1 Wafalme 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 2 (Swahili) 1st Kings 2 (English)

Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema, 1 Wafalme 2:1

Now the days of David drew near that he should die; and he charged Solomon his son, saying,

Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; 1 Wafalme 2:2

I am going the way of all the earth: be you strong therefore, and show yourself a man;

uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako; 1 Wafalme 2:3

and keep the charge of Yahweh your God, to walk in his ways, to keep his statutes, [and] his commandments, and his ordinances, and his testimonies, according to that which is written in the law of Moses, that you may prosper in all that you do, and wherever you turn yourself.

ili Bwana afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli. 1 Wafalme 2:4

That Yahweh may establish his word which he spoke concerning me, saying, If your children take heed to their way, to walk before me in truth with all their heart and with all their soul, there shall not fail you (said he) a man on the throne of Israel.

Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake. 1 Wafalme 2:5

Moreover you know also what Joab the son of Zeruiah did to me, even what he did to the two captains of the hosts of Israel, to Abner the son of Ner, and to Amasa the son of Jether, whom he killed, and shed the blood of war in peace, and put the blood of war on his sash that was about his loins, and in his shoes that were on his feet.

Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia Ahera kwa amani. 1 Wafalme 2:6

Do therefore according to your wisdom, and don't let his gray head go down to Sheol in peace.

Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako. 1 Wafalme 2:7

But show kindness to the sons of Barzillai the Gileadite, and let them be of those who eat at your table; for so they came to me when I fled from Absalom your brother.

Hata, angalia, yuko pamoja nawe Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu, ndiye aliyenilaani kwa laana kuu siku ile nilipokwenda Mahanaimu; lakini akashuka kunilaki kule Yordani, nami nikamwapia kwa Bwana, nikamwambia, Mimi sitakuua kwa upanga. 1 Wafalme 2:8

Behold, there is with you Shimei the son of Gera, the Benjamite, of Bahurim, who cursed me with a grievous curse in the day when I went to Mahanaim; but he came down to meet me at the Jordan, and I swore to him by Yahweh, saying, I will not put you to death with the sword.

Basi kwa hiyo usimwachilie, kwa kuwa wewe u mtu wa akili; nawe utajua ikupasayo umtendee, na mvi zake utazishusha Ahera pamoja na damu. 1 Wafalme 2:9

Now therefore don't hold him guiltless, for you are a wise man; and you will know what you ought to do to him, and you shall bring his gray head down to Sheol with blood.

Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi. 1 Wafalme 2:10

David slept with his fathers, and was buried in the city of David.

Na siku alizotawala Daudi juu ya Israeli zilikuwa miaka arobaini; huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. 1 Wafalme 2:11

The days that David reigned over Israel were forty years; seven years reigned he in Hebron, and thirty-three years reigned he in Jerusalem.

Basi Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake; na ufalme wake ukawa imara sana. 1 Wafalme 2:12

Solomon sat on the throne of David his father; and his kingdom was established greatly.

Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akaja kwa Bath-sheba mamaye Sulemani. Naye akasema, Je! Umekuja kwa amani? 1 Wafalme 2:13

Then Adonijah the son of Haggith came to Bathsheba the mother of Solomon. She said, Come you peaceably? He said, Peaceably.

Naye akajibu, Kwa amani. Tena akasema, Nina shauri ninalotaka kukuambia. Naye akamwambia, Sema. 1 Wafalme 2:14

He said moreover, I have somewhat to tell you. She said, Say on.

Basi akasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili nimiliki mimi; walakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa Bwana. 1 Wafalme 2:15

He said, You know that the kingdom was mine, and that all Israel set their faces on me, that I should reign: however the kingdom is turned about, and is become my brother's; for it was his from Yahweh.

Basi sasa nina haja moja ninayokuomba, usinikataze hiyo. Naye akamwambia, Sema. 1 Wafalme 2:16

Now I ask one petition of you; don't deny me. She said to him, Say on.

Akasema, Nena, nakusihi, na Sulemani, mfalme, (kwa kuwa hawezi kukukataza neno), kwamba anioze Abishagi, Mshunami. 1 Wafalme 2:17

He said, Please speak to Solomon the king (for he will not tell you 'no'), that he give me Abishag the Shunammite as wife.

Naye Bath-sheba akasema, Vema; nitasema na mfalme kwa ajili yako. 1 Wafalme 2:18

Bathsheba said, Well; I will speak for you to the king.

Basi Bath-sheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kuume. 1 Wafalme 2:19

Bathsheba therefore went to king Solomon, to speak to him for Adonijah. The king rose up to meet her, and bowed himself to her, and sat down on his throne, and caused a throne to be set for the king's mother; and she sat on his right hand.

Ndipo akasema, Haja moja ndogo nakuomba; usinikataze. Mfalme akamwambia, Omba, mama; kwa kuwa siwezi kukukataza neno. 1 Wafalme 2:20

Then she said, I ask one small petition of you; don't deny me. The king said to her, Ask on, my mother; for I will not deny you.

Naye akasema, Nataka Adonia, ndugu yako, aozwe Abishagi, Mshunami. 1 Wafalme 2:21

She said, Let Abishag the Shunammite be given to Adonijah your brother as wife.

Akajibu mfalme Sulemani akamwambia mamaye, Na mbona wamtakia Adonia Abishagi, Mshunami? Umtakie na ufalme pia; kwa kuwa yeye ni ndugu yangu mkubwa; naam, umtakie yeye, na Abiathari kuhani, na Yoabu mwana wa Seruya. 1 Wafalme 2:22

King Solomon answered his mother, Why do you ask Abishag the Shunammite for Adonijah? ask for him the kingdom also; for he is my elder brother; even for him, and for Abiathar the priest, and for Joab the son of Zeruiah.

Ndipo mfalme Sulemani akaapa kwa Bwana, akasema, Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, isipokuwa Adonia amenena neno hili juu ya uhai wake mwenyewe. 1 Wafalme 2:23

Then king Solomon swore by Yahweh, saying, God do so to me, and more also, if Adonijah has not spoken this word against his own life.

Basi kwa hiyo, Bwana aishivyo, aliyenithibitisha na kunikalisha katika kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, akanifanyia nyumba, kama alivyoahidi, hakika atauawa leo hivi Adonia. 1 Wafalme 2:24

Now therefore as Yahweh lives, who has established me, and set me on the throne of David my father, and who has made me a house, as he promised, surely Adonijah shall be put to death this day.

Mfalme Sulemani akatuma kwa mkono wa Benaya mwana wa Yehoyada: naye akampiga, hata akafa. 1 Wafalme 2:25

King Solomon sent by Benaiah the son of Jehoiada; and he fell on him, so that he died.

Tena, mfalme akamwambia Abiathari kuhani, Enenda Anathothi mashambani kwako; kwa kuwa wastahili kufa; ila leo sikuui, kwa sababu wewe ulichukua sanduku la Bwana mbele ya Daudi baba yangu, na kwa sababu wewe uliteswa kwa mateso yote ya baba yangu. 1 Wafalme 2:26

To Abiathar the priest said the king, Get you to Anathoth, to your own fields; for you are worthy of death: but I will not at this time put you to death, because you bear the ark of the Lord Yahweh before David my father, and because you were afflicted in all in which my father was afflicted.

Hivyo Sulemani akamtoa Abiathari asiwe kuhani wa Bwana; ili alitimize neno la Bwana, alilonena juu ya nyumba ya Eli katika Shilo. 1 Wafalme 2:27

So Solomon thrust out Abiathar from being priest to Yahweh, that he might fulfill the word of Yahweh, which he spoke concerning the house of Eli in Shiloh.

Tena, habari zikamfikia Yoabu; kwa maana Yoabu alikuwa amemfuata Adonia, ingawa hakumfuata Absalomu. Yoabu akakimbilia Hemani kwa Bwana, akazishika pembe za madhabahu. 1 Wafalme 2:28

The news came to Joab; for Joab had turned after Adonijah, though he didn't turn after Absalom. Joab fled to the Tent of Yahweh, and caught hold on the horns of the altar.

Akaambiwa mfalme Sulemani ya kwamba, Yoabu amekimbilia Hemani kwa Bwana, naye, tazama, yuko madhabahuni. Ndipo Sulemani akamtuma Benaya, mwana wa Yehoyada, akisema, Enenda, umpige. 1 Wafalme 2:29

It was told king Solomon, Joab is fled to the Tent of Yahweh, and, behold, he is by the altar. Then Solomon sent Benaiah the son of Jehoiada, saying, Go, fall on him.

Basi Benaya akaja Hemani kwa Bwana, akamwambia, Mfalme asema hivi, Njoo utoke. Naye akajibu, La, sivyo; ila nitakufa papa hapa. Naye Benaya akamletea mfalme habari, akisema, Hivi ndivyo alivyonena Yoabu, na ndivyo alivyonijibu. 1 Wafalme 2:30

Benaiah came to the Tent of Yahweh, and said to him, Thus says the king, Come forth. He said, No; but I will die here. Benaiah brought the king word again, saying, Thus said Joab, and thus he answered me.

Mfalme akamwambia, Fanya alivyonena, umpige, ukamzike; ili uniondolee mimi na nyumba ya babangu damu aliyoimwaga Yoabu bure. 1 Wafalme 2:31

The king said to him, Do as he has said, and fall on him, and bury him; that you may take away the blood, which Joab shed without cause, from me and from my father's house.

Naye Bwana atamrudishia damu yake kichwani pake mwenyewe, kwa kuwa aliwapiga watu wawili wenye haki, na wema kuliko yeye, akawaua kwa upanga, wala babangu Daudi hakujua habari hiyo; yaani Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa, mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda. 1 Wafalme 2:32

Yahweh will return his blood on his own head, because he fell on two men more righteous and better than he, and killed them with the sword, and my father David didn't know it, [to wit], Abner the son of Ner, captain of the host of Israel, and Amasa the son of Jether, captain of the host of Judah.

Hivyo damu yao itarudi kichwani pa Yoabu, na kichwani pa wazao wake hata milele; ila kwa Daudi, na kwa wazao wake, na kwa nyumba yake, na kwa kiti chake cha enzi, kutakuwa na amani hata milele kutoka kwa Bwana. 1 Wafalme 2:33

So shall their blood return on the head of Joab, and on the head of his seed forever: but to David, and to his seed, and to his house, and to his throne, shall there be peace for ever from Yahweh.

Ndipo Benaya, mwana wa Yehoyada, akapanda, akampiga, akamwua; naye akazikwa katika nyumba yake mwenyewe iliyoko nyikani. 1 Wafalme 2:34

Then Benaiah the son of Jehoiada went up, and fell on him, and killed him; and he was buried in his own house in the wilderness.

Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, mahali pake juu ya jeshi; na Sadoki, kuhani, mfalme akamweka mahali pa Abiathari. 1 Wafalme 2:35

The king put Benaiah the son of Jehoiada in his room over the host; and Zadok the priest did the king put in the room of Abiathar.

Tena, mfalme akatuma watu akamwita Shimei, akamwambia, Ujijengee nyumba humu Yerusalemu, ukae ndani yake, wala usitoke humo kwenda mahali po pote. 1 Wafalme 2:36

The king sent and called for Shimei, and said to him, Build yourself a house in Jerusalem, and dwell there, and don't go forth from there any where.

Kwa kuwa siku ile ya kutoka kwako, na kuvuka kijito Kidroni, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe. 1 Wafalme 2:37

For on the day you go out, and pass over the brook Kidron, know you for certain that you shall surely die: your blood shall be on your own head.

Naye Shimei akamwambia mfalme, Neno hili ni jema; kama alivyosema bwana wangu mfalme, ndivyo atakavyofanya mtumwa wako. Basi Shimei akakaa Yerusalemu siku nyingi. 1 Wafalme 2:38

Shimei said to the king, The saying is good: as my lord the king has said, so will your servant do. Shimei lived in Jerusalem many days.

Ikawa miaka mitatu ilipokwisha, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi, mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Wakamwambia Shimei, wakasema, Angalia, watumwa wako wako huko Gathi. 1 Wafalme 2:39

It happened at the end of three years, that two of the servants of Shimei ran away to Achish, son of Maacah, king of Gath. They told Shimei, saying, Behold, your servants are in Gath.

Shimei akaondoka, akatandika punda wake, akaenda Gathi kwa Akishi, ili kuwatafuta watumwa wake. Akaenda Shimei, akawaleta watumwa wake toka Gathi. 1 Wafalme 2:40

Shimei arose, and saddled his donkey, and went to Gath to Achish, to seek his servants; and Shimei went, and brought his servants from Gath.

Naye Sulemani akaambiwa, ya kwamba Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi, na kurudi tena. 1 Wafalme 2:41

It was told Solomon that Shimei had gone from Jerusalem to Gath, and was come again.

Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa Bwana, na kukushuhudia, kusema, Siku ile ya kutoka kwako ukienda mahali po pote, ujue hakika ya kwamba kufa utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema? 1 Wafalme 2:42

The king sent and called for Shimei, and said to him, Didn't I adjure you by Yahweh, and protest to you, saying, Know for certain, that on the day you go out, and walk abroad any where, you shall surely die? and you said to me, The saying that I have heard is good.

Mbona basi hukukishika kiapo cha Bwana, na amri niliyokuagiza? 1 Wafalme 2:43

Why then have you not kept the oath of Yahweh, and the commandment that I have charged you with?

Tena, mfalme akamwambia Shimei, Umejua uovu wote uliouona moyoni mwako, uliomtenda Daudi baba yangu; basi kwa hiyo Bwana atakurudishia uovu wako kichwani pako mwenyewe. 1 Wafalme 2:44

The king said moreover to Shimei, You know all the wickedness which your heart is privy to, that you did to David my father: therefore Yahweh shall return your wickedness on your own head.

Ila mfalme Sulemani atakuwa amebarikiwa, na kiti cha enzi cha Daudi kitathibitika mbele za Bwana hata milele. 1 Wafalme 2:45

But king Solomon shall be blessed, and the throne of David shall be established before Yahweh forever.

Basi mfalme akamwamuru Benaya, mwana wa Yehoyada; naye akatoka, akampiga, hata akafa. Nao ufalme ukawa imara mkononi mwa Sulemani. 1 Wafalme 2:46

So the king commanded Benaiah the son of Jehoiada; and he went out, and fell on him, so that he died. The kingdom was established in the hand of Solomon.