Mambo ya Walawi 23 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 23 (Swahili) Leviticus 23 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 23:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Sikukuu za Bwana, ambazo mtazipigia mbiu kuwa ni makusanyiko matakatifu; hizi ni sikukuu zangu. Mambo ya Walawi 23:2

"Speak to the children of Israel, and tell them, 'The set feasts of Yahweh, which you shall proclaim to be holy convocations, even these are my set feasts.

Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu yote. Mambo ya Walawi 23:3

"'Six days shall work be done: but on the seventh day is a Sabbath of solemn rest, a holy convocation; you shall do no manner of work. It is a Sabbath to Yahweh in all your dwellings.

Sikukuu za Bwana ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake. Mambo ya Walawi 23:4

"'These are the set feasts of Yahweh, even holy convocations, which you shall proclaim in their appointed season.

Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni pasaka ya Bwana. Mambo ya Walawi 23:5

In the first month, on the fourteenth day of the month in the evening, is Yahweh's Passover.

Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba. Mambo ya Walawi 23:6

On the fifteenth day of the same month is the feast of unleavened bread to Yahweh. Seven days you shall eat unleavened bread.

Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi. Mambo ya Walawi 23:7

In the first day you shall have a holy convocation. You shall do no regular work.

Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. Mambo ya Walawi 23:8

But you shall offer an offering made by fire to Yahweh seven days. In the seventh day is a holy convocation: you shall do no regular work.'"

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 23:9

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtakapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; Mambo ya Walawi 23:10

"Speak to the children of Israel, and tell them, 'When you have come into the land which I give to you, and shall reap its the harvest, then you shall bring the sheaf of the first fruits of your harvest to the priest:

naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya Sabato kuhani atautikisa. Mambo ya Walawi 23:11

and he shall wave the sheaf before Yahweh, to be accepted for you. On the next day after the Sabbath the priest shall wave it.

Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. Mambo ya Walawi 23:12

On the day when you wave the sheaf, you shall offer a male lamb without blemish a year old for a burnt offering to Yahweh.

Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini. Mambo ya Walawi 23:13

The meal offering with it shall be two tenth parts of an ephah of fine flour mingled with oil, an offering made by fire to Yahweh for a sweet savor; and the drink offering with it shall be of wine, the fourth part of a hin.

Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote. Mambo ya Walawi 23:14

You shall eat neither bread, nor roasted grain, nor fresh grain, until this same day, until you have brought the offering of your God. This is a statute forever throughout your generations in all your dwellings.

Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya Sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia Sabato saba; Mambo ya Walawi 23:15

"'You shall count from the next day after the Sabbath, from the day that you brought the sheaf of the wave offering; seven Sabbaths shall be completed:

hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya. Mambo ya Walawi 23:16

even to the next day after the seventh Sabbath you shall number fifty days; and you shall offer a new meal offering to Yahweh.

Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa Bwana. Mambo ya Walawi 23:17

You shall bring out of your habitations two wave-loaves of two tenth parts of an ephah: they shall be of fine flour, they shall be baked with yeast, for first fruits to Yahweh.

Nanyi, pamoja na hiyo mikate, mtasongeza wana-kondoo saba, walio wakamilifu, wa mwaka wa kwanza, na ng'ombe mume mmoja, na kondoo waume wawili; watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, pamoja na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji, sadaka ya harufu ya kupendeza iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 23:18

You shall present with the bread seven lambs without blemish a year old, one young bull, and two rams. Yhey shall be a burnt offering to Yahweh, with their meal offering, and their drink offerings, even an offering made by fire, of a sweet aroma to Yahweh.

Nanyi mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili waume wa mwaka wa kwanza kuwa dhabihu ya sadaka za amani. Mambo ya Walawi 23:19

You shall offer one male goat for a sin offering, and two male lambs a year old for a sacrifice of peace offerings.

Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana, pamoja na wale wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa Bwana, wawe wa huyo kuhani. Mambo ya Walawi 23:20

The priest shall wave them with the bread of the first fruits for a wave offering before Yahweh, with the two lambs. They shall be holy to Yahweh for the priest.

Nanyi mtapiga mbiu siku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yo yote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu. Mambo ya Walawi 23:21

You shall make proclamation on the same day: there shall be a holy convocation to you; you shall do no regular work. This is a statute forever in all your dwellings throughout your generations.

Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini, na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Mambo ya Walawi 23:22

"'When you reap the harvest of your land, you shall not wholly reap into the corners of your field, neither shall you gather the gleanings of your harvest: you shall leave them for the poor, and for the foreigner. I am Yahweh your God.'"

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 23:23

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu. Mambo ya Walawi 23:24

"Speak to the children of Israel, saying, 'In the seventh month, on the first day of the month, shall be a solemn rest to you, a memorial of blowing of trumpets, a holy convocation.

Msifanye kazi yo yote ya utumishi; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 23:25

You shall do no regular work; and you shall offer an offering made by fire to Yahweh.'"

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 23:26

Yahweh spoke to Moses, saying,

Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. Mambo ya Walawi 23:27

"However on the tenth day of this seventh month is the day of atonement: it shall be a holy convocation to you, and you shall afflict yourselves; and you shall offer an offering made by fire to Yahweh.

Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Bwana, Mungu wenu. Mambo ya Walawi 23:28

You shall do no manner of work in that same day; for it is a day of atonement, to make atonement for you before Yahweh your God.

Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake. Mambo ya Walawi 23:29

For whoever it is who shall not deny himself in that same day; shall be cut off from his people.

Na mtu ye yote afanyaye kazi ya namna yo yote siku hiyo, mtu huyo nitamwangamiza atoke katika watu wake. Mambo ya Walawi 23:30

Whoever it is who does any manner of work in that same day, that person I will destroy from among his people.

Msifanye kazi ya namna yo yote; ni amri ya milele katika vizazi vyenu, katika makao yenu yote. Mambo ya Walawi 23:31

You shall do no manner of work: it is a statute forever throughout your generations in all your dwellings.

Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu. Mambo ya Walawi 23:32

It shall be a Sabbath of solemn rest for you, and you shall deny yourselves. In the ninth day of the month at evening, from evening to evening, you shall keep your Sabbath."

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 23:33

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana. Mambo ya Walawi 23:34

"Speak to the children of Israel, and say, 'On the fifteenth day of this seventh month is the feast of tents for seven days to Yahweh.

Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. Mambo ya Walawi 23:35

On the first day shall be a holy convocation: you shall do no regular work.

Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi. Mambo ya Walawi 23:36

Seven days you shall offer an offering made by fire to Yahweh. On the eighth day shall be a holy convocation to you; and you shall offer an offering made by fire to Yahweh. It is a solemn assembly; you shall do no regular work.

Sikukuu za Bwana ni hizi, ambazo mtazipigia mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu, ili mmsongezee Bwana sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na dhabihu, na sadaka za kinywaji, kila sadaka kwa siku yake; Mambo ya Walawi 23:37

"'These are the appointed feasts of Yahweh, which you shall proclaim to be holy convocations, to offer an offering made by fire to Yahweh, a burnt offering, and a meal offering, a sacrifice, and drink offerings, each on its own day;

zaidi ya hizo Sabato za Bwana, na zaidi ya matoleo yenu, na zaidi ya hizo nadhiri zenu zote, na zaidi ya sadaka zenu za hiari, ambazo mwampa Bwana. Mambo ya Walawi 23:38

besides the Sabbaths of Yahweh, and besides your gifts, and besides all your vows, and besides all your freewill offerings, which you give to Yahweh.

Lakini siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, hapo mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya Bwana muda wa siku saba; siku ya kwanza kutakuwa na kustarehe kabisa, na siku ya nane kutakuwa na kustarehe kabisa. Mambo ya Walawi 23:39

"'So on the fifteenth day of the seventh month, when you have gathered in the fruits of the land, you shall keep the feast of Yahweh seven days: on the first day shall be a solemn rest, and on the eighth day shall be a solemn rest.

Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za Bwana, Mungu wenu, muda wa siku saba. Mambo ya Walawi 23:40

You shall take on the first day the fruit of goodly trees, branches of palm trees, and boughs of thick trees, and willows of the brook; and you shall rejoice before Yahweh your God seven days.

Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa Bwana muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba. Mambo ya Walawi 23:41

You shall keep it a feast to Yahweh seven days in the year: it is a statute forever throughout your generations; you shall keep it in the seventh month.

Mtakaa katika vibanda muda wa siku saba; wazalia wote wa Israeli watakaa katika vibanda; Mambo ya Walawi 23:42

You shall dwell in booths seven days. All who are native-born in Israel shall dwell in booths,

ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa niliwaketisha wana wa Israeli katika vibanda, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri; mimi ndimi Bwana Mungu wenu. Mambo ya Walawi 23:43

that your generations may know that I made the children of Israel to dwell in booths, when I brought them out of the land of Egypt. I am Yahweh your God.'"

Naye Musa akawaambia wana wa Israeli hizo sikukuu za Bwana. Mambo ya Walawi 23:44

Moses declared to the children of Israel the appointed feasts of Yahweh.