Waebrania 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 11 (Swahili) Hebrews 11 (English)

Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Waebrania 11:1

Now faith is assurance of things hoped for, proof of things not seen.

Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. Waebrania 11:2

For by this, the elders obtained testimony.

Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Waebrania 11:3

By faith, we understand that the universe has been framed by the word of God, so that what is seen has not been made out of things which are visible.

Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena. Waebrania 11:4

By faith, Abel offered to God a more excellent sacrifice than Cain, through which he had testimony given to him that he was righteous, God bearing witness with respect to his gifts; and through it he, being dead, still speaks.

Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu. Waebrania 11:5

By faith, Enoch was taken away, so that he wouldn't see death, and he was not found, because God translated him. For he has had testimony given to him that before his translation he had been well pleasing to God.

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Waebrania 11:6

Without faith it is impossible to be well pleasing to him, for he who comes to God must believe that he exists, and that he is a rewarder of those who seek him.

Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. Waebrania 11:7

By faith, Noah, being warned about things not yet seen, moved with godly fear, prepared an ark for the saving of his house, through which he condemned the world, and became heir of the righteousness which is according to faith.

Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. Waebrania 11:8

By faith, Abraham, when he was called, obeyed to go out to the place which he was to receive for an inheritance. He went out, not knowing where he went.

Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Waebrania 11:9

By faith, he lived as an alien in the land of promise, as in a land not his own, dwelling in tents, with Isaac and Jacob, the heirs with him of the same promise.

Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. Waebrania 11:10

For he looked for the city which has the foundations, whose builder and maker is God.

Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Waebrania 11:11

By faith, even Sarah herself received power to conceive, and she bore a child when she was past age, since she counted him faithful who had promised.

Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika. Waebrania 11:12

Therefore as many as the stars of the sky in multitude, and as innumerable as the sand which is by the sea shore, were fathered by one man, and him as good as dead.

Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. Waebrania 11:13

These all died in faith, not having received the promises, but having seen{TR adds "and being convinced of"} them and embraced them from afar, and having confessed that they were strangers and pilgrims on the earth.

Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Waebrania 11:14

For those who say such things make it clear that they are seeking after a country of their own.

Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. Waebrania 11:15

If indeed they had been thinking of that country from which they went out, they would have had enough time to return.

Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji. Waebrania 11:16

But now they desire a better country, that is, a heavenly one. Therefore God is not ashamed of them, to be called their God, for he has prepared a city for them.

Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee; Waebrania 11:17

By faith, Abraham, being tested, offered up Isaac. Yes, he who had gladly received the promises was offering up his one and only son;

naam, yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, Waebrania 11:18

even he to whom it was said, "In Isaac will your seed be called;"

akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu; akampata tena toka huko kwa mfano. Waebrania 11:19

accounting that God is able to raise up even from the dead. Figuratively speaking, he also did receive him back from the dead.

Kwa imani Isaka akawabariki Yakobo na Esau, hata katika habari ya mambo yatakayokuwa baadaye. Waebrania 11:20

By faith, Isaac blessed Jacob and Esau, even concerning things to come.

Kwa imani Yakobo, alipokuwa katika kufa, akambariki kila mmoja wa wana wa Yusufu, akaabudu akiegemea kichwa cha fimbo yake. Waebrania 11:21

By faith, Jacob, when he was dying, blessed each of the sons of Joseph, and worshiped, leaning on the top of his staff.

Kwa imani Yusufu, alipokuwa amekaribia mwisho wake, alitaja habari za kutoka kwao wana wa Israeli, akaagiza kwa habari ya mifupa yake. Waebrania 11:22

By faith, Joseph, when his end was near, made mention of the departure of the children of Israel; and gave instructions concerning his bones.

Kwa imani Musa, alipozaliwa, akafichwa miezi mitatu na wazazi wake, kwa sababu waliona kwamba ni mtoto mzuri; wala hawakuiogopa amri ya mfalme. Waebrania 11:23

By faith, Moses, when he was born, was hidden for three months by his parents, because they saw that he was a beautiful child, and they were not afraid of the king's commandment.

Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao; Waebrania 11:24

By faith, Moses, when he had grown up, refused to be called the son of Pharaoh's daughter,

akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo; Waebrania 11:25

choosing rather to share ill treatment with God's people, than to enjoy the pleasures of sin for a time;

akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Waebrania 11:26

accounting the reproach of Christ greater riches than the treasures of Egypt; for he looked to the reward.

Kwa imani akatoka Misri, asiogope ghadhabu ya mfalme; maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana. Waebrania 11:27

By faith, he left Egypt, not fearing the wrath of the king; for he endured, as seeing him who is invisible.

Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao. Waebrania 11:28

By faith, he kept the Passover, and the sprinkling of the blood, that the destroyer of the firstborn should not touch them.

Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa. Waebrania 11:29

By faith, they passed through the Red sea as on dry land. When the Egyptians tried to do so, they were swallowed up.

Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba. Waebrania 11:30

By faith, the walls of Jericho fell down, after they had been encircled for seven days.

Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. Waebrania 11:31

By faith, Rahab the prostitute, didn't perish with those who were disobedient, having received the spies in peace.

Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; Waebrania 11:32

What more shall I say? For the time would fail me if I told of Gideon, Barak, Samson, Jephthah, David, Samuel, and the prophets;

ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, Waebrania 11:33

who, through faith subdued kingdoms, worked out righteousness, obtained promises, stopped the mouths of lions,

walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Waebrania 11:34

quenched the power of fire, escaped the edge of the sword, from weakness were made strong, grew mighty in war, and turned to flight armies of aliens.

Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; Waebrania 11:35

Women received their dead by resurrection. Others were tortured, not accepting their deliverance, that they might obtain a better resurrection.

wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; Waebrania 11:36

Others were tried by mocking and scourging, yes, moreover by bonds and imprisonment.

walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; Waebrania 11:37

They were stoned. They were sawn apart. They were tempted. They were slain with the sword. They went around in sheep skins and in goat skins; being destitute, afflicted, ill-treated

(watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. Waebrania 11:38

(of whom the world was not worthy), wandering in deserts, mountains, caves, and the holes of the earth.

Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; Waebrania 11:39

These all, having had testimony given to them through their faith, didn't receive the promise,

kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi. Waebrania 11:40

God having provided some better thing concerning us, so that apart from us they should not be made perfect.