Waebrania 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 1 (Swahili) Hebrews 1 (English)

Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, Waebrania 1:1

God, having in the past spoken to the fathers through the prophets at many times and in various ways,

mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Waebrania 1:2

has at the end of these days spoken to us by his Son, whom he appointed heir of all things, through whom also he made the worlds.

Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; Waebrania 1:3

His Son is the radiance of his glory, the very image of his substance, and upholding all things by the word of his power, when he had by himself made purification for our sins, sat down on the right hand of the Majesty on high;

amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao. Waebrania 1:4

having become so much better than the angels, as he has inherited a more excellent name than they have.

Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana? Waebrania 1:5

For to which of the angels did he say at any time, "You are my Son, Today have I become your father?" and again, "I will be to him a Father, And he will be to me a Son?"

Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu. Waebrania 1:6

Again, when he brings in the firstborn into the world he says, "Let all the angels of God worship him."

Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto. Waebrania 1:7

Of the angels he says, "Who makes his angels winds, And his servants a flame of fire."

Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. Waebrania 1:8

but of the Son he says, "Your throne, O God, is forever and ever; The scepter of uprightness is the scepter of your Kingdom.

Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio. Waebrania 1:9

You have loved righteousness, and hated iniquity; Therefore God, your God, has anointed you with the oil of gladness above your fellows."

Na tena, Wewe,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako; Waebrania 1:10

And, "You, Lord, in the beginning, laid the foundation of the earth. The heavens are the works of your hands.

Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu; Nazo zote zitachakaa kama nguo, Waebrania 1:11

They will perish, but you continue. They all will grow old like a garment does.

Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma. Waebrania 1:12

As a mantle you will roll them up, And they will be changed; But you are the same. Your years will not fail."

Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Waebrania 1:13

But of which of the angels has he said at any time, "Sit at my right hand, Until I make your enemies the footstool of your feet?"

Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu? Waebrania 1:14

Aren't they all ministering spirits, sent out to do service for the sake of those who will inherit salvation?