1 Wafalme 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 7 (Swahili) 1st Kings 7 (English)

Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote. 1 Wafalme 7:1

Solomon was building his own house thirteen years, and he finished all his house.

Kwa kuwa aliijenga nyumba ya mwitu wa Lebanoni; mikono mia urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo. 1 Wafalme 7:2

For he built the house of the forest of Lebanon; the length of it was one hundred cubits, and the breadth of it fifty cubits, and the height of it thirty cubits, on four rows of cedar pillars, with cedar beams on the pillars.

Ikafunikwa juu kwa mwerezi juu ya mihimili arobaini na mitano, iliyokuwa juu ya nguzo; kumi na mitano kwa safu. 1 Wafalme 7:3

It was covered with cedar above over the forty-five beams, that were on the pillars; fifteen in a row.

Na madirisha yalikuwako safu tatu, mwangaza kuelekea mwangaza katika madaraja matatu. 1 Wafalme 7:4

There were beams in three rows, and window was over against window in three ranks.

Na milango yote na miimo ilikuwa ya mraba, ilivyoangaziwa; na mwangaza kuelekea mwangaza katika madaraja matatu. 1 Wafalme 7:5

All the doors and posts were made square with beams: and window was over against window in three ranks.

Akaifanya baraza ya nguzo; mikono hamsini urefu wake, na mikono thelathini upana wake; na ukumbi mbele yake; na nguzo na mihimili minene mbele yake. 1 Wafalme 7:6

He made the porch of pillars; the length of it was fifty cubits, and the breadth of it thirty cubits; and a porch before them; and pillars and a threshold before them.

Akaifanya baraza ya kiti cha enzi, ili ahukumu ndani yake, ndiyo baraza ya hukumu; nayo ikafunikwa mwerezi tangu sakafu mpaka dari. 1 Wafalme 7:7

He made the porch of the throne where he was to judge, even the porch of judgment: and it was covered with cedar from floor to floor.

Nayo nyumba yake atakayokalia, katika behewa nyingine iliyokuwa ndani kupita baraza, ilikuwa ya kazi kama hiyo. Tena akamjengea nyumba binti Farao, (ambaye Sulemani alikuwa amemwoa), mfano wa ile baraza. 1 Wafalme 7:8

His house where he was to dwell, the other court within the porch, was of the like work. He made also a house for Pharaoh's daughter (whom Solomon had taken as wife), like this porch.

Hizi zote zilikuwa za mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, yaliyokatwa kwa misumeno, ndani na nje, tangu msingi hata mawe ya juu, na nje vile vile hata behewa kuu. 1 Wafalme 7:9

All these were of costly stones, even of hewn stone, according to measure, sawed with saws, inside and outside, even from the foundation to the coping, and so on the outside to the great court.

Nao msingi ulikuwa wa mawe ya thamani, mawe makubwa, mawe mikono kumi, na mawe ya mikono minane. 1 Wafalme 7:10

The foundation was of costly stones, even great stones, stones of ten cubits, and stones of eight cubits.

Na juu kulikuwa na mawe ya thamani, mawe ya kuchongwa, sawasawa na cheo, na mierezi. 1 Wafalme 7:11

Above were costly stones, even hewn stone, according to measure, and cedar-wood.

Na behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba. 1 Wafalme 7:12

The great court round about had three courses of hewn stone, and a course of cedar beams; like as the inner court of the house of Yahweh, and the porch of the house.

Mfalme Sulemani akatuma watu kumleta Huramu kutoka Tiro. 1 Wafalme 7:13

King Solomon sent and fetched Hiram out of Tyre.

Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila ya Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, mstadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikilia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote. 1 Wafalme 7:14

He was the son of a widow of the tribe of Naphtali, and his father was a man of Tyre, a worker in brass; and he was filled with wisdom and understanding and skill, to work all works in brass. He came to king Solomon, and performed all his work.

Kwa maana alizifanyiza zile nguzo mbili za shaba, mikono kumi na minane kwenda juu kwake kila moja; na uzi wa mikono kumi na miwili kuizunguka nguzo hii au hii. 1 Wafalme 7:15

For he fashioned the two pillars of brass, eighteen cubits high apiece: and a line of twelve cubits compassed either of them about.

Akafanya taji mbili za shaba iliyoyeyushwa za kuwekwa juu ya vichwa vya nguzo; kwenda juu kwake taji moja mikono mitano, na mikono mitano kwenda juu kwake taji ya pili. 1 Wafalme 7:16

He made two capitals of molten brass, to set on the tops of the pillars: the height of the one capital was five cubits, and the height of the other capital was five cubits.

Kulikuwa na nyavu kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa taji zilizokuwako juu ya vichwa vya nguzo; saba kwa taji moja, na saba kwa taji ya pili 1 Wafalme 7:17

There were nets of checker-work, and wreaths of chain-work, for the capitals which were on the top of the pillars; seven for the one capital, and seven for the other capital.

Hivyo akazifanya nguzo; na kulikuwa na safu mbili za kuzunguka juu ya wavu mmoja, zifunike taji zilizokuwako juu ya vichwa vya nguzo; akafanya vivyo hivyo kwa taji ya pili. 1 Wafalme 7:18

So he made the pillars; and there were two rows round about on the one network, to cover the capitals that were on the top of the pillars: and so did he for the other capital.

Na taji zilizokuwa juu ya nguzo ukumbini zilikuwa za kazi ya mayungi, mikono minne. 1 Wafalme 7:19

The capitals that were on the top of the pillars in the porch were of lily-work, four cubits.

Kulikuwako tena taji juu ya nguzo mbili, karibu na uvimbe uliokuwako kando ya wavu; na makomamanga yalikuwa mia mbili, safu safu pande zote juu ya taji ya pili. 1 Wafalme 7:20

There were capitals above also on the two pillars, close by the belly which was beside the network: and the pomegranates were two hundred, in rows round about on the other capital.

Akazisimamisha nguzo ukumbini pa hekalu; akaisimamisha nguzo ya kuume, akaiita jina lake Yakini; akaisimamisha nguzo ya kushoto ,akaiita jina lake Boazi. 1 Wafalme 7:21

He set up the pillars at the porch of the temple: and he set up the right pillar, and called the name of it Jachin; and he set up the left pillar, and called the name of it Boaz.

Na juu ya nguzo kulikuwa na kazi ya mayungi; hivyo mambo ya nguzo yakatimia. 1 Wafalme 7:22

On the top of the pillars was lily-work: so was the work of the pillars finished.

Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ikaviringana, na mikono mitano ilikuwa kwenda juu kwake; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa. 1 Wafalme 7:23

He made the molten sea of ten cubits from brim to brim, round in compass, and the height of it was five cubits; and a line of thirty cubits compassed it round about.

Na chini ya ukingo wake kulikuwa na maboga yaliyoizunguka, kwa mikono kumi, yakiizunguka bahari; kulikuwa na safu mbili za hayo maboga, yakafanywa kalibuni hapo bahari ilipofanywa. 1 Wafalme 7:24

Under the brim of it round about there were buds which did compass it, for ten cubits, compassing the sea round about: the buds were in two rows, cast when it was cast.

Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 1 Wafalme 7:25

It stood on twelve oxen, three looking toward the north, and three looking toward the west, and three looking toward the south, and three looking toward the east; and the sea was set on them above, and all their hinder parts were inward.

Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu mbili. 1 Wafalme 7:26

It was a handbreadth thick: and the brim of it was worked like the brim of a cup, like the flower of a lily: it held two thousand baths.

Akayafanya yale matako kumi ya shaba; mikono minne urefu wa tako moja, na mikono minne upana wake, na mikono mitatu kwenda juu kwake. 1 Wafalme 7:27

He made the ten bases of brass; four cubits was the length of one base, and four cubits the breadth of it, and three cubits the height of it.

Na kazi ya matako ndiyo hii; yalikuwa na papi; na papi zilikuwa katikati ya vipandio; 1 Wafalme 7:28

The work of the bases was on this manner: they had panels; and there were panels between the ledges;

na juu ya papi zilizokuwa katikati ya vipandio kulikuwa na simba, na ng'ombe, na makerubi; na juu ya vipandio kulikuwa na tako; na chini ya simba na ng'ombe kulikuwa na masongo ya kazi ya kupembeza. 1 Wafalme 7:29

and on the panels that were between the ledges were lions, oxen, and cherubim; and on the ledges there was a pedestal above; and beneath the lions and oxen were wreaths of hanging work.

Kila tako lilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vipini vya shaba; na miguu yake minne ilikuwa na mataruma; chini ya birika yalikuwako mataruma ya kusubu, yenye masongo kila moja mbavuni. 1 Wafalme 7:30

Every base had four brazen wheels, and axles of brass; and the four feet of it had supports: beneath the basin were the supports molten, with wreaths at the side of each.

Na kinywa chake ndani ya taji na juu yake kilikuwa mkono mmoja; na kinywa chake kikaviringana kama kazi ya tako, mkono mmoja na nusu; tena juu ya kinywa chake kulikuwa na nakshi, na papi zao zilikuwa za mraba, wala hazikuviringana. 1 Wafalme 7:31

The mouth of it within the capital and above was a cubit: and the mouth of it was round after the work of a pedestal, a cubit and a half; and also on the mouth of it were engravings, and their panels were foursquare, not round.

Na magurudumu manne yalikuwa chini ya papi; na mikono ya magurudumu ndani ya tako; na kwenda juu kwake gurudumu moja mkono mmoja na nusu. 1 Wafalme 7:32

The four wheels were underneath the panels; and the axles of the wheels were in the base: and the height of a wheel was a cubit and half a cubit.

Na kazi ya magurudumu ilikuwa kama kazi ya gurudumu la gari; mikono yake, na maduara, na matindi, na vipande vya ndani, vyote vilikuwa vya kusubu. 1 Wafalme 7:33

The work of the wheels was like the work of a chariot wheel: their axles, and their rims, and their spokes, and their naves, were all molten.

Kulikuwa na mataruma manne katika pembe nne za tako moja; mataruma hayo ni kitu kimoja na tako lenyewe. 1 Wafalme 7:34

There were four supports at the four corners of each base: the supports of it were of the base itself.

Na juu ya tako kulikuwa na duara nusu mkono kwenda juu kwake; na juu ya tako mashikio yake na papi zake vilikuwa vya namna iyo hiyo. 1 Wafalme 7:35

In the top of the base was there a round compass half a cubit high; and on the top of the base the stays of it and the panels of it were of the same.

Akachora juu ya mabamba ya mashikio yake, na juu ya papi zake, makerubi, na simba, na mitende, moja moja kama ilivyokuwa nafasi, na masongo pande zote. 1 Wafalme 7:36

On the plates of the stays of it, and on the panels of it, he engraved cherubim, lions, and palm trees, according to the space of each, with wreaths round about.

Hivyo akayafanya yale matako kumi; yote yalikuwa ya kalibu moja, na cheo kimoja, na namna moja. 1 Wafalme 7:37

After this manner he made the ten bases: all of them had one casting, one measure, and one form.

Akafanya birika kumi za shaba; birika moja huingia bathi arobaini; na kila birika ilikuwa mikono minne; birika moja juu ya tako moja, katika yale matako kumi. 1 Wafalme 7:38

He made ten basins of brass: one basin contained forty baths; and every basin was four cubits; and on very one of the ten bases one basin.

Akayaweka yale matako, matano upande wa kuume wa nyumba, na matano upande wa kushoto wa nyumba; akaiweka ile bahari upande wa kuume wa nyumba upande wa mashariki, kuelekea kusini. 1 Wafalme 7:39

He set the bases, five on the right side of the house, and five on the left side of the house: and he set the sea on the right side of the house eastward, toward the south.

Tena Huramu akazifanya birika, na majembe, na mabakuli. Hivyo Huramu akazimaliza kazi zote alizomfanyia mfalme Sulemani katika nyumba ya Bwana; 1 Wafalme 7:40

Hiram made the basins, and the shovels, and the basins. So Hiram made an end of doing all the work that he worked for king Solomon in the house of Yahweh:

zile nguzo mbili, na vimbe mbili za taji zilikuwa juu ya nguzo; na nyavu mbili za kuzifunika hizo vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 1 Wafalme 7:41

the two pillars, and the two bowls of the capitals that were on the top of the pillars; and the two networks to cover the two bowls of the capitals that were on the top of the pillars;

na makomamanga mia nne ya zile nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika hizo vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 1 Wafalme 7:42

and the four hundred pomegranates for the two networks; two rows of pomegranates for each network, to cover the two bowls of the capitals that were on the pillars;

na yale matako kumi, na birika kumi juu ya matako; 1 Wafalme 7:43

and the ten bases, and the ten basins on the bases;

na ile bahari moja, na ng'ombe kumi na wawili chini ya ile bahari; 1 Wafalme 7:44

and the one sea, and the twelve oxen under the sea;

na masufuria, na majembe, na mabakuli; hata vyombo hivyo vyote, Huramu alivyomfanyia mfalme Sulemani, katika nyumba ya Bwana, vyote vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa. 1 Wafalme 7:45

and the pots, and the shovels, and the basins: even all these vessels, which Hiram made for king Solomon, in the house of Yahweh, were of burnished brass.

Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sarethani. 1 Wafalme 7:46

In the plain of the Jordan did the king cast them, in the clay ground between Succoth and Zarethan.

Sulemani akaviacha vyombo vyote visipimwe kwa kuwa vilikuwa vingi mno; wala uzito wa shaba haukujulikana. 1 Wafalme 7:47

Solomon left all the vessels [unweighed], because they were exceeding many: the weight of the brass could not be found out.

Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Bwana; madhabahu ya dhahabu, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya dhahabu; 1 Wafalme 7:48

Solomon made all the vessels that were in the house of Yahweh: the golden altar, and the table whereupon the show bread was, of gold;

na vinara vya taa, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu safi; na maua, na taa, na koleo ya dhahabu; 1 Wafalme 7:49

and the lampstands, five on the right side, and five on the left, before the oracle, of pure gold; and the flowers, and the lamps, and the tongs, of gold;

na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu safi; na bawaba za dhahabu, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu. 1 Wafalme 7:50

and the cups, and the snuffers, and the basins, and the spoons, and the fire pans, of pure gold; and the hinges, both for the doors of the inner house, the most holy place, and for the doors of the house, [to wit], of the temple, of gold.

Hivyo ikamalizika kazi yote Sulemani mfalme aliyoifanya katika nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vile vitu alivyovitakasa Daudi baba yake, yaani, fedha, na dhahabu, na vyombo; akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Bwana. 1 Wafalme 7:51

Thus all the work that king Solomon worked in the house of Yahweh was finished. Solomon brought in the things which David his father had dedicated, [even] the silver, and the gold, and the vessels, and put them in the treasuries of the house of Yahweh.