Mambo ya Walawi 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mambo ya Walawi 21 (Swahili) Leviticus 21 (English)

Kisha Bwana akamwambia Musa, Nena na hao makuhani, wana wa Haruni, uwaambie, Mtu asijinajisi kwa ajili ya wafu katika watu wake; Mambo ya Walawi 21:1

Yahweh said to Moses, "Speak to the priests, the sons of Aaron, and say to them, 'A priest shall not defile himself for the dead among his people;

isipokuwa ni kwa ajili ya jamaa yake wa karibu, kwa ajili ya mama yake, na kwa ajili baba yake, na kwa ajili ya mwanawe, na kwa ajili ya binti yake, na kwa ajili ya nduguye mwanamume; Mambo ya Walawi 21:2

except for his relatives that are near to him: for his mother, for his father, for his son, for his daughter, for his brother,

na kwa ajili ya umbu lake aliye mwanamwali, aliye wa udugu kwake, ambaye hajaolewa na mume; ana ruhusa kujitia unajisi kwa ajili yake huyo. Mambo ya Walawi 21:3

and for his virgin sister who is near to him, who has had no husband; for her he may defile himself.

Asijitie unajisi, ijapokuwa ni mkubwa katika watu wake, hata akajinajisi. Mambo ya Walawi 21:4

He shall not defile himself, being a chief man among his people, to profane himself.

Wasijifanyie upaa kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje chale katika miili yao. Mambo ya Walawi 21:5

"'They shall not shave their heads, neither shall they shave off the corners of their beards, nor make any cuttings in their flesh.

Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za Bwana kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu. Mambo ya Walawi 21:6

They shall be holy to their God, and not profane the name of their God; for they offer the offerings of Yahweh made by fire, the bread of their God; therefore they shall be holy.

Wasimwoe mwanamke aliye kahaba, au huyo aliye mwenye unajisi; wala wasimwoe mwanamke aliyeachwa na mumewe; kwa kuwa yeye kuhani ni mtakatifu kwa Mungu wake. Mambo ya Walawi 21:7

"'They shall not marry a woman who is a prostitute, or profane; neither shall they marry a woman divorced from her husband: for he is holy to his God.

Kwa hiyo basi utamtakasa; kwa kuwa yeye husongeza chakula cha Mungu wako; atakuwa mtakatifu kwako wewe; kwa kuwa mimi Bwana niwatakasaye ninyi ni mtakatifu. Mambo ya Walawi 21:8

You shall sanctify him therefore; for he offers the bread of your God: he shall be holy to you: for I Yahweh, who sanctify you, am holy.

Na binti ya kuhani ye yote atakapojitia unajisi kwa ukahaba, amemtia unajisi baba yake; atachomwa moto. Mambo ya Walawi 21:9

"'The daughter of any priest, if she profanes herself by playing the prostitute, she profanes her father: she shall be burned with fire.

Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake; Mambo ya Walawi 21:10

"'He who is the high priest among his brothers, upon whose head the anointing oil is poured, and that is consecrated to put on the garments, shall not let the hair of his head hang loose, nor tear his clothes;

wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake; Mambo ya Walawi 21:11

neither shall he go in to any dead body, nor defile himself for his father, or for his mother;

wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi Bwana. Mambo ya Walawi 21:12

neither shall he go out of the sanctuary, nor profane the sanctuary of his God; for the crown of the anointing oil of his God is upon him. I am Yahweh.

Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake. Mambo ya Walawi 21:13

"'He shall take a wife in her virginity.

Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe. Mambo ya Walawi 21:14

A widow, or one divorced, or a woman who has been defiled, or a prostitute, these he shall not marry: but a virgin of his own people shall he take as a wife.

Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi Bwana nimtakasaye. Mambo ya Walawi 21:15

He shall not profane his seed among his people: for I am Yahweh who sanctifies him.'"

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Mambo ya Walawi 21:16

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. Mambo ya Walawi 21:17

"Say to Aaron, 'None of your seed throughout their generations who has a blemish, may approach to offer the bread of his God.

Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili, Mambo ya Walawi 21:18

For whatever man he is that has a blemish, he shall not draw near: a blind man, or a lame, or he who has a flat nose, or any deformity,

au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono, Mambo ya Walawi 21:19

or a man who has an injured foot, or an injured hand,

au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu; Mambo ya Walawi 21:20

or hunchbacked, or a dwarf, or one who has a defect in his eye, or an itching disease, or scabs, or who has damaged testicles;

mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za Bwana kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake. Mambo ya Walawi 21:21

no man of the seed of Aaron the priest, who has a blemish, shall come near to offer the offerings of Yahweh made by fire. Since has a blemish, he shall not come near to offer the bread of his God.

Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu. Mambo ya Walawi 21:22

He shall eat the bread of his God, both of the most holy, and of the holy.

Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye. Mambo ya Walawi 21:23

He shall not come near to the veil, nor come near to the altar, because he has a blemish; that he may not profane my sanctuaries, for I am Yahweh who sanctifies them.'"

Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote. Mambo ya Walawi 21:24

So Moses spoke to Aaron, and to his sons, and to all the children of Israel.