Waebrania 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 8 (Swahili) Hebrews 8 (English)

Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, Waebrania 8:1

Now in the things which we are saying, the main point is this. We have such a high priest, who sat down on the right hand of the throne of the Majesty in the heavens,

mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. Waebrania 8:2

a minister of the sanctuary, and of the true tabernacle, which the Lord pitched, not man.

Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. Waebrania 8:3

For every high priest is appointed to offer both gifts and sacrifices. Therefore it is necessary that this high priest also have something to offer.

Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; Waebrania 8:4

For if he were on earth, he would not be a priest at all, seeing there are priests who offer the gifts according to the law;

watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima. Waebrania 8:5

who serve a copy and shadow of the heavenly things, even as Moses was warned by God when he was about to make the tabernacle, for he said, "See, you shall make everything according to the pattern that was shown to you on the mountain."

Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Waebrania 8:6

But now he has obtained a more excellent ministry, by so much as he is also the mediator of a better covenant, which has been enacted on better promises.

Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili. Waebrania 8:7

For if that first covenant had been faultless, then no place would have been sought for a second.

Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; Waebrania 8:8

For finding fault with them, he said, "Behold, the days come," says the Lord, "That I will make a new covenant with the house of Israel and with the house of Judah;

Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. Waebrania 8:9

Not according to the covenant that I made with their fathers, In the day that I took them by the hand to lead them out of the land of Egypt; For they didn't continue in my covenant, And I disregarded them," says the Lord.

Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. Waebrania 8:10

"For this is the covenant that I will make with the house of Israel. After those days," says the Lord; "I will put my laws into their mind, I will also write them on their heart. I will be to them a God, And they will be to me a people.

Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao. Waebrania 8:11

They will not teach every man his fellow citizen,{TR reads "neighbor" instead of "fellow citizen"} Every man his brother, saying, 'Know the Lord,' For all will know me, From the least of them to the greatest of them.

Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. Waebrania 8:12

For I will be merciful to their unrighteousness. I will remember their sins and lawless deeds no more."

Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka. Waebrania 8:13

In that he says, "A new covenant," he has made the first old. But that which is becoming old and grows aged is near to vanishing away.