Waebrania 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 9 (Swahili) Hebrews 9 (English)

Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia. Waebrania 9:1

Now indeed even the first{TR adds "tabernacle"} covenant had ordinances of divine service, and an earthly sanctuary.

Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu. Waebrania 9:2

For there was a tabernacle prepared. In the first part were the lampstand, the table, and the show bread; which is called the Holy Place.

Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu, Waebrania 9:3

After the second veil was the tabernacle which is called the Holy of Holies,

yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; Waebrania 9:4

having a golden altar of incense, and the ark of the covenant overlaid on all sides with gold, in which was a golden pot holding the manna, Aaron's rod that budded, and the tables of the covenant;

na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja. Waebrania 9:5

and above it cherubim of glory overshadowing the mercy seat, of which things we can't now speak in detail.

Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada. Waebrania 9:6

Now these things having been thus prepared, the priests go in continually into the first tabernacle, accomplishing the services,

Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu. Waebrania 9:7

but into the second the high priest alone, once in the year, not without blood, which he offers for himself, and for the errors of the people.

Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama; Waebrania 9:8

The Holy Spirit is indicating this, that the way into the Holy Place wasn't yet revealed while the first tabernacle was still standing;

ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye, Waebrania 9:9

which is a symbol of the present age, where gifts and sacrifices are offered that are incapable, concerning the conscience, of making the worshipper perfect;

kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya. Waebrania 9:10

being only (with meats and drinks and various washings) fleshly ordinances, imposed until a time of reformation.

Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, Waebrania 9:11

But Christ having come as a high priest of the coming good things, through the greater and more perfect tabernacle, not made with hands, that is to say, not of this creation,

wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Waebrania 9:12

nor yet through the blood of goats and calves, but through his own blood, entered in once for all into the Holy Place, having obtained eternal redemption.

Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; Waebrania 9:13

For if the blood of goats and bulls, and the ashes of a heifer sprinkling those who have been defiled, sanctify to the cleanness of the flesh:

basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Waebrania 9:14

how much more will the blood of Christ, who through the eternal Spirit offered himself without blemish to God, cleanse your conscience from dead works to serve the living God?

Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. Waebrania 9:15

For this reason he is the mediator of a new covenant, since a death has occurred for the redemption of the transgressions that were under the first covenant, that those who have been called may receive the promise of the eternal inheritance.

Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. Waebrania 9:16

For where a last will and testament is, there must of necessity be the death of him who made it.

Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. Waebrania 9:17

For a will is in force where there has been death, for it is never in force while he who made it lives.

Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. Waebrania 9:18

Therefore even the first covenant has not been dedicated without blood.

Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, Waebrania 9:19

For when every commandment had been spoken by Moses to all the people according to the law, he took the blood of the calves and the goats, with water and scarlet wool and hyssop, and sprinkled both the book itself and all the people,

akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. Waebrania 9:20

saying, "This is the blood of the covenant which God has commanded you."

Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. Waebrania 9:21

Moreover he sprinkled the tabernacle and all the vessels of the ministry in like manner with the blood.

Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Waebrania 9:22

According to the law, nearly everything is cleansed with blood, and apart from shedding of blood there is no remission.

Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. Waebrania 9:23

It was necessary therefore that the copies of the things in the heavens should be cleansed with these; but the heavenly things themselves with better sacrifices than these.

Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; Waebrania 9:24

For Christ hasn't entered into holy places made with hands, which are representations of the true, but into heaven itself, now to appear in the presence of God for us;

wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake; Waebrania 9:25

nor yet that he should offer himself often, as the high priest enters into the holy place year by year with blood not his own,

kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. Waebrania 9:26

or else he must have suffered often since the foundation of the world. But now once at the end of the ages, he has been revealed to put away sin by the sacrifice of himself.

Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; Waebrania 9:27

Inasmuch as it is appointed for men to die once, and after this, judgment,

kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu. Waebrania 9:28

so Christ also, having been once offered to bear the sins of many, will appear a second time, without sin, to those who are eagerly waiting for him for salvation.