na pamoja na sadaka zake za amani, kwa ajili ya shukrani. Mambo ya Walawi 7:13

With cakes of leavened bread he shall offer his offering with the sacrifice of his peace offerings for thanksgiving.

Na katika hayo atasongeza kimoja katika kila toleo kiwe sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana; itakuwa ni ya kuhani atakayeinyunyiza hiyo damu ya sadaka za amani. Mambo ya Walawi 7:14

Of it he shall offer one out of each offering for a heave offering to Yahweh. It shall be the priest's who sprinkles the blood of the peace offerings.

Na hiyo nyama ya sadaka zake za amani zilizochinjwa kwa ajili ya shukrani italiwa siku iyo hiyo ya matoleo yake; asisaze yo yote hata asubuhi. Mambo ya Walawi 7:15

The flesh of the sacrifice of his peace offerings for thanksgiving shall be eaten on the day of his offering. He shall not leave any of it until the morning.

Lakini kwamba hii sadaka ya matoleo yake ni nadhiri, au sadaka ya hiari, italiwa siku hiyo aliyoileta sadaka yake; kisha siku ya pili yake kitakachosalia kitaliwa; Mambo ya Walawi 7:16

"'But if the sacrifice of his offering is a vow, or a freewill offering, it shall be eaten on the day that he offers his sacrifice; and on the next day what remains of it shall be eaten:

lakini hicho kitakachosalia, katika hizo nyama za sadaka, hata siku ya tatu kitachomwa moto. Mambo ya Walawi 7:17

but what remains of the flesh of the sacrifice on the third day shall be burned with fire.

Tena kama nyama yo yote katika hiyo dhabihu yake ya sadaka za amani ikiliwa siku ya tatu, haitakubaliwa, wala haitahesabiwa kwake huyo mwenye kuisongeza; itakuwa ni machukizo, na mtu atakayeila atachukua uovu wake. Mambo ya Walawi 7:18

If any of the flesh of the sacrifice of his peace offerings is eaten on the third day, it will not be accepted, neither shall it be imputed to him who offers it. It will be an abomination, and the soul who eats any of it will bear his iniquity.

Tena nyama itakayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa; itachomwa moto. Na katika hiyo nyama nyingine, kila mtu aliye safi ana ruhusa kuila; Mambo ya Walawi 7:19

"'The flesh that touches any unclean thing shall not be eaten. It shall be burned with fire. As for the flesh, everyone who is clean may eat it;

lakini mtu huyo atakayekula katika nyama ya sadaka za amani, ambazo ni za Bwana, na unajisi wake akiwa nao juu yake, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. Mambo ya Walawi 7:20

but the soul who eats of the flesh of the sacrifice of peace offerings, that belongs to Yahweh, having his uncleanness on him, that soul shall be cut off from his people.

Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu cho chote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yo yote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za Bwana, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. Mambo ya Walawi 7:21

When anyone touches any unclean thing, the uncleanness of man, or an unclean animal, or any unclean abomination, and eats some of the flesh of the sacrifice of peace offerings, which belong to Yahweh, that soul shall be cut off from his people.'"

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 7:22

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yo yote, ya ng'ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi. Mambo ya Walawi 7:23

"Speak to the children of Israel, saying, 'You shall eat no fat, of ox, or sheep, or goat.

Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa ajili ya matumizi mengine; lakini msiyale kabisa. Mambo ya Walawi 7:24

The fat of that which dies of itself, and the fat of that which is torn of animals, may be used for any other service, but you shall in no way eat of it.

Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa Bwana kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake. Mambo ya Walawi 7:25

For whoever eats the fat of the animal, of which men offer an offering made by fire to Yahweh, even the soul who eats it shall be cut off from his people.

Tena msiile damu yo yote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote. Mambo ya Walawi 7:26

You shall not eat any blood, whether it is of bird or of animal, in any of your dwellings.

Mtu ye yote alaye damu, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. Mambo ya Walawi 7:27

Whoever it is who eats any blood, that soul shall be cut off from his people.'"

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 7:28

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa Israeli uwaambie, Yeye asongezaye dhabihu yake ya sadaka za amani kwa Bwana, atamletea Bwana matoleo yake, kutoka katika ile dhabihu ya sadaka zake za amani; Mambo ya Walawi 7:29

"Speak to the children of Israel, saying, 'He who offers the sacrifice of his peace offerings to Yahweh shall bring his offering to Yahweh out of the sacrifice of his peace offerings.

mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Bwana. Mambo ya Walawi 7:30

With his own hands he shall bring the offerings of Yahweh made by fire. He shall bring the fat with the breast, that the breast may be waved for a wave offering before Yahweh.

Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu; lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na cha wanawe. Mambo ya Walawi 7:31

The priest shall burn the fat on the altar, but the breast shall be Aaron's and his sons'.

Mguu wa nyuma wa upande wa kuume mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka katika hizo sadaka zenu za amani. Mambo ya Walawi 7:32

The right thigh you shall give to the priest for a heave offering out of the sacrifices of your peace offerings.

Katika wana wa Haruni, huyo atakayeisongeza damu ya sadaka za amani, na mafuta yake, yeye atapata mguu wa nyuma wa upande wa kuume kuwa sehemu yake. Mambo ya Walawi 7:33

He among the sons of Aaron who offers the blood of the peace offerings, and the fat, shall have the right thigh for a portion.

Kwa maana, hicho kidari cha kutikiswa, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli. Mambo ya Walawi 7:34

For the waved breast and the heaved thigh I have taken from the children of Israel out of the sacrifices of their peace offerings, and have given them to Aaron the priest and to his sons as their portion forever from the children of Israel.'"

Hii ndiyo sehemu ya Haruni, na sehemu ya wanawe, katika kutiwa mafuta kwao, katika hizo dhabihu zisongezwazo kwa Bwana kwa njia ya moto, siku hiyo aliyowaweka ili wamtumikie Bwana katika kazi ya ukuhani; Mambo ya Walawi 7:35

This is the anointing portion of Aaron, and the anointing portion of his sons, out of the offerings of Yahweh made by fire, in the day when he presented them to minister to Yahweh in the priest's office;

sehemu ambayo Bwana aliagiza wapewe na wana wa Israeli, siku hiyo aliyowatia mafuta. Ni haki yao ya milele katika vizazi vyao vyote. Mambo ya Walawi 7:36

which Yahweh commanded to be given them of the children of Israel, in the day that he anointed them. It is their portion forever throughout their generations.

Sheria ya sadaka ya kuteketezwa ni hii, na ya sadaka ya unga, na ya sadaka ya dhambi, na ya sadaka ya hatia, na ya kuwekwa wakfu, na ya sadaka za amani; Mambo ya Walawi 7:37

This is the law of the burnt offering, of the meal offering, and of the sin offering, and of the trespass offering, and of the consecration, and of the sacrifice of peace offerings;

ambazo Bwana alimwagiza Musa katika mlima wa Sinai, siku hiyo aliyowaagiza wana wa Israeli wamtolee Bwana matoleo yao, huko katika jangwa la Sinai. Mambo ya Walawi 7:38

which Yahweh commanded Moses in Mount Sinai, in the day that he commanded the children of Israel to offer their offerings to Yahweh, in the wilderness of Sinai.