1 Wafalme 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 19 (Swahili) 1st Kings 19 (English)

Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 1 Wafalme 19:1

Ahab told Jezebel all that Elijah had done, and withal how he had slain all the prophets with the sword.

Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. 1 Wafalme 19:2

Then Jezebel send a messenger to Elijah, saying, So let the gods do to me, and more also, if I don't make your life as the life of one of them by tomorrow about this time.

Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko. 1 Wafalme 19:3

When he saw that, he arose, and went for his life, and came to Beersheba, which belongs to Judah, and left his servant there.

Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu. 1 Wafalme 19:4

But he himself went a day's journey into the wilderness, and came and sat down under a juniper tree: and he requested for himself that he might die, and said, It is enough; now, O Yahweh, take away my life; for I am not better than my fathers.

Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 1 Wafalme 19:5

He lay down and slept under a juniper tree; and, behold, an angel touched him, and said to him, Arise and eat.

Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. 1 Wafalme 19:6

He looked, and, behold, there was at his head a cake baked on the coals, and a jar of water. He ate and drink, and laid him down again.

Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 1 Wafalme 19:7

The angel of Yahweh came again the second time, and touched him, and said, Arise and eat, because the journey is too great for you.

Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu. 1 Wafalme 19:8

He arose, and ate and drink, and went in the strength of that food forty days and forty nights to Horeb the Mount of God.

Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 1 Wafalme 19:9

He came there to a cave, and lodged there; and, behold, the word of Yahweh came to him, and he said to him, What are you doing here, Elijah?

Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe. 1 Wafalme 19:10

He said, I have been very jealous for Yahweh, the God of hosts; for the children of Israel have forsaken your covenant, thrown down your altars, and slain your prophets with the sword: and I, even I only, am left; and they seek my life, to take it away.

Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 1 Wafalme 19:11

He said, Go forth, and stand on the mountain before Yahweh. Behold, Yahweh passed by, and a great and strong wind tore the mountains, and broke in pieces the rocks before Yahweh; but Yahweh was not in the wind: and after the wind an earthquake; but Yahweh was not in the earthquake:

na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. 1 Wafalme 19:12

and after the earthquake a fire; but Yahweh was not in the fire: and after the fire a still small voice.

Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya? 1 Wafalme 19:13

It was so, when Elijah heard it, that he wrapped his face in his mantle, and went out, and stood in the entrance of the cave. Behold, there came a voice to him, and said, What are you doing here, Elijah?

Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu waiondoe. 1 Wafalme 19:14

He said, I have been very jealous for Yahweh, the God of hosts; for the children of Israel have forsaken your covenant, thrown down your altars, and slain your prophets with the sword; and I, even I only, am left; and they seek my life, to take it away.

Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu. 1 Wafalme 19:15

Yahweh said to him, Go, return on your way to the wilderness of Damascus: and when you come, you shall anoint Hazael to be king over Syria;

Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako. 1 Wafalme 19:16

and Jehu the son of Nimshi shall you anoint to be king over Israel; and Elisha the son of Shaphat of Abel Meholah shall you anoint to be prophet in your room.

Na itakuwa atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na upanga wa Yehu, Elisha atamwua. 1 Wafalme 19:17

It shall happen, that he who escapes from the sword of Hazael shall Jehu kill; and he who escapes from the sword of Jehu shall Elisha kill.

Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu. 1 Wafalme 19:18

Yet will I leave [me] seven thousand in Israel, all the knees which have not bowed to Baal, and every mouth which has not kissed him.

Basi, akaondoka huko, akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima, mwenye jozi za ng'ombe kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa pamoja na lile la kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa vazi lake juu yake. 1 Wafalme 19:19

So he departed there, and found Elisha the son of Shaphat, who was plowing, with twelve yoke [of oxen] before him, and he with the twelfth: and Elijah passed over to him, and cast his mantle on him.

Naye akawaacha ng'ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Enenda, urudi; ni nini niliyokutendea? 1 Wafalme 19:20

He left the oxen, and ran after Elijah, and said, Let me, I pray you, kiss my father and my mother, and then I will follow you. He said to him, Go back again; for what have I done to you?

Akarudi akiacha kumfuata, akatwaa lile jozi la ng'ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya ng'ombe, akawapa watu, wakala. Kisha akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.

1 Wafalme 19:21

He returned from following him, and took the yoke of oxen, and killed them, and boiled their flesh with the instruments of the oxen, and gave to the people, and they ate. Then he arose, and went after Elijah, and ministered to him.