Waebrania 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 7 (Swahili) Hebrews 7 (English)

Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; Waebrania 7:1

For this Melchizedek, king of Salem, priest of God Most High, who met Abraham returning from the slaughter of the kings and blessed him,

ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; Waebrania 7:2

to whom also Abraham divided a tenth part of all (being first, by interpretation, king of righteousness, and then also king of Salem, which is king of peace;

hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. Waebrania 7:3

without father, without mother, without genealogy, having neither beginning of days nor end of life, but made like the Son of God), remains a priest continually.

Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara. Waebrania 7:4

Now consider how great this man was, to whom even Abraham, the patriarch, gave a tenth out of the best spoils.

Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu. Waebrania 7:5

They indeed of the sons of Levi who receive the priest's office have a commandment to take tithes of the people according to the law, that is, of their brothers, though these have come out of the loins of Abraham,

Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi. Waebrania 7:6

but he whose genealogy is not counted from them has taken tithes of Abraham, and has blessed him who has the promises.

Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa. Waebrania 7:7

But without any dispute the less is blessed by the better.

Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai. Waebrania 7:8

Here people who die receive tithes, but there one receives tithes of whom it is testified that he lives.

Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi; Waebrania 7:9

So to say, through Abraham even Levi, who receives tithes, has paid tithes,

kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye. Waebrania 7:10

for he was yet in the loins of his father when Melchizedek met him.

Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni? Waebrania 7:11

Now if there was perfection through the Levitical priesthood (for under it the people have received the law), what further need was there for another priest to arise after the order of Melchizedek, and not be called after the order of Aaron?

Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike. Waebrania 7:12

For the priesthood being changed, there is of necessity a change made also in the law.

Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia madhabahu. Waebrania 7:13

For he of whom these things are said belongs to another tribe, from which no one has officiated at the altar.

Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani. Waebrania 7:14

For it is evident that our Lord has sprung out of Judah, about which tribe Moses spoke nothing concerning priesthood.

Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki; Waebrania 7:15

This is yet more abundantly evident, if after the likeness of Melchizedek there arises another priest,

asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo; Waebrania 7:16

who has been made, not after the law of a fleshly commandment, but after the power of an endless life:

maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki. Waebrania 7:17

for it is testified, "You are a priest forever, According to the order of Melchizedek."

Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake; Waebrania 7:18

For there is an annulling of a foregoing commandment because of its weakness and uselessness

(kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu. Waebrania 7:19

(for the law made nothing perfect), and a bringing in thereupon of a better hope, through which we draw near to God.

Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo, Waebrania 7:20

Inasmuch as he was not made priest without the taking of an oath

(maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani wa milele;) Waebrania 7:21

(for they indeed have been made priests without an oath), but he with an oath by him that says of him, "The Lord swore and will not change his mind, 'You are a priest forever, According to the order of Melchizedek'".

basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Waebrania 7:22

By so much has Jesus become the collateral of a better covenant.

Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; Waebrania 7:23

Many, indeed, have been made priests, because they are hindered from continuing by death.

bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Waebrania 7:24

But he, because he lives forever, has his priesthood unchangeable.

Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee. Waebrania 7:25

Therefore he is also able to save to the uttermost those who draw near to God through him, seeing he ever lives to make intercession for them.

Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu; Waebrania 7:26

For such a high priest was fitting for us: holy, guiltless, undefiled, separated from sinners, and made higher than the heavens;

ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake. Waebrania 7:27

who doesn't need, like those high priests, to daily offer up sacrifices, first for his own sins, and then for the sins of the people. For this he did once for all, when he offered up himself.

Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele. Waebrania 7:28

For the law appoints men as high priests who have weakness, but the word of the oath which came after the law appoints a Son forever who has been perfected.